PreGE2025 Wasira kuna Mtu mmoja adaiwa kutoa laki moja kwa Wajumbe kila Mwezi kujitengenezea mazingira ya kugombea 2025

PreGE2025 Wasira kuna Mtu mmoja adaiwa kutoa laki moja kwa Wajumbe kila Mwezi kujitengenezea mazingira ya kugombea 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amefichua kuwepo kwa tuhuma za mtu mmoja anayehusishwa na kugawa fedha kwa wajumbe wote wa CCM Wilaya ya Ilala kiasi cha shilingi laki moja kwa kila mwezi, kwa lengo la kujitengenezea mazingira ya jina lake kupitishwa katika harakati za kuwania uongozi.

Akizungumza kama Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilala, uliofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi, Wasira ameeleza kuwa vitendo hivyo ni kinyume na maadili ya chama na vinaashiria matumizi mabaya ya rasilimali. Jimbo la Ilala kwa sasa lipo chini ya Mbunge na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azan Zungu.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Wasira amesisitiza kuwa CCM haitavumilia vitendo vya rushwa wala mikakati ya kificho inayolenga kuvuruga misingi ya demokrasia ndani ya chama, huku akitoa rai kwa wanachama kuwa waangalifu na watu wanaotumia fedha kama chambo cha kuwania madaraka.

 
Back
Top Bottom