Wasiopenda Uhuru wa Vyombo vya Habari, Siasa, na Katiba Mpya wana nia gani na Tanzania?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Group 1. Kuna Watanzania ambao wanaamini nchi yetu inahitaji dikteta ambaye ataendesha nchi kimabavu na kuwa kama Mungu mtu.

Dikteta ambaye awe na uwezo wa kufunga yeyote, kuuwa yeyote na kufanya lolote kwasababu yeye ndiye atakayejua nani ni muhimu na manufaa kwa taifa.

Huyu mtu Mungu ndiyo yeye atuambie watu milioni 62 nani ni mzalendo na nani ni msaliti. Kuna wanao amini kabisa kwamba hii ndiyo style ya kuendeleza nchi yetu.

Group 2. Lakini kuna wengine wanasema nchi inahitaji haki kwa kila mwananchi kuchagua watu wa kuwaongoza, tutaendelea kwa biashara huru na za ushindani na uwazi wa nchi na mawazo ndiyo utatufanya tuendelee.

Lakini hawa wanaamini tuwe na katiba nzuri ya nchi bila kujali chama au vyama vya siasa. Hawa wanaamini tutaendelea kwa kuwa na katiba nzuri yaani mfumo mzuri na sio kuwa na mtu mzuri kwasababu kama unaweza kuwa na kiongozi mzuri vilevile unaweza kuwa na kiongozi mbaya.

Tumeshaona kuna madikteta mazuri na kuna madikteta wabaya. Lakini tukiwa na mfumo mzuri hata kiongozi akiwa mbaya bado nchi itaenda mbele au wananchi wataweza kumtoa kwa kupitia kura.
 
Hao wanaotaka kuwa na dikteta hebu waambie huyo dikteta basi awe Samia
Watakupinga watasema hafai, sasa utashangaa wanataka dikteta halafu hapo hapo wanataka kumchagua huyo dikteta awe nani, yaani wanataka udikteta na wanataka demokrasia hapo hapo
 
Group 1. Kuna Watanzania ambao wanaamini nchi yetu inahitaji dikteta ambaye ataendesha nchi kimabavu na kuwa kama Mungu mtu. Dikteta ambaye awe na uwezo wa kufunga yeyote, kuuwa yeyote na kufanya lolote kwasababu yeye ndiye atakayejua nani ni muhimu na manufaa kwa taifa. Huyu mtu Mungu ndiyo yeye atuambie watu milioni 62 nani ni mzalendo na nani ni msaliti. Kuna wanao amini kabisa kwamba hii ndiyo style ya kuendeleza nchi yetu
Yes kuna mahali Tanzania tulifika tukafanywa shamba la bibi too much hivyo tukamuhitaji mtu udikiteta Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba! na baada ya kukamilisha kazi, akaitwa kupangiwa kazi nyingine.
Group 2. Lakini kuna wengine wanasema nchi inahitaji haki kwa kila mwananchi kuchagua watu wa kuwaongoza, tutaendelea kwa biashara huru na za ushindani na uwazi wa nchi na mawazo ndiyo utatufanya tuendelee. Lakini hawa wanaamini tuwe na katiba nzuri ya nchi bila kujali chama au vyama vya siasa. Hawa wanaamini tutaendelea kwa kuwa na katiba nzuri yaani mfumo mzuri na sio kuwa na mtu mzuri kwasababu kama unaweza kuwa na kiongozi mzuri vilevile unaweza kuwa na kiongozi mbaya. Tumeshaona kuna madikteta mazuri na kuna madikteta wabaya. Lakini tukiwa na mfumo mzuri hata kiongozi akiwa mbaya bado nchi itaenda mbele au wananchi wataweza kumtoa kwa kupitia kura.
Ndipo tukaletewa Samia Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
P
 
Mimi niko group 2
 
Hao wanaotaka kuwa na dikteta hebu waambie huyo dikteta basi awe Samia
Watakupinga watasema hafai, sasa utashangaa wanataka dikteta halafu hapo hapo wanataka kumchagua huyo dikteta awe nani, yaani wanataka udikteta na wanataka demokrasia hapo hapo
Hayo ndio maajabu
 
Kuna watu walinufaika sana na udikteta, sasa wanapoambiwa tunarudi kulekule kwa kukimbizana mchakamchaka na vijana wa upinzani tena wengine watoto wadogo kabisa waliomaliza chuo juzi tu hapa lazima matumbo yajae gesi. Tuwasamehe.
 
Yes kuna mahali Tanzania tulifika tukafanywa shamba la bibi too much hivyo tukamuhitaji mtu udikiteta Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba! na baada ya kukamilisha kazi, akaitwa kupangiwa kazi nyingine.

Ndipo tukaletewa Samia Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
P

Tatizo la udikteta ni kwamba hawaondoki mfano wenzetu wa Uganda wamepata dikteta mzuri Museveni lakini wangepata mbaya leo Uganda ingekuwa wapi kuanzia 1986

Kwa mawazo yangu tuwe na katiba nzuri na idara imara kiasi kwamba tusitegemee hero
 
Back
Top Bottom