Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Watu wasiofahamika wamechoma moto gari la Mwenyekiti wa vijana CCM wilaya ya Lindi bwana Frenk Mzani Menuka na kusababisha uharibifu mkubwa kwa gari hilo aina ya Toyota Cresta GX 100 lenye namba za usajili T 402 BCH ambalo lilikuwa limeegeshwa kwenye nyumba anayoishi Mwenyekiti huyo wa vijana.
Tukio hilo limetokea usiku wa Februari 06, 2025 baada ya Mwenyekiti huyo kurudi katika mizunguko yake majira ya saa tisa na nusu usiku na ndipo alibaini kutokea kwa tukio hilo baada ya muda mchache tu kurudi nyumbani kwake hapo na baada ya kuegesha gari hilo aliingia ndani haikuchukuwa muda ndipo akabaini kutokea kwa tukio hilo ambalo limegharimu hasara uharibifu mkubwa eneo la injini sehemu ambayo walilenga wahalifu hao.
Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi limeanza upelelezi wa kubaini watuhumiwa waliohusika kutenda kosa hilo.