Kwetu pa ajabu kidogo, hawa wetu wanabebwa na baba zao tena wala sio kwa kuchaguliwa na wapiga kura, wanawaibia kura, wanaingia madarakani wanaanza kutuibia huku wengine wakiwaita hao wajinga "genious".
Kama wangekuwa "genious" kwanini wasianzishe biashara/kampuni zao, waajiri watanzania wengi wasiokuwa na kazi ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira lililokuzwa na baba zao?
Hawa "genious" wetu tayari wana mitaji, lakini ajabu badala ya kuwekeza hiyo mitaji yao iwaingizie faida, wao wanaendelea kuiba na kujilimbikizia mali, hawa ndio "role model" wa baadhi ya wajinga.