Wasifu wa Julius Nyerere: Matatizo katika historia ya TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WASIFU WA JULIUS NYERERE: MATATIZO BADO YAPO KATIKA USAHIHI WA HISTORIA YA TANU

Mwananyamala nje ya nyumba ya Mzee Mwinjuma Mwinyikambi kumeweka kibao kinachosema kuwa TANU iliasisiwa ndani ya nyumba hiyo tarehe 7 Julai 1954.

Juu ya kibao pameandikwa: ''Kumbukumbu'' na chini yake ndiyo yako maneno hayo kuwa ndani ya nyumba hiyo ndimo ilipoasisiwa TANU.

Bahati mbaya hakuna popote palipoandikwa kibao hicho kimewekea na mamlaka ipi.

Sina taarifa ni lini kibao hicho kimewekwa lakini toka udogoni kwangu nikimfahamu Mzee Mwinjuma Mwinyikambi na mkewe bibi yetu Bi. Fatuma bint Agombe mwanamke wa Kingazija.

Bi. Fatuma alikuwa na madrasa hapo nyumbani kwake na akilea watoto yatima.

Mzee Mwinjuma alikuwa mtu maarufu sana pale Mwananyamala na Dar es salaam nzima.

Mzee Mwinjuma alikuwa na ardhi kubwa kuzunguka hii nyumba yake, ardhi iliyojaa miembe na minazi.

Mzee Mwinjuma ni kati ya wazee waliokuwa na sauti kubwa ndani ya Baraza la Wazee wa TANU.

Lakini hili la kuwa TANU iliiasisiwa nyumbani kwake lina tatizo kwa kukosa ushahidi katika historia ya kuasisiwa kwa chama hicho.

Mipango yote ya siasa wakati ule katika miaka ya 1950 wakati wa TAA kuelekea kuundwa kwa TANU ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes aliyekuwa Kaimu Rais wa TAA na Katibu kuazina 1951 - 1953 alipokuwa Kaimu Rais wa TAA, Rais akiwa Julius Nyerere kufuatia uchaguzi wa TAA wa uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 19 April, 1953.

Nyumba hii ya Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu ndiyo nyumba Nyerere alipokutana na Abdul Sykes kwa mara ya kwanza mwaka wa 1952 na ndiyo nyumba alikuja kuishi baada ya kuacha kazi ya ualimu mwaka wa 1955.

Inashangaza kuwa iwe TANU isianzishwe kwenye nyumba hii ije kuanzishwa Mwananyamala nyumbani kwa Mwinjuma Mwinyikambi.

Historia ya TANU imejaa vitendawili vingi sana.

Picha ya kwanza nyumba ya Mzee Mwinjuma Mwinyikambi ikiwa na kibao kinachosema kuwa TANU ndipo ilipoanzishwa hapo.

Picha ya pili nyumba ya Abdul Sykes ambapo harakati za kuundwa kwa TANU zilipokuwa zikifanyika.

Nyumba hii imefanyiwa ukarabati mkubwa lakini sehemu mbili za nyumba hii zilibakizwa.

Sehemu ya mkono wa kulia iliyoko Mtaa wa Sikukuu ndiyo sehemu alipoishi Mwalimu Nyerere kwa miezi mitatu baada ya kuacha kazi na sehemu ya mkono wa kushoto Mtaa wa Stanley ndipo ilipokuwa nyumba kubwa akiishi Abdul Sykes.

Picha ya tatu nyumba ya Abdul Sykes kama ilivyo sasa baada ya kuvunjwa na kujengwa ghorofa.
 
Attachments

  • NYUMBA YA MWINJUMA MWINYIKAMBI MWANANYAMALA.jpg
    NYUMBA YA MWINJUMA MWINYIKAMBI MWANANYAMALA.jpg
    27.6 KB · Views: 4
  • NYUMBA YA ABDUL SYKES ALIYOISHI NA NYERERE 1955.jpg
    NYUMBA YA ABDUL SYKES ALIYOISHI NA NYERERE 1955.jpg
    72.5 KB · Views: 5
  • NYUMBA YA ABDUL SYKES ILIVYO SASA.jpg
    NYUMBA YA ABDUL SYKES ILIVYO SASA.jpg
    28.7 KB · Views: 4
Mohamed Said Ahsante kwa historia nzuri ,naomba kufahamu kama una vitabu umeshaandika kama vipo navipataje mi niko Moshi, Kilimanjaro
 
Agogwe,
Nimeandika vitabu kadhaa peke yangu na vingine na waandishi wengine nje ya Tanzania na Afrika.

Bahati mbaya mimi ni mwandishi sihusiki na usambazaji wa vitabu lakini vitabu vyangu vinapatikana Dar es Salaam Ibn Hazm Media Centre, Msikiti wa Mtoro, Manyema na Mtambani.
 
nyerere alikaa nyumbani kwa abdul sykes, lakini TANU iliasisiwa kwenye ofisi zake, sio nyumbani kwa abdul
 
Laki...
Nyumba ya Abdul Sykes ndiyo ikikuwa pia kituo cha harakati za kupambana dhulma za ukoloni toka wakati baba yake Mzee Kleist yu hai.

Nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey na Sikukuu ndiyo tunaweza kusema ndicho kituo cha kwanza katika safari ya Mwalimu Nyerere kuelekea kule ambako alihitimisha safari yake katika kuiongoza Tanganyika kisha Tanzania.

Wengi hawafahamu kuwa Abdul Sykes na Dossa Aziz ndiyo walimpeleka Nyerere Zanzibar kumtambulisha kwa Abeid Amani Karume.

Hapa katika nyumba hii ndipo ulipojengwa msingi wa umaarufu wa Nyerere ambao TANU uliusambaza kwanza Dar es Salaam ndani ya Soko la Kariakoo kisha katika majimbo.

Nyumba hii ina historia ya pekee katika nyumba zote za Dar es Salaam.

Hii ilikuwa nyumba ya mwisho kwa baba yake Abdul, Mzee Kleist kujenga na aliijenga mwaka wa 1942 alipostaafu kazi Tanganyika Railways.

Hapa nyumbani kwake ndipo ilipokuwa barza kubwa kabisa ya wazee maarufu wa Dar es Salaam walipokutana jioni kwa mazungumzo na kunywa kahawa.

Kila deli lililopita pale liliitwa na wazee wakawa wanakunywa vikombe na vikombe vya kahawa hadi jua kuzama wakaagana na kurejea majumbani kwao.

Baada ya kifo cha Mzee Kleist na barza pia ikafa lakini ikaibuka barza mpya na wanachama wapya vijana tofauti kabisa na wale wazee baba zao watu mashuhuri wa mji wa Dar es Salaam.

Nyumba hii baada ya kifo cha Kleist sasa Abdul akiwa ndiyo baba mwenye nyumba ikawa kituo cha mikutano ya Tanganyika Government Servants Association (TAGSA) ambako Ally Sykes alikuwa Secretary kwa miula minne mfululizo.

Katika baadhi ya watu ambao nimeona majina yao katika Nyaraka za Sykes kuwa walikuwa wakihudhuria mikutano ya TAGSA pale na nilikuja kuwajua kwa karibu ukubwani ni Othman Chande na Leonard Bakuname.

Halikadhalika Abdul Sykes alipochukua uongozi wa TAA 1950 baadhi ya mikutano yake ikifanyika hapo nyumbani kwake.

Baada ya kifo cha Kleist rafiki zake kama Aziz Ali na John Rupia hawakuweza tena kuja pale kupiga gumzo.

Wafate nini ilhali mwenyeji wao mwenye nyumba ile hakuwapo?

Hivi ndivyo ilivyojengeka umaarufu wa nyumba ile.

Lakini kubwa ambalo lilinynyanyua sana hadhi ya nyumba hii ni kule Abdul kuwa anatembelewa pale nyumbani kwake na machifu takriban wote wa Tanganyika - Chief Abdallah Said Fundikira, Chief David Kidaha Makwaia, Thomas Marealle, Mwami Theresa Ntare, Chief Adam Sapi Mkwawa kwa kuwataja wachache.

Ilikuwa katika nyumba hii katika moja ya siku za mwanzo za TANU baada ya kikao pale na kula chakula cha mchana Nyerere aliugua ghafla na ikadhaniwa amelishwa sumu ili kumuua.

Mipango yote ya safari ya kwanza ya Nyerere UNO ilikuwa ikipangwa hapa hasa yale mambo yaliyokuwa yanahitajika kufanywa kwa usiri mkubwa.

Halikadhalika pia mipango ya mikutano ya hadhara ya TANU na jinsi ya kuhamasisha wananchi kuhuduhuria kwa wingi mipango yote ilikuwa ikisukwa nyumba hii.

Taarifa za usajili wa TANU Nyerere alizifikisha nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata na Abdul alikuwapo kupokea taarifa hizo.

Nadhani umeelewa.
 
Laki...
Nyumba ya Abdul Sykes ndiyo ikikuwa pia kituo cha harakati za kupambana na dhulma za ukoloni toka wakati baba yake Mzee Kleist yu hai.

Angalia picha:
Ally Sykes na Julius Nyerere, 1958.
Screenshot_20200506-071411.jpg
 
Mzee Said, ama hakika wewe ni mwanahistoria makini sana.

Unajua mengi kuhusu chimbuko la harakati za uhuru wa nchi hii, wewe ni kati ya hazina chache zilizobaki.

My argue; Keep all that in writings for posterity. (A preserved history)
 
Mokaze,
Kwani hujasoma kitabu cha Abdul Sykes?
IMG-20200701-WA0097.jpg
 
kikao kilichoweka azimio la kuivunja TAA na kuunda TANU kilifanyika wapi?
Laki...
Kulikuwa na fikra ya kuunda TANU kwa muda mrefu.

Kikao cha kwanza ambacho kipo katika shajara ya Abdul Sykes kilikuwa Kalieni Camp nje ya Bombay, India tarehe 24 December, 1945 kuamkia Christmas wakati askari wa KAR 6th Battalion walipokuwa wakisubiri kurudishwa Tanganyika baada ya WW II.

Kukawa na vikao kadhaa baina ya Abdul Sykes na Chief David Kidaha Makwaia nyumbani kwa Abdul Sykes.

Kisha kikafanyika kikao Nansio Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu baina ya Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe miezi ya mwanzo 1953.

Baada ya kikao hiki ukafanyika uchaguzi ule wa Arnautoglo April 1953 Julius Nyerere akachaguliwa Territorial President TAA na Abdul Vice-President.

Kati ya 1953 - 1954 pakawa na mazungumzo mengi vikao vikizunguka kati ya nyumba ya Dossa Aziz Mtaa wa Mbaruku, nyumbanu kwa Abdul na ofisi ya TAA New Street.
 
Mzee Said shikamoo.

Kwa ufupi tu unaweza kutaja wakristo na umuhimu wao katika harakati za uhuru? Wanatubagaza sisi waislam kwakua wakristo hujawapambanua
Marashi,
Hapana haja ya hayo.

Mimi nimeandika historia ya uhuru kama nilivyojua ndani ya nyumba yetu na kutoka katika utafiti.

Hii inatosha
 
Majina ya sasa ya hii mitaa ni yapi?
Stanley ndo lindi?
 
Back
Top Bottom