The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa katika kura za maoni mwaka huu, wanachama wa chama hicho watapewa majina matatu pekee ya wagombea watakaoshindania nafasi ya kupeperusha bendera ya chama katika nafasi ya ubunge.
Akihutubia wananchi wa Tunduma Machi 15, 2025, Wasira ameonya wale wanaotegemea kutumia fedha badala ya hoja kushawishi wapiga kura.
Alisema kuwa CCM inawachunguza na endapo watabainika, wataelekezwa kutumia fedha zao kwa kuanzisha biashara badala ya kuwania uongozi.
"Hiari haiuzwi. Akina mama wanajua hili vizuri, mapenzi yanayotolewa kwa hiari hayanunuliwi. Ndio maana hata ukiwa tajiri unaweza kunyang’anywa mkeo na bodaboda kwa sababu ya hiari," alisema Wasira akifananisha siasa na uchaguzi wa wapiga kura.
Alihimiza wananchi kuchagua viongozi kwa kuzingatia hoja na si fedha