Wasiostahili kurudi bungeni 2010


Mkuu hata kama hajafanya kitu lakini jimboni mwake wanampenda sana kwa sababu ni waziri.

Na ameweza kusaidia jimbo lake likawa na makao makuu ya wilaya Bunazi/kyaka misenye karibu na mtukula badala ya kuwa katikati ya jimbo lake kama ilivyo jina la jimbo lake la uchaguzi Hivyo kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha wananchi wake.

Na pia ameweza kuhama kutoka katika kijiji chake na kusogea karibu na kagera sugar
 
Jina la Mbunge:ROSTAM AZIZ
Jimbo lake:IGUNGA
Chama Chake:CCM
Muda aliokaa bungeni(ikiwezekana sio umri please):MIAKA 16
Sababu za kukataa kurudi kwake:HACHANGII ISSUES BUNGENI

Kwa nini achangie wakati wananchi wake wameridhika na hata akigombea atapata tu?
 
kwa kuwa mie ni mkazi wa ukonga,nilitaka pia Makongoro asirudi bungeni,kwa sababu kama hizo hapo juu mie kura yangu hapati,ameanza kampeni na pati ya kukuaribisha mwaka 2010.wanaukonga tumsurubu huyu, kam vile kumkoma nyani giladi.
 
Jina: Zitto Kabwe
Jimbo: Kigoma
Sababu: Amedhihirisha udhaifu mkubwa kwenye kutoa maamuzi makini, ni mpiga soga asiye na nidhamu na hafai kuitwa kiongozi kwa tabia yake chafu ya uhuni ikiwa pamoja na kufikia kumvisha mbwa bendera ya CCM kule Tarime na kuchoma moto bendera kadhaa za CCM hukohuko Tarime, ni kigeugeu ndani ya chama chake, anafuata upepo badala ya fikra, anatia kichefuchefu hata kumuona bungeni, anapenda umaarufu badala ya kufanya kazi, aliwahi kudangaya bunge mara kadhaa hadi akafukuzwa, ana jazba za jino kwa jino, hata kigoma wanamuona msanii na juha wa siasa.
 
Unanikumbusha wakati fulani alipokuwa akifanya kampeni mwaka 2005, mtu fulani akasema, si bora hata mke wake angegombea maana huyu jamaa tangu nianze kumsikiliza haonyeshi kuwa na uwezo wa kutuwakilisha. Afadhali hata mke wake akisimama aghalabu unaona matumaini.
 
Mie nafikiri wale wote wanaounga mkono ufisadi hawastahili kurudi, wakiongozwa na Peter serukamba na Makongoro mahanga, na wale wanaofaidisha familia zao pia wasirudi bngeni
 
Jina la Mbunge:ROSTAM AZIZ
Jimbo lake:IGUNGA
Chama Chake:CCM
Muda aliokaa bungeni(ikiwezekana sio umri please):MIAKA 16
Sababu za kukataa kurudi kwake:HACHANGII ISSUES BUNGENI
Tatizo la huyu jamaa haongei bungeni lakini cha ajabu wananchi wake wengi wanampenda!!!!!!
Jina la Mbunge: Elisa Mollel
Jimbo lake: Arumeru Magharibi
Chama Chake: CCM
Muda aliokaa bungeni(ikiwezekana sio umri please): 15years
Sababu za kukataa kurudi kwake: Anataka kufanya ubunge ni ufalme eti anasema akitoka atamwachia mwanae. Hachangii pia bungeni, hatembelei wananchi wake mara kwa mara.
 

Huyu atoke tu kabisa mapema, hatumtaki kabisa!
 
Mbona hata Mo Dewji huwa haongei wala kuchangia mada Bungeni lakini anafanya kazi nzuri sana kule Singida? Na wananchi wake wanampenda!

Ubunge sio kupiga kelele Bungeni na kuwa mtu wa kuandikwa magazetini na kuonekana luningani kila siku, Ubunge ni kuchapa kazi.
 
watu wengi wanadhani mtu muongeaji ndiyi anafanya kitu cha maana...kuna wengine siyo watu wa kuongea sana ila matendo yao ni mazuri huko kwenye majimbo yao....siyo lazima uonekane unaongea sanaaaa!.....mtu anayeongea sana ni comedian tuu hajui nini afanye ku make changes.
 

kuongea si ndio karakta ya mwanasiasa?sasa miaka mitano huzungumzi bungeni si ungekaa home tu....kuna miswada ya kuchangia....walionunua ubunge wote mabubu...
 
Rostam achape mwendo

Jimboni kwetu wanampenda sana, yaani hata hilo neno ufisadi kule ni msamiati mpya ambao wala hawaelewi maana yake!

Mimi najua kwanini wanampenda, anajitahidi kufanya kazi nzuri jimboni kwake. Mfano barabara ya kwenda kijijini kwetu inapita wakati wote wa mwaka, kuna miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji, kuna zahanati na gari la wagonjwa, kuna umeme wa gridi ya taifa (ambao hata mkoa wa Kigoma kwa ujumla wake hauna), shule za msingi kadhaa na moja ya sekondari. Pia siyo mvivu kutembelea jimbo lake la uchaguzi. Huwa si mtu wa kusubiri mpaka kipindi cha uchaguzi kifike.

Hilo la tuhuma za ufisadi ni suala lingine kabisa kwa wananchi wa jimboni kwake. Ukitaka kushindana naye ingia na gia nyingine lakini sio huo msamiati wa ufisadi. Watu wa vijijini hata magazeti hawapati kwa hiyo wengi wao hawaelewi ufisadi ni nini.
 
kuongea si ndio karakta ya mwanasiasa?sasa miaka mitano huzungumzi bungeni si ungekaa home tu....kuna miswada ya kuchangia....walionunua ubunge wote mabubu...

I am sure nusu ya hiyo miaka mitano lazima aliongea..siyo kwamba watu walikuwa bubu kipindi chote cha bunge....kama kuna point muhimu na inamuhusu i am sure wanachangia...inategemea lakini kama hapa jf siyo kila mtu anachangia everywhere lazima kuwa area fulani upo makini......lakini kama hasaidii jimbo lake kendeea hiyo ndiyo sekta muhimu ya ku-dela naye na kuweza kumuangusha kisiasa...maana wanasema don't judge a book by it's cover....

Kuna mtu katoa mfano wa Dewji kuwa yupo bubu bungeni na mwingine kasema lakini he is doing great job katika jimbo lake.....so utamtoa kisa haongei au??
 
Majukumu ya mbunge ni nini kwa uelewa wako?
 
wabunge wote wa mkoa wa mikoa ya shy na mwanza hawastahili kabisa.
Sababu wameshindwa kutetea raslimali za mikoa yao,wawekezaji wanalamba madini yote na wananufaika sana kuliko wazawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…