Wasio na uwezo wa kushika au kutia mimba wanachangamoto nyingi maishani

Wasio na uwezo wa kushika au kutia mimba wanachangamoto nyingi maishani

Joined
Jul 11, 2020
Posts
66
Reaction score
145
Bila shaka tunatambua ustawi wa jamii unaanzia kwenye ngazi ya familia, kwa hiyo ni jukumu la ustawi wa jamii kuwa na sera inayoyaangazia matatizo yote yanayoikumba ngazi ya familia ili kuiweka sawa

Ngazi ya familia ina kitu wanaita TARAKA, ambaye sababu yake kuu kwa tafiti zilizopo ni mtu kushindwa kumtia mtu mimba au mwanamke kushika mimba, baada ya sababu hiyo ndio inafuata usaliti. Kwa hiyo sababu kuu za migogoro ya ndoa ni Kushindwa kuzaa/kuzalisha ikifuatiwa na usaliti ndio unafuata sababu nyingine zikiwemo za kiuchumi

Tatizo la kushindwa kuzaa ni tatizo zaidi kwa mwanamke kwa kuwa manyanyaso huwa ni mengi ikiwemo unyanyapaa. Kama mmeisikia ile kesi ya Mauaji kule Mbezi jamaa alikuwa anamsaliti mkewe waziwazi kwa sababu kuwa mkewe hawezi kumzalia mtoto, pia personaly nimeona wanaume wanavyowanyanyasa wanawake kisa tu kushindwa kupata mtoto

Baadhi ya maneno wanayoambiwa ni kuwa wametoa mimba, kwa hiyo walikuwa malaya kiasi cha kuharibu vizazi vyao, ila si kweli kuwa mwanamke asiyeshika mimba husababishwa na kutoa mimba tu, wengine huwa ni tatizo la kualiwa au mparanganyiko kwenye mfumo wa uzazi

Kwa hiyo watu hawa huonekana walikuwa malaya kiasi cha kutoa mimba nyingi

Pia bado jamii inaona asiyeweza kuzaa kama ana laana. Hapa ndio manyanyaso huwa mengi kwa ngazi zote hata kwenye familia yake mwenyewe sio kwa sehemu aliyoolewa tu. Unakuta mzazi anamuuliza mwanae, 'mwanangu mwaka wa pili huu nataka mjukuu, changamka'

Marafiki na jamaa nao wanamaswali yanayoumiza rafiki zao bila kujua, utasikia he! bado?

Katika watu wenye msongo wa mawazo basi hawa watu naona wanaumia zaidi

Hata wanaume pia hukumbana na matusi, kuambiwa kama hauna mkojo, wewe bado mtoto..nk. ila kijamii mwanamke anaumia zaidi

Ushauri
Kwa kuwa tatizo hili linawaumiza sana wanawake hasa wanapoingia kwenye mapenzi, ni vyema kuwa na mtu ambaye anajiweza kisaikolojia ili asije akawa chanzo cha maumivu

Pili muwe wawazi na msitafute dawa kwa waganga mkaishiwa kutapeliwa, magonjwa mengine hujitibu kwa muda, aidha matatizo mengine huanza na saikolojia, kama reaction kwa kitu ulichokiweza(Scientifically proven) kwamba kuna matatizo huja kweli bila kuwa na chanzo halisi bali hofu ya mtu husika

Tatu, zingatia masuala ya chakula na epuka msongo wa mawazo kwa kuwa na mpenzi au watu watakaokufurahisha ili kama una tatizo lijitibu taratibu, sio ajabu mtu akapata mtoto baada ya miaka kadhaa

Poleni wote!
Tunaelimishana kuhakikisha hatuyumbishwi na stresses
 
Mkuu yani wewe una deal na Mambo ya Mimba tuu huna mda na Maswala Mengine.
Wewe ni Mimba tuu Mimba na wewe

Nazungumzia kitu ambacho najua kinawagusa watu, kujenga ustawi wa jamii

Ustawi wa jamii unaanza na ngazi ya familia, hii ndio angle yangu mimi na mchango wangu wa kimawazo kwa jamii yangu

Unaweza kuwa interested na mambo mengine kama siasa, uchumi nk, wapo wanaoandika kuhusu masuala hayo unaweza wafuatilia kiongozi

Karibu!
 
Naogopa Sana hii kadhia..Namuomba Mungu namimi nipate kafamilia kangu...
 
Kumbuka siyo wote waliokuja Duniani lazima wapate watoto! Na pia kuna watoto wengine hawana watu wakuwalea!!
 
Kumbuka siyo wote waliokuja Duniani lazima wapate watoto! Na pia kuna watoto wengine hawana watu wakuwalea!!
Hiyo ndio hali ya dunia ila ni muhimu kuangalia vitu hivyo bila kuwa na sababu ya kumnyanyasa mtu

Mfano... hatuzaliwi sawa lakini leo hii walemavu wanafurahia mapenzi baada ya kubadili mindset za watu, the same issue can happen kwa ambao hawana uwezo wa kupata mimba
 
Back
Top Bottom