GE2025 Wasimamizi wa Uchaguzi Geita Waaswa Kuepuka Vitisho na Upendeleo

GE2025 Wasimamizi wa Uchaguzi Geita Waaswa Kuepuka Vitisho na Upendeleo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wasimamizi wa uchaguzi mkoani Geita wametakiwa kuhakikisha wanaweka mazingira salama na ya haki, bila vitisho, ununuzi wa kura na upendeleo kama sehemu ya wajibu wao wa kusimamia zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya halmashauri na kata, pamoja na maofisa uchaguzi wa halmashauri za wilaya na Manispaa ya Geita, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita, James Ruge amesema uchaguzi ni fursa ya kuwezesha wananchi kumchagua mgombea watakayeshirikiana naye kutatua changamoto za maendeleo.

 
Back
Top Bottom