Wasira: Nawapa pole wale wanaodhani hawana Uhuru wa kuongea, 2010 mambo yalikuwa magumu

Wasira: Nawapa pole wale wanaodhani hawana Uhuru wa kuongea, 2010 mambo yalikuwa magumu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, akizungumza leo Septemba 8, 2026, kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Kutafakari hali ya Kisiasa nchini, uliondaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), amesema:

"Nia ni kuleta maridhiano, na kuhakikisha Watanzania wana maridhiano kuwa hii nchi ni yao. Hakuna mtu mwenye hisani ya kusema hii Tanzania ni yangu mimi.

"Kwa hiyo kwa sababu hiyo, mawazo yenu yatawekwa maanani. Nawapa pole wale wanaofikiri hawana uhuru wa kusema.

Lakini mwaka 2021, labda waandishi wa habari watakubali hali ilikuwa ngumu kidogo kuliko sasa. Wakati ule waandishi wa habari walikuwa wanasema wakiandika wanafutwa, hawasemi.

Lakini Mama Samia alipokuja akasema: 'Andikeni, kosoweni.' Sindio waandishi wa habari? Na kwamba mtakuwa salama. Na tangu siku hiyo gazeti ambalo limefungiwa walilotoa mfano ni moja tu. Linaitwa nani lile? MwanaHALISI.

Lakini MwanaHALISI walikuwa hawandiki habari, walikuwa wanaandika uongo. Sasa uongo sio habari. Wewe unasema fulani amegoma kujiuzulu, lakini hakuna aliyemwambia ajiuzulu. Sasa hiyo ni habari au ni uongo? Sasa wakikuuliza na wewe unasema: 'Oh, samahani sana. Nilikuwa nataka kupata hela tu watu wanunue.' Lakini hiyo sio habari, unauza uongo."

 
Back
Top Bottom