Wasiojulikana walivyopora kiwanda cha Mzee wa miaka 67 kibabe. Aomba Rais Samia amsaidie kupata Mali yake

Wasiojulikana walivyopora kiwanda cha Mzee wa miaka 67 kibabe. Aomba Rais Samia amsaidie kupata Mali yake

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
Mwekezaji mzawa wa kiwanda cha maziwa(New Northen) creameries Ltd na mjasiriamali wa mazao mbalimbali,
John Kyenkungu arejea kumiliki mali yake aliyokuwa amenyang'anywa na watu walio jiita maofisa wa Serikali wasiofahamika tangu mwaka 2019 na

Mali hiyo ni Kiwanda alichonunua sh.milioni 440 serikalini mnamo mwaka 1999 ambacho kipo katika kiwanja namba 4-13 maeneo ya Unga Ltd jijini Arusha kitalu D kwa lengo la kuwekeza ili kujiinua kiuchumi na kusaidia watanzania kupata ajira.

Akizungumza kwa machungu mbele ya vyombo vya habari mbalimbali,Mwekezaji huyo,Kyenkungu alisema kiwanda kilikuwa kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita elfu 70 kwa siku za maziwa ambapo kupitia uwekezaji wake aliweza kuajiri watu zaidi ya 100 wakiwemo vijana.

Kyenkungu alisema kiwanda hicho kilichokuwa tegemezi katika maisha yake ambapo aliweza fikia hatua ya kukodisha mashamba ya West Kilimanjaro lengo likiwa ni kupanua biashara yake ya maziwa kwa kuweza kuzalisha kwa wingi maziwa katika kiwanda chake pamoja na kusaidia wakulima na wafugaji kupata faida kupitia biashara wanazofanya.

"Wakati naendelea kujihimarisha zaidi kwenye kiwanda changu ghafla nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa anatoka Ofisi ya Msajili wa hazina ambaye alinitaka nifikie Arusha ikiwa mimi nilikuwa Dar es Salaam lakini baadaye nilifika katika eneo langu la kiwanda,"alisema Mwekezaji huyo.

Alisema baada ya yeye kuwasili mkoani Arusha katika eneo lake la biashara walijitokeza kundi la watu wanaokadiriwa ishirini wakiwemonpolisi wenye silaa za moto ambao hawafahamu na hawakujitambulisha mahali walipotoka wakampatia barua iliyoonyesha notisi kwa stakeholder meeting na kumtaka kuondoka araka eneo hilo la kiwanda.

"Barua hii ilikuwa ni confidential iliyoandikwa mei 27,2019 ambapo ilionyesha imetoka Ofisi ya Msajili wa hazina ambapo ilisainia na Peter Gwalilo lakini aliyeileta sikumtambua kutokana na kutojitambulisha,"alisema.

Kyenkungu alisema baada ya hapo aliona kikundi cha watu kikiongozana na polisi waliokuwa na bunduki wakimwambia achague mawili kati ya kupewa kesi ya uhujumu uchumi au aachie kiwanda hicho ambapo walidai kuwa kinarudishwa kwa serikali yeye alijibu ni vyema wakamfunga maana ayupobtayari kuachia mali yake lakini hawakufanya hivyo.

"Baada ya hapo nilirudi Dar es Salam kutokana na ndipo nilipokuwa nafanya shughuli zangu ndogo ndogo lakini waliwaondoa wapangaji wangu katika magodauni yangu pamoja na walinzi wakawaweka wa kwao,"alisema.

Hata hivyo alisema baada ya kufika Dar es Salaam alifika na kutafuta njia nyingine ya kuishi kutokana na hali ya msongo wa mawazo aliyokuwa nayo katika kipindi hicho cha kunyang'anywa mali yake aliyokuwa anahitegemea na alishindwa kuwekeza chochote katika kiwanda hicho tangu alipoporwa mali hiyo na mtu asiyejulikana.

"Katika maisha yangu sikutegemea kama kuna kitu kama hicho kinaweza kutokea katika maisha yangu lakini baada ya mwaka mmoja nikapigiwa simu na watu ambao hawakujitambulisha kunataka nifike benki kuu ambapo nilipofika niliwakuta watu kama 20 kwenye chumba na walisema hawawezi kujitambulisha kwangu,"alisema Muwekezaji huyo.

Aliongeza kuwa katika kikao hicho kilichofanyika BOT alienda na Mwanasheria wangu na Consultant laki waliwakataa na kudai wanamuhitaji yeye tu na baada ya kubaki walimsisitiza kuwa akitaka uzee wake uende salama ni vyema akarudisha hati ya kiwanda kile serikalini la sivyo watampeleka uhujumu uchumi.

"Nilichosema kwani niko tayari na wala sikutaka kupoteza muda mwingi ikiwa kipindi hicho nipo na msongo wa mawazo ambapo niliona ni bora niende uhujumu uchumi tu nikiona hata nilipokuwepo nilikuwa sina namna ya kuishi,"alisema.

Naye wakili Emmanuel Antony alisema mteja wake hadi sasa ni mmiliki halali wa kiwanda hicho hivyo hana budi kurejea kwenye mali yake kutokana alinunua kihalali kwani kitendo cha kuchukuliwa na mtu asiyejulikana ni mazingira ambayo hayana baraka za serikali.

"Kitendo hicho hakina baraka kwa serikali kutokana na kuwa na taarifa zote za ununuzi wa kiwanda hicho lakini pamoja na hilo watu waliokuwa wanakuja kiwandani hawakujitambulisha kwa mmiliki wa kiwanda,"alisema Wakili huyo.

Pia alisema barua yenyewe ya notisi aliyoletewa imeandikwa ni ya siri ambayo ilikuwa wito wa kikao cha wadau na mawasiliano yenyewe yaliyokuwa yanafanyika baina ya mteja wake na hao watu wasiojulikana yalikuwa ya siri hivyo kupitia vigezo hivyo ni dhahiri kuwa hiyo siyo serikali bali ni mtu asiyejulikana ambaye ni mpokonyaji wa mali hiyo na sasa anayohaki wa kurudi katika mali yake.

20220404_120045.jpg
 
Aliponyang'anywa tu Kiwanda akaamua kurejea DSM kuendelea na mambo yake mengine siyo?
 
Na bado wanakwambia eti jiwe alikua Ni mtetezi wa wanyonge na Ni shujaa wa Africa [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Jiwe alikuwa anatembeza ubabe kama ule wa wild wild east uliomkumba daktari Shika
 
Mwekezaji mzawa wa kiwanda cha maziwa(New Northen) na mjasiriamali wa mazao mbalimbali, John Kyenkungu arejea kumiliki mali yake aliyokuwa amenyang'anywa na watu walio jiita maofisa wa Serikali wasiofahamika tangu mwaka 2019

Mali hiyo ni Kiwanda alichonunua sh.milioni 440 serikalini mnamo mwaka 1999 ambacho kipo katika kiwanja namba 4-13 maeneo ya Unga Ltd jijini Arusha kitalu D kwa lengo la kuwekeza ili kujiinua kiuchumi na kusaidia watanzania kupata ajira.

Akizungumza kwa machungu mbele ya vyombo vya habari mbalimbali,Mwekezaji huyo,Kyenkungu alisema kiwanda kilikuwa kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita 60 za maziwa ambapo kupitia uwekezaji wake aliweza kuajiri watu zaidi ya 100 wakiwemo vijana.

Kyenkungu alisema kiwanda hicho kilichokuwa tegemezi katika maisha yake ambapo aliweza fikia hatua ya kukodisha mashamba ya West Kilimanjaro lengo likiwa ni kupanua biashara yake ya maziwa kwa kuweza kuzalisha kwa wingi maziwa katika kiwanda chake pamoja na kusaidia wakulima na wafugaji kupata faida kupitia biashara wanazofanya.

"Wakati naendelea kujihimarisha zaidi kwenye kiwanda changu ghafla nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa anatoka Ofisi ya Msajili wa hazina ambaye alinitaka nifikie Arusha ikiwa mimi nilikuwa Dar es Salaam lakini baadaye nilifika katika eneo langu la kiwanda,"alisema Mwekezaji huyo.

Alisema baada ya yeye kuwasili mkoani Arusha katika eneo lake la biashara walijitokeza kundi la watu wanaokadiriwa ishirini wakiwemonpolisi wenye silaa za moto ambao hawafahamu na hawakujitambulisha mahali walipotoka wakampatia barua iliyoonyesha notisi kwa stakeholder meeting na kumtaka kuondoka araka eneo hilo la kiwanda.

"Barua hii ilikuwa ni confidential iliyoandikwa mei 27,2019 ambapo ilionyesha imetoka Ofisi ya Msajili wa hazina ambapo ilisainia na Peter Gwalilo lakini aliyeileta sikumtambua kutokana na kutojitambulisha,"alisema.

Kyenkungu alisema baada ya hapo aliona kikundi cha watu kikiongozana na polisi waliokuwa na bunduki wakimwambia achague mawili kati ya kupewa kesi ya uhujumu uchumi au aachie kiwanda hicho ambapo walidai kuwa kinarudishwa kwa serikali yeye alijibu ni vyema wakamfunga maana ayupobtayari kuachia mali yake lakini hawakufanya hivyo.

"Baada ya hapo nilirudi Dar es Salam kutokana na ndipo nilipokuwa nafanya shughuli zangu ndogo ndogo lakini waliwaondoa wapangaji wangu katika magodauni yangu pamoja na walinzi wakawaweka wa kwao,"alisema.

Hata hivyo alisema baada ya kufika Dar es Salaam alifika na kutafuta njia nyingine ya kuishi kutokana na hali ya msongo wa mawazo aliyokuwa nayo katika kipindi hicho cha kunyang'anywa mali yake aliyokuwa anahitegemea na alishindwa kuwekeza chochote katika kiwanda hicho tangu alipoporwa mali hiyo na mtu asiyejulikana.

"Katika maisha yangu sikutegemea kama kuna kitu kama hicho kinaweza kutokea katika maisha yangu lakini baada ya mwaka mmoja nikapigiwa simu na watu ambao hawakujitambulisha kunataka nifike benki kuu ambapo nilipofika niliwakuta watu kama 20 kwenye chumba na walisema hawawezi kujitambulisha kwangu,"alisema Muwekezaji huyo.

Aliongeza kuwa katika kikao hicho kilichofanyika BOT alienda na Mwanasheria wangu na Consultant laki waliwakataa na kudai wanamuhitaji yeye tu na baada ya kubaki walimsisitiza kuwa akitaka uzee wake uende salama ni vyema akarudisha hati ya kiwanda kile serikalini la sivyo watampeleka uhujumu uchumi.

"Nilichosema kwani niko tayari na wala sikutaka kupoteza muda mwingi ikiwa kipindi hicho nipo na msongo wa mawazo ambapo niliona ni bora niende uhujumu uchumi tu nikiona hata nilipokuwepo nilikuwa sina namna ya kuishi,"alisema.

Naye wakili Emmanuel Antony alisema mteja wake hadi sasa ni mmiliki halali wa kiwanda hicho hivyo hana budi kurejea kwenye mali yake kutokana alinunua kihalali kwani kitendo cha kuchukuliwa na mtu asiyejulikana ni mazingira ambayo hayana baraka za serikali.

"Kitendo hicho hakina baraka kwa serikali kutokana na kuwa na taarifa zote za ununuzi wa kiwanda hicho lakini pamoja na hilo watu waliokuwa wanakuja kiwandani hawakujitambulisha kwa mmiliki wa kiwanda,"alisema Wakili huyo.

Pia alisema barua yenyewe ya notisi aliyoletewa imeandikwa ni ya siri ambayo ilikuwa wito wa kikao cha wadau na mawasiliano yenyewe yaliyokuwa yanafanyika baina ya mteja wake na hao watu wasiojulikana yalikuwa ya siri hivyo kupitia vigezo hivyo ni dhahiri kuwa hiyo siyo serikali bali ni mtu asiyejulikana ambaye ni mpokonyaji wa mali hiyo na sasa anayohaki wa kurudi katika mali yake.

View attachment 2176717
Tulipigwa
 
MFANYABIASHARA, John Kyenkungu ameleezea namna alivyonyang'anywa kiwanda chake cha New Nothern Creameries LTD na watu walioingia kiwandani kwake wakiwa na magari yenye ving’ora na askari wenye mitutu ya bunduki huku wakigoma kujitambulisha majina wala taasisi ya serikali waliyotokea.

Aidha, ameeleza kuwa mwaka mmoja baadaye aliitwa kwenye taasisi moja ya serikali (jina tunalihifadhi kwani wahusika hawajapatikana kutokea ufafanuzi) akakuta watu zaidi ya 20 ambao walikataa kujitambulisha huku wakamtaka achague kati ya mambo mawili ama awapatie hati ya kiwanda hicho au afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi.

Pia ameeleza kuwa siku moja kabla ya watu hao wenye mitutu kuvamia kiwanda alipokea wito wa barua kutoka kwa msajili wa taasisi nyingine ya serikali (wahusika hawajapatikana kutolea ufafanuzi) akimtaka kushiriki kikao cha wadau wa kiwanda cha Tanzania Dairies Limited Pants ambacho kilishakufa ndiyo yeye akauziwa na serikali huku barua hiyo ikigongwa muhuri wa siri.

Kyenkungu aliyasema hayo April 4, 2022 nyumbani kwake jijini Arusha wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya sakata hilo ambapo alisema aliamua kuongea sasa kwani Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa serikali yake haitaki dhuluma na anaamini waliomnyang’anya kiwanda hawana baraka za serikali.

“Baada ya kutafakari tokea hawa watu wasiofahamika kuchukua kiwanda changu mwaka 2019 nimeona nilikuwa natakiwa kuripoti wizara ya mambo ya ndani kila baada ya mwezi mmoja lakini kuanzia desemba mwaka jana wakasema nisiripoti kwani namba za simu zangu wanazo,” alisema Kyenkungu na kuongeza.

… Wakinihitaji watanipigia hivyo ndiyo imenipa nguvu sasa kurejea kwenye kiwanda changu na hasa msisitizo anaoweka Rais Samia kwenye uwekezaji na kulinda uhuru wa mtu kutoa maoni yake na kusikilizwa nilitafakari nikaona nirudi kwenye kiwanda change,”.

Kyenkungu ambaye aliwahi kuajiriwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ya zamani, Kitengo cha Forodha na aliamua kuacha kazi mwenyewe mwaka 1985 akaamua kujiajiri.

"Mimi nilikuwa mtu wa kwanza kufungua mgahawa wa Jamaa fast food jijini Dar es salaam niliendesha mgahawa huo na ndiyo ulioniwezesha kupata fedha za kuweza kununua kiwanda,” alisema Kyenkungu na kuongeza.

...Nilinunua kiwanda baada ya serikali kutangaza tenda kuwa wanauza kiwanda cha TDL Arusha Plant nilinunua zabuni nikasoma masharti kitu kilichonivutia ni kuwa serikali ilikuwa inauza kiwanda kwa asilimia 100 na baada kuuza haitaweka fedha nyingine kwa maana hatirudi nyuma kufanya kitu chochote,”.

Mtaji wa kununua kiwanda nilikopa benki, mtaji wa pili wa kununua kiwanda nilikopeshwa na taasisi ya Shirika la Msaada wa Marekani (US AID) kitengo cha Social Action Trust Fund, (SATF) ambapo kiwanda alikinunua shilingi milioni 440 mwaka 1999 kisha akaongiza shilingi miliono 600 kwa ajili ya kufufua kiwanda.

Alisema baada ya kukinunua kiwanda hicho chenye hati namba 55042/2, kiwanja namba 4-13 kitalu D kilichopo maeneo ya Esso Unga Limitedi jijini Arusha ilimbidi kukikarabati kwa kiwango kikubwa kukifufua kwani kabla ya kuuziwa kilikuwa kimefungwa kwa miaka mitano hivyo kulikuwa na madeni ya bili za maji, umeme, simu na sanduku la posta.

“Tulifanya kazi tukanunua maziwa ya wafugaji lakini bahati mbaya shida ilikuwa uwezo wa kiwanda kuzalisha ukawa ni mkubwa kuliko maziwa tuliyokuwa tukipata kwa wafugaji kama malighafi hivyo ikawa ni changamoto kwani kiwanda kilikuwa na uwezo wa kuchakata maziwa lita elfu 70 lakini sisi tulikuwa tunachakata lita elfu 10 kwa siku,” alisema Kyenkungu na kuongeza

…Zile fedha tulizokopa kwa ajili ya kufufua kiwanda shilingi 600 milioni ikatengeza ‘interest’ wakatupeleka mahakamani wakatudai fedha zao lakini bahati nzuri baada ya kupata ‘decree’ tukakaa nao wakasimamisha riba hapo ilikuwa imeshafika zaidi milioni 400 kwenye mkopo wa shilingi milioni 600 hivyo jumla nilikuwa nadaiwa kama bilioni moja.

...walitupa miaka 10 tulipe deni hilo hivyo tukaingia ubia na kampuni ya Kenya ya Brookside ambao walikuwa wanapeleka maziwa Kenya ila siasa iliingia ikawa inasemwa vibaya mwaka 2014 wakaamua kuondoka lakini deni lilikuwa limeshalipwa kwa asilimia 80

…Asilimia 20 ilibidi nitafute marafiki zangu tuuze mali zetu tulipe deni la SATF 2018 tukamaliza mkopo wakaturejeshea hati ya kiwanda ambayo mpaka sasa tunayo,”.

Kyenkungu alieleza kuwa ili wasirejee kwenye tatizo la nyuma la kuzalisha chini ya uwezo waliamua kuiomba serikali ili kutumia mashamba ya serikali yaliyo maeneo ya West Kilimanjaro kwa ajili ya kuzalisha maziwa.

“Tukaambiwa tupeleke andiko letu wizara ya Kilimo wakatuambia tuandike mpango wa biashara (Busness plan) tuliwa tayari kukodisha au kununua hayo mashamba. UNDP walikuwa tayari kutupa mkopo wa dola milioni 5,” alisema Kyenkungu na kuongeza.

…Wakati tunaendelea na mchakato ili tupate fedha hizo Mei 29, 2019 nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ni afisa wa serikali kutoka msajili wa hazina wakaniambia tukutane kiwandani Mei 30 kuna kikao.

…Nilikuwa Dar hivyo nikasafiri mpaka Arusha saa nne nikawapigia simu kuwambia niko kiwandani wakaniambia nisubiri ilipofika saa nane nikaona msafara wa magari ukiongozwa na king'ora na zaidi ya polisi 20 wenye silaha wakiingia kiwandani.

… Hawakujitambulisha ila wakanipatia barua ya kikao cha wadau TDL ambayo ni barua iliyogongwa muhuri wa SIRI iliyotolewa Mei 27,2019 na ofisi moja ya msajili wa hazina na ilisainiwa na Peter Gwarilo lakini sijui kama aliyenipa kama ndiyo Peter.

…Walipofika walifunguliwa mlango na walinzi wangu nikaona wameingia na askari na mabunduki wakaniambia serikali inachukua kiwanda nikapata mshangao nikapata ‘emotion’ nikawaambia kama mnataka mniweke ndani ndiyo niwakabidhi lakini hawakufanya hivyo mimi nikarudi zangu Dar es Salaam.

…Hawa watu hawakunionyesha vitambulisho vyao isipokuja walikuja na gari ya kimulimuli na askari walishuka kwenye magari wakaanza kukoki bunduki zao kama wamekuja kumkamata jambazi wakasema serikali imeamua kuchukua kiwanda nikawaambia wanipe barua hiyo wakanivuta nje ya ofisi wakaweka polisi.

… Baada ya kufika Dar nilitafakari endapo nitaishi au nitakufa kwani kuanzia mwaka 1999 fedha zangu na nguvu zangu zote niliwekeza kwenye hicho kiwanda,”.

Kyenkungu alisema kuwa baada ya mwaka mmoja alipigiwa simu na watu ambao hawakujitambulisha wakamtaka aende (tassisi moja ya serikali) ambapo alipofika alikuta watu kama 20 kwenye chumba wakasema hawawezi kujitambulisha kwake.

“Nilikuwa nimeenda na wakili na mshauri wangu wakasema hawahitaji mwanasheria wala mshauri wanajitaka mimi tu.Walinipa masharti kuwa nikitaka nikae vizuri na uzee wangu uende salama nirudishe hati ya kiwanda na watatengeneza nyaraka kuonyesha kuwa narudisha hicho kiwanda serikalini la sivyo watakupeleka uhujumu uchumi,” alisema Kyenkungu na kuongeza.

....Nikasema ‘I’m ready’ sikutaka kupoteza muda kwa kuwa nikuwa nimeshachoka, nikawaambia kuliko nirudishe hicho kiwanda ambacho nimenunua kwa asilimia 100 ni bora niende uhujumu uchumi manake hata uraiani nilipo sina namna ya kuishi.

…Tukakaa pale wakaniambia una mtu yeyote aliyeko serikalini akuwekee dhamana nikasema sina mtu yeyote, dhamana hiyo ni ya nini? Mimi niko tayari kwenda ndani wakajadiliana wakasema wewe utajidhamini utakuwa unaripoti kila wiki wizara ya mambo ya ndani,”

Kyenkungu alisema kuwa wakati anaendelea kuripoti wakamuita mdogo wake ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa Jamaa fast food naye wakamuhoji wakawa wanamwambia mwambie kaka yako arudishe hicho kiwanda sisi tuachane naye akasema hawezi.

“Niliendelea kuripoti kila wiki baadaye wakaniambia niwe naripoti kila mwezi. Tarehe 24 Agost 2020 wale watu waliokuwa pale benki kuu wakasema wanataka kwenda kiwandani Arusha nikawaambia kufanya nini wakanisisitiza nikawaambia sina nauli wakanilipia nauli shilingi laki 3,” alisema Kyenkungu na kuongeza.

…Tunaenda Arusha pale polisi Central wakachukua polisi wakaenda wakavunja ofisini kwangu pale kiwandani wakachukua nyaraka nikawaambia wanipatie ‘certificate of seizure’ wakaniandikia.

…Walichukua mafaili ya uendeshaji wa kiwanda, maji, umeme watumishi waliokuwa pale stamp duty baada ya hapo mimi nikarudi Dar nikaendelea kuripoti ilipofika Desemba 2021 wakaniambia usiripoti tena tukikuhitaji tutakupigia tuna namba zako. Baada ya kuniachia desemba hawajanitafuta nimeona nirudi kiwandani kwangu,”.

ATAKA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUZALISHA MBEGU KIWANDANI HAPO

Kyenkungu alisema kuwa kwa sasa yeye ni mjasiriamali amenunua mashamba ya kulima soya maeneo ya Madaba Songea ambapo anataka kushirikiane na serikali tutengeneze mbegu kwa sababu hapa nchini haku mbegu hiyo.

“Mwezi wa tano nataka kuvuna hivyo nahitaji kiwanda changu nitumie maghala yangu. Kuna ambayo nitatumia kutengenezea mbegu na kuuza kwa wakulima.

“Nichukue nafasi hii kumpongeza Rais Samia katika mwaka wake mmoja amefanya mambo makubwa sisi wajasiriamali.Nimevutiwa na hotuba zake anazosema hataki dhuluma na anataka wafanyabiashara tufanye kazi na mimi nikaona nirejee kwenye biashara yangu nichape kazi,” alisema Kyenkungu na kuongeza

..Ifike mahali sisi wajasiriamali tumuombe rais akatutafutie masoko nje ya nchi na si kwenda kutafuta fedha serikali iko pale kutuwekea mazingira mazuri na usalama uliopo sasa hivi,”.
[https://blogger]ili mmanuel Antony (kulia) akiongea na waandishi wa habari akiwa na mteja wake, John Kyenkungu

Wakili wa Kyenkungu, Emmanuel Antony kutoka kampuni ya uwakili ya Kilimanjaro Elite Attorneys and consultancy alisema kuwa mteja wao alinunua kiwanda hicho kihalali baada ya kutangazwa zabuni akasoma akaelewa akaona masharti yote anaweza kutekeleza basi akachukua hatua kuwa mmoja wa wazabuni kati ya 20 waliojitokeza ambapo kwenye mchakato yeye alikuwa wa pili kwani aliyeshinda zabuni alikuwa ni kampuni ya Kenya ya KCC

“Baada ya KCC kushindwa kutimiza masharti mteja wetu walifuatwa na serikali akaambiwa kuwa yeye alikuwa wa pili hivyo wakaona ni sawa afike kumilikishwa kiwanda hivyo alifuata taratibu za awali za kulipa ili amaliki kiwanda,” alisema wakili Emmanuel na kuongeza.

Alivyotueleza namna alivyang’anywa kiwanda chake tuliona jambo lile halina baraka za serikali kwa sababu serikali ina taarifa zote za namna ambavyo iliuza kile kiwanda ikiwemo sababu zilizopelekea kukiuza,”.

Wakili huyo alisema kuwa wale waliofika kiwandani kunyang’anya kiwanda hawakujitambulisha kama jambo alilodai kuwa kama hatua hiyo ingekuwa na baraka za serikali basi watu wale wangeonyesha vitambulisho vyao au wangesema majina, vyeo, na wakamwambia dhumuni lao

“Tatu mteja wetu ameeleza hapa aliitwa ( taasisi ya serikali) wale watu walimwambia sisi hatujitambulishi kwako lakini wewe unatujua sisi ni akina nani. Siku ya Mei 30,2019 walipokuwa wanaenda kwenye kiwanda cha mteja wetu alipokea barua iliyokuwa inampa taarifa ya mkutano wa wadau kwenye kiwanda cha Tanzania Diary LTD ambacho kilishakufaga hakipo huku barua hiyo ikigongwa muhuri wa SIRI,” alisema Emmanuel na kuongeza.

…Inawezekana vipi mkutano wa wadau ambao hata idadi haijaelezwa ukawa mkutano wa siri? Hata mawasiliano ambayo mteja wetu aliyafanya hayakuwa ya wazi yaani hayakuwa rasmi kwani tunaelewa vema mawasiliano ya serikali ni kwa njia ya maandishi na barua lakini kwa mteja wetu walikuwa wanawasiliana naye kwa simu yake ya kiganjani.

...Wangefuata taratibu stahili ingetuwezesha kujua kiwanda hiki kimechukuliwa na serikali hivyo tungefuata taratibu kuishitaki serikali tungekuwa tumezifuata na kungeshawasilisha notisi ya nia ya kuishitaki serikali lakini kwa sasa hatujui tumshitaki nani kwani hakuna barua yoyote inayoonyesha nani kachukua kiwanda zaidi ya barua ya wito wa kikao cha wadau.

…Kwa tunavyoangalia vielelezo alivyo navyo mteja wetu tunaona serikali haihusiki ila ni uhuni tu ulifanyika hivyo tulichomshauri mteja wetu anayo haki ya kurudi kiwandani kwake na kuendelea na shughuli zake ili yule ambaye alianzisha huu mchakato wa kumnyang’anya kiwanda kinyemela ajitokeze.

…Pindi atakapojitokeza huyo ndiye tutakayemchukulia hatua kwa kumnyang’anya mteja wetu kiwanda kinyemela na hasara aliyomsababishia kwa kipindi chote kuanzia alipochukua kiwanda mpaka sasa ambapo mteja wetu ameshindwa kuzalisha,”.

Wakili Emmanuel alisema kuwa wao wana uthibitisho wa mteja wao kumiliki hiki kiwanda ikiwemo nyaraka za tenda na hati za umiliki wa kiwanda, risiti kuonyesha alilipia matumizi ambayo serikali aliyafanya wakati huo kabla hajanunua kiwanda, mteja wao alifanya uwekezaji na alichukua mikopo kwenye taasisi za fedha.

“Huyu ndiye mmiliki halali wa kile kiwanda na ana nguvu kubwa kuliko yule aliyeenda kuchukua kiwanda na kibarua kinachosema ‘stakeholder meeting’,” alisisitiza Wakili Emanuel na kuongeza.

…Tumemshauri mteja wetu arudi kiwandani ili ajue nani anayetaka kumnyang'anya kiwanda chake na atakapojitokeza ajue kabisa ‘ataface consequances’ . Mteja wetu kapata madhara makubwa sana ukipiga mahesabu hapa kimtaji, kihisia, kisaikolojia, maumivu kuna vingine huwezi kumlipa sasa tutavibadili viwe kwa thamani ya fedha ili mteja wetu apate haki yake,”.

Alisema kuwa kabla ya kwenda kiwandani tayari walitoa taarifa kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha kupitia kwa Katibu Tawala wa mkoa,(RAS), Mkuu wa Makosa ya Jinai Mkoa, (RCO), Mkuu wa Polisi wilayani Arusha,(OCD) na ofisi ya mwenyekiti wa mtaa wa Esso.

“Wote wanataarifa mteja wetu anakwenda kwenye kiwanda chake, anakwenda kwenye mali yake ili kusudi akaangalie mali yake inaendeleaje sasa kama kutakuwa na mtu wa kumzuia hapo ndiyo tutaanzia hapo kuchukua hatua za kisheria,” alisema Wakili Emanuel.

“Tunataka tujue aliyemuondoa pale kama ni muhuni tu tutamshitaki, kama ni mtumishi wa umma Rais wetu mama Samia alishasema hapendi dhuluma serikali yake itamshughulikia,”.

AKABIDHIWA KIWANDA BAADA YA DAKIKA CHACHE UAMUZI HUO WABATILISHWA

Msimamizi wa SUMA-JKT, Ally Selemen ambao ndyo wanalinda kiwanda hicho alimruhusu Kyenkungu na mawakili wake kuingia ndani ya kiwanda hicho huku akisema kuwa wakuu wake wa kazi wamemwambia akabidhi kiwanda.

“ Nimepewa idhini ya kuja kukabidhi hiki kiwanda na supervisor mimi sina mengine ni hayo tu,” alisema Ally wakati akiongea na mfanyabishara huyo na mawakili wake.

Hata hivyo alipoambiwa aeleze alielekezwa na nai kukabidhi kiwanda alisema kuwa yeye aliambiwa akabidhi kiwanda tu.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Esso, Amani Abdallah alisema kuwa anashukuru kama kiwanda hicho cha maziwa kilichopo kwenye mtaa wake kama kitaanza uzalishaji kwa sababu kuna vijana wanahitaji ajira na ndiyo watapatia hapo na kuweza kuhudumia familia zao.

“Tutashirikiana na hawa wanaoingia hata wale waliokuwepo tulishirikiana nao vizuri hatukupata shida hivyo nawakaribisha karibuni sana Esso,” alisema Amani.

Mtendaji wa Kata ya Unga Limitedi naye alifika kwenye eneo hilo ingawa alikataa kuongea wala kujitambulisha kwa majina yake kwa waandishi kwa kile alichodai kuwa yeye si msemaji.

“ waandishi wa habari eneo hili ndiyo Nothern creameries LTD ambalo eneo hili analimiliki mteja wangu tokea mwaka 1999 na aliondolewa hapa kinyemela lakini bahati nzuri tumefika hapa na kuwakuta wanaosimamia ulinzi wamewasiliana na viongozi wao kwa njia ya amani na makubaliano wamewaeleza kuwa kuwa watukabidhi tu eneo letu,” Wakili Emanuel aliwaeleza waandishi wa habari na kuongeza

…Kama tulivyosema awali hakukuwa na mkono wowote wa serikali ni watu waliamua kufanya vitendo vyao kinyemela na kama nilivyosema mteja wangu ni mtu wa amani hivyo ataendelea kufanya kazi na wakati anafanya kazi kama ikibainika kuwa kuna hatua yoyote ya kisheria tunayoweza kuchukua tutaangalia ni hatua gani tutachukua lakini kwa hatua ya sasa mteja wangu atachukua kiwanda chake na ataangalia ni namna gani sasa ataweza kufanya kazi,”.

Mmilikiwa kiwanda hicho Kyenkungu alizunguka kwenye uwanja wa kiwanda hicho ambapo aliagiza kampuni yake ya ulinzi kuingia kuanza kushika lindo ambapo wakati zoezi hilo likiendelea alielezea kufarijika kurejea kiwandani kwake.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa hii nguvu mpaka sasa, naishukuru serikali ya mama Samia bila yeye tusingepata ushirikiano huu, tutatoa shukurani zetu baada ya kuona utendaji wa kazi ni vipi na yeye siku moja aje aone hiki kiwanda kinafanya nini,” alishukuru Kyenkungu.

Mfanyabiashara huyo aliagiza lindo la kiwanda hicho likabidhiwe kampuni ya ulinzi ya A One Securite ambapo walinzi wanne wa kampuni hiyo wakiwa na sare zao walianza kubandika mabango yao.

Mlinzi wa kampuni, Sweetbert Lwilamila alisema kuwa wao ndiyo waliokuwa wakilinda awali kabla kiwanda hicho kuchukuliwa na lindo hilo kukabidhiwa kiwanda Jeshi la Kujenga Taifa, ( SUMA- JKT)

Hata hivyo wakati zoezi hilo likiendelea, Msimamizi wa SUMA-JKT, Ally, alisema kuwa amepokea maelekezo toka kwa kiongozi wake kuwa zoezi hilo lisitishwe hivyo kuwalazimu mawakili kuelekea kwenye ofisi za SUMA JKT.

View attachment 2177621View attachment 2177622
20220404_120045.jpg
 
Back
Top Bottom