Wasiokula nyama wako hatarini kuvunjika mifupa kadiri umri unavyoendelea

Wasiokula nyama wako hatarini kuvunjika mifupa kadiri umri unavyoendelea

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Tafiti iliyofanyika Uingereza ilijumlisha watu 26,000 wenye umri kati ya miaka 26-60. Imeonyesha kuwa ulaji wa nyama unatoa virutubisho vinavyosaidia mwili kuimarisha mifupa.

Idadi kubwa ya wanaofanyiwa upasuaji kwa matatizo ya mifupa hasa ya nyonga ni wanawake na wengi ni wale walioacha au kupunguza na wasiokula nyama nyekundu.

Kama kawaida hakuna kitu kinachokosa upinzani. Walaji wa mboga mboga wanaikosoa hii tafiti kwa kusema Nyani, Sokwe na tumbili hawali nyama na wala hawavunjiki

Watafiti wamejibu hoja hii kwa kusema life span ya binadamu ni ndefu kuliko ya sokwe na tumbili.

Kwa kufupi ulaji wa nyama kupitiliza si mzuri kwa afya na pia ulaji wa chakula cha sungura unaunyima mwili virutubisho muhimu.
 
Wakati huo huo kuna tafiti nyingine zinatuambia ulaji wa nyama ni sumu kwa miili yetu! Sasa sijui tufanyeje.
 
Nyama kuacha ngumu Sana,,,! Poletelea mbali, unataka uishi karne ngapi ??
 
Back
Top Bottom