kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Watu wenye mali kama nyumba, mashamba, magari, kazi, mifugo, viwanda, biashara kubwa na mali nyinginezo ni watu wenye uwezo mkubwa sana wa kuvumilia mambo, kutafakari na kusamehe. Idadi ya watu wa aina hii wakiwa wengi kwenye familia, mtaa, kitongoji, kijiji, kata, tarafa. wilaya, mkoa na nchini migogoro inakuwa michache sana, watavumilia hata kama hawapendi ili kunusuru mali zao. kwao wao "present is known"
Kinyume chake watu ambao wasiomiliki vitu vingi vya thamani kama vile familia, nyumba, mashamba, mifugo, ajira au kitu chochote cha thamani ni rahisi sana kuchokozeka na kufanya mambo bila ya kutafakari sana. Hawa ni watu ambao riziki zao wanazipata kwa taabu nyingi sana. Kama ukipakana na watu wa aina hii kwenye mtaa wako itakubidi kukaa chonjo na chukua tahadhari, maana wanao uwezo mkubwa wa kufanya chochote na lolote wakati wowote. Na mabadiliko makubwa sana ya mifumo duniani huwa yanasababishwa na kundi hili la watu.
Wakati makundi haya ya watu wasiokuwanacho yakiongezeka duniani kutokana na mifumo ya utawala, hali ya hewa na utandawazi njia pekee ya kuzuia machafuko zaidi na migogoro ni kuimarisha mifumo ya kutoa haki na kupunguza matumizi ya nguvu za dola kwa wananchi.
Ni haki pekee inayoweza kuwatuliza watu wenye njaa waliokata tamaa.