Akizungumza katika mahojiano na shirika la habari la DW yaliyochapishwa leo Julai 22, 2026, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amesema kwa sasa Tanzania kuna mporomoko wa maadili na uzalendo akitolea mfano tabia inayozidi kuenea ya watu kushangilia na kutukana pindi wanapofariki viongozi wa kisiasa. Amesisitiza kuwa vitendo hivyo ni vigeni kwa utamaduni wa Kitanzania
"Sasa hivi katika Tanzania kuna watu unaweza ukasoma kwenye mtandao mtu amekufa wanashangilia. Hatukuwa na Tanzania namna hiyo! Lazima tuchanganyikiwe, hata Ulaya hawashangilii kufa mtu kabisa.
Hata wakifa mahasimu wa kisiasa, wote mnaenda mnazika maana huwezi kuadhibu marehemu. Hata kama angekuwa ametenda mambo ya namna gani lakini akishakufa, Mungu ndiye amemchukua."