Wasira: Demokrasia Lazima Ianzie Ndani ya CCM, Wanachama Wawe na Uwezo wa Kuamua Yanayohusu Chama Chao

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kuwa mfano wa demokrasia nchini, kikisisitiza kuwa misingi hiyo inaanza ndani ya Chama chenyewe.

CCM imesema imekuwa ikizingatia misingi ya demokrasia katika uendeshaji wa shughuli zake, ikiwemo katika mchakato wa uchaguzi wa viongozi wake.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Stephen Wasira alipokuwa akifungua mafunzo ya Iitikadi na uenezi kwa makada wa Chama yaliyofanyika katika Chuo cha CCM, mkoani Iringa, jana.

Wasira akisema uchaguzi unaofanyika ndani ya CCM unalenga kutoa nafasi kwa wanachama kushiriki katika kuwachagua viongozi wanaowataka kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuhakikisha misingi ya demokrasia inaendelea kuimarika ndani ya Chama.

Aidha, alivitaka vyama vingine vya siasa nchini kuiga mfano huo kwa kuhakikisha vinazingatia demokrasia katika shughuli zake na uchaguzi wa viongozi wao.

Makamu Mwenyekiti Wasira alisisitiza kuwa, demokrasia ni muhimu katika kujenga vyama imara, vinavyoweza kuwajibika kwa wanachama na wananchi kwa ujumla.

Kwa upande mwingine, alisema CCM haiwezi kuingilia mihimili ya dola kwa kuwa kila mhimili una majukumu yake kwa mujibu wa Katiba na sheria.

Alieleza kuwa, Mahakama ni miongoni mwa mihimili inayopaswa kutekeleza majukumu yake kwa uhuru na kwa kuzingatia sheria.

Wasira alibainisha kwamba, kuheshimu mgawanyo wa madaraka ni sehemu muhimu ya uendeshaji wa nchi kwa misingi ya kikatiba.

Hivyo siyo sahihi kwa chama cha siasa kuingilia utekelezaji wa majukumu ya Mahakama au mhimili mwingine unaotambulika kikatiba.
 
Hivi mzee wetu Wasira hajui kwamba kila Uchaguzi wao kuna wagombea huenguliwa na wengine hukatwa majina yao hata kabla ya wanachama kuwapitia kura?

Sababu utaambiwa hana sifa, hizo sifa gani ambazo hazikuanishwa ndani ya Katiba? Huu mpango wa kila chama kuwa na Utamafuni na utaratiby wake kinyume cha Katiba ndio chanzo cha kuenguliwa wagombea ndani ya vyama na ndio sababu kubwa baadhi ya Wanasiasa wanahama Chama kujiunga na chama kingine japokuwa Kiitikadi bado ana imani na Chama.
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kuwa mfano wa demokrasia nchini, kikisisitiza kuwa misingi hiyo inaanza ndani ya Chama chenyewe.

CCM imesema imekuwa ikizingatia misingi ya demokrasia katika uendeshaji wa shughuli zake, ikiwemo katika mchakato wa uchaguzi wa viongozi wake.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Stephen Wasira alipokuwa akifungua mafunzo ya Iitikadi na uenezi kwa makada wa Chama yaliyofanyika katika Chuo cha CCM, mkoani Iringa, jana.

Wasira akisema uchaguzi unaofanyika ndani ya CCM unalenga kutoa nafasi kwa wanachama kushiriki katika kuwachagua viongozi wanaowataka kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuhakikisha misingi ya demokrasia inaendelea kuimarika ndani ya Chama.

Aidha, alivitaka vyama vingine vya siasa nchini kuiga mfano huo kwa kuhakikisha vinazingatia demokrasia katika shughuli zake na uchaguzi wa viongozi wao.

Makamu Mwenyekiti Wasira alisisitiza kuwa, demokrasia ni muhimu katika kujenga vyama imara, vinavyoweza kuwajibika kwa wanachama na wananchi kwa ujumla.

Kwa upande mwingine, alisema CCM haiwezi kuingilia mihimili ya dola kwa kuwa kila mhimili una majukumu yake kwa mujibu wa Katiba na sheria.

Alieleza kuwa, Mahakama ni miongoni mwa mihimili inayopaswa kutekeleza majukumu yake kwa uhuru na kwa kuzingatia sheria.

Wasira alibainisha kwamba, kuheshimu mgawanyo wa madaraka ni sehemu muhimu ya uendeshaji wa nchi kwa misingi ya kikatiba.

Hivyo siyo sahihi kwa chama cha siasa kuingilia utekelezaji wa majukumu ya Mahakama au mhimili mwingine unaotambulika kikatiba.
Subiri hadi utekwe na wewe ndiyo utaacha unaa na kuwa Mzalendo kwa taifa na kubali ipatikane katiba mpya
 
Nchimbi katuambia tuipambanie katiba kesho yake mkamteka.
 
Back
Top Bottom