Habari za Kitaifa
Chadema Bunda kutokimbilia mahakamani
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Bunda; Tarehe: 3rd November 2010 @ 20:00 Imesomwa na watu: 204; Jumla ya maoni: 0
Habari Zaidi:
Wazee: Pinda 'hajachakachua' kura
Mgaya:Kikwete teua mawaziri wengi vijana
Meya Mpanda ashambuliwa kwa mawe
Kikwete aanza kuteua, Werema wa kwanza
Kikwete: Tulifanya kazi ya ziada tushinde
Raia wa kigeni waibiwa Dar es Salaam
Dk. Slaa aendelea kumsusia Kikwete
Aliyebwagwa Sumbawanga Mjini kukata rufaa
Hospitali Musoma ina uhaba wa madaktari bingwa
Dar yarindima, Mugabe, Zuma kivutio
EAC kutafiti ukubwa wa tatizo la ajira
Nafasi ya umeya gumzo Mwanza
Madiwani Chadema waandamana
Musiba azikwa Musoma
Kikwete ashinda, Slaa asusa
Lowassa:Slaa anakurupuka, mzushi
Lipumba ataja kasoro za uchaguzi 2010
Anna Abdallah kuwania uspika
Pinda: Wapinzani wametoa changamoto CCM
Upinzani waongeza viti vya udiwani Morogoro
Habari zinazosomwa zaidi:
Balaa lingine kwa Chenge
Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
‘Housigeli' anataka kuniharibia ndoa
Vatican yamvua jimbo Askofu
Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
ALIYEKUWA mgombea ubunge Jimbo la Bunda kupitia Chadema, Elias Maarugu, amesema hakusudii kukimbilia mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi, kwa vile ulikuwa huru na wa haki.
Amesema badala yake atashirikiana na Mbunge mteule wa jimbo hilo, Stephen Wasira
(CCM) ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika juhudi za kuliletea jimbo hilo maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo mwanzoni mwa wiki hii, Maarugu alikubaliana na uamuzi uliofanywa na wakazi wa jimbo hilo wa kumchagua Wasira.
"Sitakimbilia mahakamani; kufanya hivyo ni kuwadharau wana-Bunda kwa kile
walichokifanya.
Nakubaliana na matokeo kwani uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na isitoshe uliendeshwa kwa amani na utulivu mkubwa," alisema Maarugu.
Maarugu alitoa mwito kwa wakazi wa jimbo hilo wa vyama vyote, kutambua kuwa mchakato wa uchaguzi kwa sasa umekwisha na kilichopo mbele yao ni kushikamana kwa pamoja kulijenga jimbo lao.
Aliwataka wakazi hao kuondoa tofauti zao za kisiasa na kuwaonya kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na misingi ya demokrasia iliyokomaa nchini.
Kauli ya Maarugu inafanana na iliyotolewa na Mbunge mteule wa jimbo hilo, Wasira ya kuwataka wakazi wa jimbo hilo kushikamana kuleta maendeleo, bila kujali mambo yaliyojiri katika uchaguzi.
Aliahidi kutekeleza yale yote aliyoyaanza katika awamu yake ya kwanza ya ubunge wa
jimbo hilo, na mapya yaliyomo katika Ilani ya CCM chama chake.
Katika matokeo ya uchaguzi kwa jimbo hilo, Msimamizi wa Uchaguzi Cyprian Oyeir alisema Wasira alipata kura 27,502; Maarugu wa Chadema kura 12,224; Asetic Malagira wa NLD kura 341 na Josephine Songambele wa CUF kura 434.