- Source #1
- View Source #1
Your browser is not able to display this video.
- Tunachokijua
- Stephen Wasira ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyeteuliwa mnamo tarehe 18 Januari 2025 akimrithi mtangulizi wake katika nafasi hiyo Abdulrahman Kinana. Pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Bunda mwaka 2005 hadi 2015.
Ipo video inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha Wasira akisema 'hapa Tanzania kwa mwaka huu CCM inaogopa CHADEMA, ndiyo maana inawakamata ili ishinde uchaguzi'
Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (key words search) pamoja na marejeo ya video umejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kwa kukata na kuunganisha vipande vya video visivyohusiana kutoka kwenye hotuba ya Wasira Mwezi Aprili 25, 2025.
Akiwa wilayani Kongwa, mkoani Dodoma, Aprili 25, 2025 wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020–2025, Wasira alitumia nafasi hiyo kujibu hoja za mwanaharakata kutoka Kenya ambapo alibainisha kuwa CCM haiogopi CHADEMA. Rejea hapa Wasira alisema,
"Martha Karua anasema CCM, inaogopa CHADEMA ndiyo maana inawakamata ili ishinde uchaguzi, Martha Karua mimi nataka nimwambie asikie na wanaopeleka habari wampelekee watu wa magazeti kwamba nimesema mwaka huu hakuna chama kinaweza kuogopwa na CCM, chama gani?
Maana ukienda mahali ugenini ni vizuri ukajua mambo ya hapo kabla hujalalamika, yeye amefika tu na ndege mara akapata hoja, ya CCM inaogopa CHADEMA, CHADEMA yenyewe ya kuogopwa ipo wapi? wao wenyewe wameshatawanyika"
Wasira alitoa kauli hiyo baada ya Mwanasheria Matha Karua, kutoka nchini Kenya Aprili 24, 2025 kusema CCM na serikali wanaiogopa CHADEMA ndiyo maana wanamuweka ndani Lissu ili washinde uchakguzi.
View: https://youtu.be/bnbSM0Eoik4?si=MhD-54MaSBOElTpA&t=198