Aramun
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 461
- 2,213
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amesema kauli mbiu ya "No Reform, No Election" haina maana yoyote kwa sasa, akisisitiza kuwa muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria umekwisha kutokana na uchaguzi mkuu kukaribia.
Soma, Pia: Lissu amjibu Wasira kuhusu Katiba Mpya, asema Uchaguzi Mkuu usogezwe mbele kupata Katibu Mpya, na tutazuia uchaguzi kwa maandamano
Akizungumza Januari 23, 2025, jijini Dodoma, Wasira ameeleza kuwa badala ya kushikilia kauli hiyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanapaswa kushiriki uchaguzi na kuhakikisha wanakubaliana na maridhiano yaliyopo.
Ameongeza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, unaotarajiwa kuchagua Rais, Wabunge, na Madiwani, unapaswa kuwa nafasi ya vyama vyote kushindana kwa hoja badala ya kutafuta visingizio. Wasira amewataka viongozi wa CHADEMA kutumia nafasi za mazungumzo zilizopo badala ya kusimamia misimamo isiyotekelezeka kwa wakati huu.