Wasifu wa Lowassa unataja aligombea urais wa JMT 2015 lakini hausemi aligombea kwa chama kipi. Je, kuna wivu wa CCM kwa CHADEMA hata msibani?

Siyo kila kitu kinaandikwa kwenye wasifu.
Wanafamilia huwa wana uhuru wa kuandika mambo/matukio wanayoyaona yanafaa.

Ni kweli, hasa kama kitu chenyewe ni ukweli unaoumiza. Mfano mtu kafa kwa HIV, huwezi kuandika hata kama ni ukweli maana unaumiza na kutia fedheha. Lakini kutoandika ukweli hakuuondoi.
 
Kwani wasipoandika una mtoto wa nje ya ndoa na unaye, mtoto anafutika?
 
Ni kweli, hasa kama kitu chenyewe ni ukweli unaoumiza. Mfano mtu kafa kwa HIV, huwezi kuandika hata kama ni ukweli maana unaumiza na kutia fedheha. Lakini kutoandika ukweli hakuuondoi.

Uko sahihi kabisa. Lakini vp ikiwa kila jambo linaandikwa alilofanya huyu bwana katika maisha yake ya miaka 71 hapa duniani, je sherehe ya maziko ingeisha leo?
 
Wasifu wa Edward Lowasa umetatua madai kuwa aliwahi kugombea urais kupitia Chadema hivyo madai kuwa akina Nape waliwahi kimkashifu na kumdhihaki ni batili.
Haya yatakuwa ni matatizo ya afya ya akili. Ukiona mtu hakubaliani na ukweli uliokuwa bayana, basi hapo ni lazima dishi litakuwa limepinda tu.
 
Wasifu wa Edward Lowasa umetatua madai kuwa aliwahi kugombea urais kupitia Chadema hivyo madai kuwa akina Nape waliwahi kimkashifu na kumdhihaki ni batili.
Nchi imebeba matukio ya aibu kubwa.

Rais anasimama mbele ya Taifa na kuruhusu wasaidizi wake kuongea uongo mkuu dhidi ya marehemu
 
Wasifu wa Edward Lowasa umetatua madai kuwa aliwahi kugombea urais kupitia Chadema hivyo madai kuwa akina Nape waliwahi kimkashifu na kumdhihaki ni batili.
Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mcha Mungu zaidi katika nyinyi.[2] Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari." (Kurani 49:13)
 
Uko sahihi kabisa. Lakini vp ikiwa kila jambo linaandikwa alilofanya huyu bwana katika maisha yake ya miaka 71 hapa duniani, je sherehe ya maziko ingeisha leo?

Hauandiki Kila kitu Hadi alipokuwa anaiba mapera utotoni, unaandika matukio muhimu. Na hilo la kuhama Chama na kugombea urais halikupaswa kutokuwepo, labda kama historia haina maana yoyote.
 
Wasifu wa Edward Lowasa umetatua madai kuwa aliwahi kugombea urais kupitia Chadema hivyo madai kuwa akina Nape waliwahi kimkashifu na kumdhihaki ni batili.
Nina imani hata kule maktaba kwenye Tume yao ya Uchaguzi, napo wametoa hizo kumbukumbu.

Sijui mgombea kupitia CHADEMA kwa mwaka 2015, wameweka jina la nani.
 
Watoto wetu wafundishwe historia ya tanzania. Historia yenyewe ndio hii? Ccm acheni utani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…