GE2025 Wasira: Badala ya kulalamika fanyeni kazi muwe kama Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira, amewataka watu wanaohoji kwanini wanamsifia Mwenyekiti wa chama hicho Samia Suluhu Hassan kuacha kulalamika badala yake nao wafanye mambo mazuri ya maendeleo ili wasifiwe.

Amezungumza hayo mjini Musoma Septemba 6, 2025 kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika jimbo la Musoma Mjini, lenye kata 16 ambapo kata mbili kati ya hizo wagombea udiwani wa chama hicho wamekosa wapinzani.

Amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake Rais Samia amefanya mambo makubwa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za kijamii ikiwemo katika sekta za afya, maji, elimu na sekta zingine na kwamba chama chake bado kinalenga kufanya mambo mengine makubwa kwa wananchi.

Wasira amesema lengo la chama hicho ni kuendelea kushika dola ili kuwatumikia wananchi na ndio maana wameandaa ilani bora yenye kujibu mahitaji na changamoto zete za wananchi.

"Sasa wanalalmika nini wakati hawana chochote walichokifanya, sisi lazima tumsifie wa kwetu kwasababu amefanya mengi sana na tunayaona, sasa wewe unalalamika wakati hata zahanati haujajenga,fanya maendeleo na wewe usifiwe kwasasa tuko na mama Samia," amesema.

Wasira amesema chama hicho kina malengo mazuri na wananchi na ndio maana kimerudi tena kuomba ridhaa ya kushika dola huku akisema katika jimbo la Musoma mjini na mkoa mzima wa Mara yapo mengi mazuri yaliyopangwa kufanyika kwa maslahi ya wakazi wa jimbo hilo.

Chanzo: Jambo TV
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amewataka watu wanaohoji kwa nini wanamsifia mwenyekiti wa chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan kuacha kulalamika na badala yake nao wafanye mambo mazuri ya maendeleo ili wasifiwe.

Akizungumza Mjini Musoma mkoani Mara kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM katika Jimbo la Musoma Mjini, Wasira amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake Dkt. Samia amefanya mambo makubwa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za kijamii na kwamba chama hicho bado kinalenga kufanya mambo mengine makubwa kwa wananchi.

Amesema lengo la CCM ni kuendelea kushika dola ili kuwatumikia wananchi na ndio maana wameandaa ilani bora yenye kujibu mahitaji na changamoto zete za wananchi.

"Sasa wanalalamika nini wakati hawana chochote walichokifanya, sisi lazima tumsifie wa kwetu kwa sababu amefanya mengi sana na tunayaona, sasa wewe unalalamika wakati hata zahanati haujajenga, fanya maendeleo na wewe usifiwe. Kwa sasa tuko na mama Samia," amesema Wasira.
1757231020137.png
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira, amewataka watu wanaohoji kwanini wanamsifia Mwenyekiti wa chama hicho Samia Suluhu Hassan kuacha kulalamika badala yake nao wafanye mambo mazuri ya maendeleo ili wasifiwe.

Amezungumza hayo mjini Musoma Septemba 6, 2025 kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika jimbo la Musoma Mjini, lenye kata 16 ambapo kata mbili kati ya hizo wagombea udiwani wa chama hicho wamekosa wapinzani.

Amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake Rais Samia amefanya mambo makubwa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za kijamii ikiwemo katika sekta za afya, maji, elimu na sekta zingine na kwamba chama chake bado kinalenga kufanya mambo mengine makubwa kwa wananchi.

Wasira amesema lengo la chama hicho ni kuendelea kushika dola ili kuwatumikia wananchi na ndio maana wameandaa ilani bora yenye kujibu mahitaji na changamoto zete za wananchi.

"Sasa wanalalmika nini wakati hawana chochote walichokifanya, sisi lazima tumsifie wa kwetu kwasababu amefanya mengi sana na tunayaona, sasa wewe unalalamika wakati hata zahanati haujajenga,fanya maendeleo na wewe usifiwe kwasasa tuko na mama Samia," amesema.

Wasira amesema chama hicho kina malengo mazuri na wananchi na ndio maana kimerudi tena kuomba ridhaa ya kushika dola huku akisema katika jimbo la Musoma mjini na mkoa mzima wa Mara yapo mengi mazuri yaliyopangwa kufanyika kwa maslahi ya wakazi wa jimbo hilo.

Chanzo: Jambo TV
Ujinga pro max
 
ghows-LS-6757fc51-c656-459c-bf45-a6dd1a6b0f28-8009f37d.jpeg

Hivi TANAPA wako wapi na kwa nini hawaikamati hio sokwe wairudishe msituni... ?
 
Moderators naomba muachie Uzi wangu wa "namna ya kutambua madini na bei zake
 
Topic za maccm yasipewe airtime humu kama kiongozi wao anaona this platform is useless akaanzishe ya kwake mambuzi yote yaende huko
 
Nikifikiria kwamba mamilioni ya kodi nayolipa yanachangia kujenga miundombinu halafu wanamsifia mtu ambaye mshahara wake haukatwi kodi; roho inaniuma tu.
 
Kujenga miundombinu gani...makodi unayolipa yanaenda kwa samia na familia yake!
 
Kwa umri alionao Wasira hawezi kuchambua mema na mabaya.
 
Back
Top Bottom