Wasiostahili kurudi bungeni 2010

Idd Azan
Hassan Zungu
Mohamed Abdulaziz
Wabunge wote ambao ni wakuu wa mikoa na kusiwe na Wabunge wa viti Maalum
 
Last edited:
Naona ulingo umechafuka ngoja tuwapishe wenye nguvu
 

JF kuna wakongwe kumbe, watu wanakumbuka mambo ya mwaka 1984 yaliosemwa na mzee Malecela.
Ndugu Pretty,

Hata darasa la nne anafundishwa harakati za Tanganyika ya 1929 ilipoanza African Association, chimbuko la CCM, kwa kuwa inafahamika ili kuelewa na kuchambua contemporary events za 2009, unaweza kuhitaji kujua ya 1929.

Kama unadhani political dynamics za mwaka 1984 ni za zamani mno na zenye upeo wa kina mno, huenda jamvi la siasa za Tanzania halikufai. Hapa wanakuja watu wa kila aina, wakiwemo watu wazima waliokuwepo na kukumbuka ya mwaka 1984. Sio teen social network. Naelewa hukuwepo au ulikua hujapevuka wakati huo, au hutaki tu kupata headache kwa mambo ya 1984, vema kabisa.

Basi tuna mabaraza lukuki humu ambavyo hayahitaji sana kunyanyua vyuma vya mawazo na historia na kumbukumbu. Si lazima uende mbali sana kwa Michuzi au DarHotwire kupata utakayo jisikia uko nyumbani, hata hapa tuna maswala ya mahusiano, ususi, vichekesho, filamu, na agenda nyingine za burudani ambazo unaweza kujikita ukawa comfortable kama ulivyoonyesha mwongozo hapa.
 

Mkuu nina wasiwasi sana na suala la kutaka kuwanyima haki watu wenye umri mkubwa kwa kutumia low perfomance ya Kingunge kama kigezo. Si wazee wote wako ovyo na sio vijana wote ni wazuri. Angalia Kina Masha wanavyo perfom, au serikali nzima iliyoingia madarakani kwa gear ya vijana. Jaribu kuangalia serikali ya sasa na zilizopita uone wapi kuna umakini. Ipi ulikuwa na vijana na ipi ina wazee, then tuwashutumu uangalie kama inalingana na ulichosema.
 
Lucas Selelii- Nzega. jamaa hajafanya chochote Nzega zaidi ya kuwagawa watu kuwa wangu hawa si wangu halafu mahudhurio yake ya shule hasa ya msingi nadhani hayakuwa mazuri!
 
Yono Stanilaus Kevela - Njombe magharibi, aliomba bungeni wenye HIV wawekwe alama.
 
Sidhani kama na wewe umetumia muda wa kufikiri kisha ukaandika maana inaonyesha una mawazo mgando kiasi kwamba unadhani mtera hakuna mtu anayeweza kuongoza kuliko huyo mbunge unayemfikiria! Maana akitoka tu tumekwisha, me sidhani kama tutakwisha kama unavyotaka iwe, kwetu mtera kuna
watu wanauwezo wa kuongoza na wataendelea kuwepo! Kwani kuna nini alicho kifanya muda wote hou wa ubunge na mwingine ashindwe kufanya "Zaidi" kwa muda huo.
Ushauri wangu Nenda ukanywe maziwa uondoe sumu ya fikra potofu!
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 


LOL.. waafrika kwakuwa condescending hatujambo.. If only it were a virtue to be proud of.
 

Mkuu,

Hiyo sheria ya umri wamejiwekea ili ikiwezekana wafie hapo. We huoni ajabu mtu ambaye anasupervise watu 10+ kwenye kampuni anaambiwa astaafu at 60. Wakati mbunge anayewakilisha 200K na rais anayeongoza watu 40 millioni wanaendelea kupeta hata wakiwa na 80 yrs. Hivi hii sheria ya kustaafu at 60 yrs ina maana gani??? Kama ni kweli inatokana na kupungua kwa uwezo wa mtu kufanya kazi baada ya 60 yrs (kama ninavyoamini) then iweje mtu wa 70+ awe na uwezo wa kutuongoza vizuri??

Hata kwenye vitabu vitakatifu huwa wanasema umri wa mtu ni miaka 70. Sasa wazee kama hawa muda wao ushapita....................!!!!!!!!!!!!!
 


Halafu sura ya huyo mzee kingunge inaniharibia wanangu mara wakimuonyesha tu kwenye TV watoto wote manalia muzimuuuu muzimuuuu baada ya hapo wote usingizi foo foooo fo!.....kwi....kwi....kwiii
 
mbunge wa magogoni hatakiwi kurudi
sababu
1. anapenda sana kutembelea majimbo ya watu wengine
2. tokea ameshika jimbo lake hamna maendeleo yeyote wala hana mikakati ya kuliendeleza, amemaliza savings zote alizoachiwa na mbunge aliyopita
na mengine mengi tu
 
Anna Kione Kilango Malecela-Same Mashariki. jimbo la Same Mashariki liko nyuma kuliko majimbo yote katika mkoa wa Kilimanjaro. Same Mashariki iko nyuma ktk elimu,afya,maji,mazingira,misitu,kilimo,barabara.
Unataka Anne Kilango ayabebe hayo maendeleo kichwani ayapeleke? Ikiwa Fisadi Yona hakuweza ataweza Kilango ndani ya miaka 5 na kwa namna gani...

Ni lazima Rost tamu atakuwa amekutuma umsemee..... Tehe tehe Nkho...
 
Waondolewe wote wa SSM isipokuwa Anna Kilango Malecela, Aloyce Kimaro, Lukas Seleli, Ole Sendeka, Harrison Mwakyembe, Eng. Stelah Manyanya na Magufuli. Waliobaki ni mzigo kwa taifa hili, ingewezekana wangeondoka sasa hivi tuteue wa kushikia nafasi zao kama ilivyokuwa kwa Tabo Mbeki!!!! Any, way ni kwa kuwa wengi wanachaguliwa kwa kutoa takrima kwa wananchi sasa kuwatoa hivi hivi tena ni ngumu. Nafurahi, 2010 si mbali.

Wa upinzani wabaki ila wapange mikakati ya kuongeza idadi yao Bungeni!!! Ni kwa vipi, nategemea kwa sasa wameshajipanga, vinginevyo 2010 ni ndoto, hata hivyo viti vichache walivyo navyo wanaweza kuvipoteza!!! Kazeni boot wapinzani!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…