Wasiojulikana Waiba Kapu la Sadaka Kanisani

Wasiojulikana Waiba Kapu la Sadaka Kanisani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Paroko wa Parokia ya Narumu, kata ya Machame Mashariki mkoani Kilimanjaro, Padri Thomas Chuwa amelaani vikali kitendo kilichofanyika katika Ibada ya Jumapili iliyopita baada ya mtu/watu wasiojulikana kuiba kapu la sadaka Kanisani na kuwataka Waamuni kusali sala maalum kwa siku 3.

May be an image of 1 person and text that says 'DCty NEWS WASIOJULIKANA WAIBA KAPU LA SADAKA KANISANI @danchibotv @dal'
 
Nimeiona hii kwenye habari.
Maisha yanawavuruga watu popote kambi siku hizi linapigwa tukio.
 
Paroko wa Parokia ya Narumu, kata ya Machame Mashariki mkoani Kilimanjaro, Padri Thomas Chuwa amelaani vikali kitendo kilichofanyika katika Ibada ya Jumapili iliyopita baada ya mtu/watu wasiojulikana kuiba kapu la sadaka Kanisani na kuwataka Waamuni kusali sala maalum kwa siku 3.

May be an image of 1 person and text that says 'DCty NEWS WASIOJULIKANA WAIBA KAPU LA SADAKA KANISANI @danchibotv @dal''DCty NEWS WASIOJULIKANA WAIBA KAPU LA SADAKA KANISANI @danchibotv @dal'
Bila shaka kanisa kupitia viongoz wake wanapaswa kuyaish yale wanayotuhubiria.

"Samehe saba mara Sabin"
 
Kilichoibwa ni sadaka zenye kila aina ya maombi.. Hao wezi wataila pesa ila laana italala nao mbele
Hatutakiwi kuwaombea laana bali kuwaombea msamaha ili hasira ya Mungu isitupige. Vipi km Mungu atadhihirisha hasira yake kwa kushusha njaa,tetemeko,au ukame si wengi tutaathirika hata km hatuhusiki? Mtoto mtundu akipiga mzinga wa nyuki sio kwamba nyuki watamuuma huyo mtoto pekee bali wengi wasiohusika wanaweza kuathirika ndivyo ikivyo hatari ya binadamu mmoja akipotoka.Muhimu ni kuomba Mungu awasamehe km Biblia inavyosema tuwe watu wa kuombeana siku zote.
 
Nakumbuka miaka ya 1998 kama sikosei kuna habari iliwahi kuripotiwa kwenye radio moja maarufu enzi hizo eti wezi waliingia kanisani wakaiba sadaka halafu hawakuishia hapo wakala mikate na divai wakasepa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]nadhani ilikuwa huko huko mikoa ya kaskazini
 
Back
Top Bottom