Pre GE2025 Wasira: Hatukatai mazungumzo, lakini hatuwezi kuamrishwa, asisitiza sera ya Samia ya 4R

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chadema watakuwa wajinga iwapo wataamua kufurahia matunda ya maridhiano eti kwa sababu walifutiwa kesi wakati kesi zenyewe zilikuwa za kubumba
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema chama hicho ni chama kiongozi cha ukombozi na hakikatai mazungumzo na kitafanya na mtu au taasisi yoyote, si vyama vya siasa pekee.

View attachment 3217773

Wasira amesema kuna watu wanazungumza kwa kusema "No reform, no election," akisisitiza: "Sera yetu ya 4R inakubali kuzungumza, hatukatai kuzungumza, lakini hatuwezi kuamrishwa."

Wasira amesema hayo leo Jumatano, Januari 29, 2025, alipozungumza na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Geita katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa CCM.

Katika maelezo yake, Wasira amesema yamewahi kufanyika mazungumzo baina ya Serikali, CCM, na Chadema, ambapo Chadema walikuwa na hoja 11. Miongoni mwa zilizofanyiwa kazi ni kurejea kwa viongozi wao waliokuwa ughaibuni, akiwemo Tundu Lissu, Godbless Lema, na Ezekia Wenje.

"Serikali ya Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) ikawambia warudi watakuwa salama. Je, wako salama, hawako salama?" amewauliza wananchi hao na kujibiwa wako salama.

Wasira ameongeza: "Kuna watu zaidi ya 400, akiwemo Lissu, walikuwa na kesi, wakaomba zifutwe, na waliokuwa wamefungwa jela walipata msamaha wa Rais kwa mamlaka aliyonayo. Wanasema maridhiano hayakuleta nafuu, sasa hiyo si nafuu?"

Soma, Pia:

Wasira awatetemesha akina Tundu Lissu na Wenzake: "Kauli Mbiu ya "No Reform, No Election" Haina Maana Kwa Sasa"
Sidhani kama wasira anajitambua kuwa yeye sio msemaji au afisa yeyote wa serikali bali ni m/mwenyekiti wa ccm.
 
Kwa uyu mzee bado ataka maneno , kombora la leo halijamuingia ,vizuri, mda wa siasa kwa uyu mzee hauko upande wake, anafikili akishafungw rubega basi anaona bado ni Dam mpya ya kushindana na Dam mpya.

Mzee wasira kaa kimia
 
Naona wanaanza kulegeza misimamo. Watakubaliana tu kufanya reform kama ambavyo ipo kwenye 4R
 
Back
Top Bottom