Wasio na kitambulisho cha taifa wataruhusiwa kupiga kura Oktoba 2020?

Wasio na kitambulisho cha taifa wataruhusiwa kupiga kura Oktoba 2020?

Babu sea

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
957
Reaction score
758
Kulingana na mambo yalivyo hiki kitambulisho cha taifa kinawanyima watu hadi haki ya mawasiliano kisa tu inashindikana kusajiliwa line zao bila kitambulisho hicho.

Wasiwasi wangu ni kuwa, itakuaje kama kitambulisho hicho kitatumika kama kigezo namba moja kwa wananchi kuchagua viongozi wanaowapenda?
 
Viparata vya kupigia kura havijaondolewa katika zoezi la kupiga kura. Vitatumika bilashaka na wananchi hawatakosa haki yao ya kupiga kura kuwachagua viongozi wao wanaowataka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Babu sea,

Unaongelea uchaguzi kuna tume huru vya uchaguzi? Kama hamna tume huru ya uchaguzi, kuongelea uchaguzi ni kupoteza muda.
 
Wasiwasi wangu nikua itakuaje kama kitambulisho hicho kitatumika kama kigezo namba moja kwa wananchi kuchagua viongozi wanao wapenda?
Sheria ya uchaguzi inataja mojawapo ya sifa ya mpiga kura,lazima asajiliwe na NEC sio NIDA,tena hata kama umepoteza kitambulisho lakini jina lako lipi kwenye orodha ya wapiga kura kwenye kituo husika,baada ya utambuzi msimazi wa kituo atakupa karatasi za kupiga kura
 
Back
Top Bottom