DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa kwa miaka minne ya uongozi wake, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanikisha mambo makubwa, hivyo Watanzania wanapaswa kumrudisha madarakani ili aendelee kuleta maendeleo.
Wasira amesema hayo leo, Septemba 27, 2025, alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM wa Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, mjini Moshi.
“Hapa Moshi, kwa muda wa miaka minne, amejenga shule mpya nne za msingi. Sio Kilimanjaro pekee, ni hapa Moshi; madarasa mapya yamejengwa kutokana na ongezeko la idadi ya watoto 40, na wananchi hapa hamkuchangishwa,” amesema Wasira.
Ameongeza kuwa katika Sekta ya Afya, Rais Samia amejenga zahanati tisa, vituo vipya vya afya vitatu, na amerekebisha hospitali pamoja na kuweka vifaa muhimu katika vituo na hospitali.
“Vituo vya afya vilivyojengwa chini ya Mama Samia vina vifaa vyote vinavyopatikana hospitalini,” amesema.
Aidha, ameeleza kuwa jitihada hizi zimepunguza vifo vya mama wajawazito kutoka 500 kwa vizazi 100,000 hadi 100. “Huyo ndiye Samia Suluhu Hassan,” amesisitiza.