Wasiotaka kustaafu kwetu, ya Malkia UK wanayatamani hapa

Wasiotaka kustaafu kwetu, ya Malkia UK wanayatamani hapa

Ama kwa hakika Kenya wamepiga hatua kubwa sana.

View attachment 2353770

Kwetu wastaafu hawataki kustaafu na wanalazimisha watoto kuja kutawala.

Nini tofauti yetu na Kenya?

Kupi kufanana kwetu na Uganda, Burundi au Rwanda?

Pole yetu Tanzania.
"Kuhusu Kurithiana"

Kwanini Kenya Mbona Kama Mfano Wako Kama Si Sahihi?

Uhuru Kenyatta Si Mtoto Jomo Kenyatta ?

Na Hata Raila Odinga Sio Mtoto wa Jaramogi Oginga Odinga ?

Au Mimi Ndio Nimekuelewa Vibaya?

Inawezekana Kenya Wametuzidi Sawa Lakini SinKatika Hili.
 
Kwetu hata mbumbumbu wa kishua bado anapewa kazi kubwa na hata uongozi
Ingawa elimu yetu ni ya kukariri tofauti na wenzetu
Sisi ukitaka kumuelewesha kiongozi au boss kama hajui utasikia UNANIFUNDISHA KAZI WEWE
Hii ni udhaifu wa mtu asie na uelewa huku akiwa amevaa viatu vinavyompwaya

Ila wenzetu ukiangalia wanavyojadili mambo utajua anaitendea haki taaluma yake
 
"Kuhusu Kurithiana"

Kwanini Kenya Mbona Kama Mfano Wako Kama Si Sahihi?

Uhuru Kenyatta Si Mtoto Jomo Kenyatta ?

Na Hata Raila Odinga Sio Mtoto wa Jaramogi Oginga Odinga ?

Au Mimi Ndio Nimekuelewa Vibaya?

Inawezekana Kenya Wametuzidi Sawa Lakini SinKatika Hili.

Sina uhakika kama uliupitia uzi vyema kujielekeza kwenye yaliyo mapya. Post #2 Ina majibu ya maswali yako.

Au wewe ni mlamba asali? Si unajua ugumu wa nyani kuona kun*ule?
 
Kwetu pa ajabu kidogo, hawa wetu wanabebwa na baba zao tena wala sio kwa kuchaguliwa na wapiga kura, wanawaibia kura, wanaingia madarakani wanaanza kutuibia huku wengine wakiwaita hao wajinga "genious".

Kama wangekuwa "genious" kwanini wasianzishe biashara/kampuni zao, waajiri watanzania wengi wasiokuwa na kazi ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira lililokuzwa na baba zao?

Hawa "genious" wetu tayari wana mitaji, lakini ajabu badala ya kuwekeza hiyo mitaji yao iwaingizie faida, wao wanaendelea kuiba na kujilimbikizia mali, hawa ndio "role model" wa baadhi ya wajinga.

Muda umefika kuwapigia Hawa watu kipyenga cha offside. Hii nchi ni yetu sote. Tufike mahali tutoleane uvivu.
 
Back
Top Bottom