LGE2024 Wasio na ajira wanabaguliwa uongozi serikali za mitaa?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kuwa na ajira au kazi ni kigezo cha kuwa kiongozi wa serikali za mtaa?

Pia soma
- LGE2024 - Askofu Mwamakula: Mtaa wa Stop Over mgombea wa CHADEMA ameenguliwa kwa kuandika ni mjasiriamali, huku wa CCM akipitishwa kwa kuandika mfanyabiashara

--
"Kibamba hapa Dar es Salaam wapo wagombea wetu (wa uchaguzi wa serikali za mitaa) walioenguliwa sababu eti kwamba hana kazi ya kumpatia kipato halali, ni kwa sababu wameandika ni wajasiriamali sasa unajiuliza sijui walitaka watu wetu wadanganye kuwa ni wakulima ili mwisho wa siku waseme Dar es Salaam hakuna mashamba"
20241108_163808.jpg
 
Kuna kazi na kuna ajira
Hebu weka vizuri swali lako
 
Sasa si ndiyo wanatafuta kazi hapo, au?
Hapo na mimi nimeduwaa, sikuwahi kujua kuna kanuni ya kuwa na kazi kama kigezo cha kugombea huko.
 
Hahaha hii haina tofauti na ile hatukupi mkopo km wazazi wako sio walemavu sio wafu yaan wafe sio wanufaika wa TASAF sio poa
 
Hapo na mimi nimeduwaa, sikuwahi kujua kuna kanuni ya kuwa na kazi kama kigezo cha kugombea huko.
Hiyo kanuni iko kinyume na katiba na hivyo ni batili.

Ipelekwe mahakamani watu wapate hukumu na tafsiri ya katiba.
 
Najua huwa wanasema "uwe na kazi/shughuli halali ya kukuingizia kipato".
 
Tofauti ya kazi na ajira ni ipi?
Mtu anataka uongozi halafu hana kazi maana yake kipato chake kinaingia kwa wizi au? Hawamaanishi awe na ajira ya mikataba wajameni kazi inayokusudiwa hapo ni shughuli kuu mtu anayojishughulisha nayo

Hana kazi maana yake hajishughulishi na shughuli yoyote yeye ni kupanda na kushuka aka mzurulaji! Sasa atapewaje uongozi mtu asiyejishughulisha kutwa kuzurura?
 
Najua huwa wanasema "uwe na kazi/shughuli halali ya kukuingizia kipato".
Huu si ubaguzi kwa wasio na kazi/shughuli ya kuingiza kipato??
 
Mtu anataka uongozi halafu hana kazi maana yake kipato chake kinaingia kwa wizi au? Hawamaanishi awe na ajira ya mikataba wajameni kazi inayokusudiwa hapo ni shughuli kuu mtu anayojishughulisha nayo

Hana kazi maana yake hajishughulishi na shughuli yoyote yeye ni kupanda na kushuka aka mzurulaji! Sasa atapewaje uongozi mtu asiyejishughulisha kutwa kuzurura?
Mama wa nyumbani aliyeolewa na anamtegemea mume wake ana kipato gani? Kwa hiyo haruhusiwi kugombea??

Kwa hiyo Mstaafu anayeishi kwa pensheni bila kufanya kazi asigombe uongozi ??
 
Huwa wanasema awe na kipato halali
Hata hilo la kuwa na kipato halali ni kinyume na katiba.

Katiba haina kifungu cha kipato kwenye haki ya kugombea uongozi.

Hiyo ni aina ya kuwachuja watu kinyume na katiba, kinyume na misingi ya demokrasia.
 
Kuwa na ajira au kazi ni kigezo cha kuwa kiongozi wa serikali za mtaa?

Pia soma
- LGE2024 - Askofu Mwamakula: Mtaa wa Stop Over mgombea wa CHADEMA ameenguliwa kwa kuandika ni mjasiriamali, huku wa CCM akipitishwa kwa kuandika mfanyabiashara

--
"Kibamba hapa Dar es Salaam wapo wagombea wetu (wa uchaguzi wa serikali za mitaa) walioenguliwa sababu eti kwamba hana kazi ya kumpatia kipato halali, ni kwa sababu wameandika ni wajasiriamali sasa unajiuliza sijui walitaka watu wetu wadanganye kuwa ni wakulima ili mwisho wa siku waseme Dar es Salaam hakuna mashamba"
View attachment 3147086
Ujasiriamali sio kazi? Ccm ni mashetani makubwa sana ndio maana mpaka viongozi wakubwa Wana tuhuma za ulawiti! Aibu hayana! Kwanza anakaa ofisi mara Kwa mara hiyo kazi ya Ajira atafanya saa ngapi?
 
Back
Top Bottom