KERO Wasimamizi Mradi wa SEQUIP, tusaidieni. Kuna kitu hakiko sawa

KERO Wasimamizi Mradi wa SEQUIP, tusaidieni. Kuna kitu hakiko sawa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wadau habarini,

Mimi ni mwalimu katika moja ya vituo binafsi vya mitihani kwa private candidates (Mufindi DC). Tuna wanafunzi wa kike waliokuja kwa programu maalumu ya serikali (SEQUIP) ambao wanalipiwa gharama zote na serikali kwa makubaliano yetu na serikali, lakini tunaenda kumaliza muhula wa 1 wiki ijayo hakuna malipo yoyote ambayo tumepokea na kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji zinategemea ada za wanafunzi.

Tumefuatilia kwa wahusika wanasema pesa zimeshatoka Wizarani lakini hatujui ni lini zitatufikia.

Vituo vya Serikali vilishapokea pesa shida ni vituo binafsi.

Wasimamizi wa mradi wa SEQUIP fuatilieni kwani tunaumia mno.
 
Back
Top Bottom