Wasira: Wanauliza mbona hatufii, na sisi tunawaambia hatufiii Ng’oo

Wasira: Wanauliza mbona hatufii, na sisi tunawaambia hatufiii Ng’oo

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mmemsikia babu wa CCM akitamba

Kumbe kuna watu wanataka wafe?
==========
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Steven Wasira, ameshangazwa na baadhi ya watu wanaohoji kwa kejeli “mbona hamfi”.

Wasira amesema ni jambo la kushangaza mtu kuuliza swali hilo kuhusu binadamu au taasisi, akisisitiza kuwa uhai wa CCM hauwezi kutiliwa shaka kwa maneno ya aina hiyo

Soma Pia: Wasira: Hatufungamani Na Upande Wowote, Tunaamua Mambo Kwa Maslahi ya Nchi

Mtu anaweza kuuliza nyinyi mna siri gani mbona nyinyi hamufi? Kwanza ni jambo la ajabu mtu kukuuliza mbona hufi... na sisi tunaambia hatufi ng'o. Kwa hiyo nataka niwaambie sisi Chama Cha Mapinduzi kilichozaliwa na Afro-Shirazi na TANU tuliachiwa kazi... Kazi ya kwanza ni kuendeleza uhuru maana tulidai uhuru na hatukutaka kuwa huru kwa muda. Tulitaka kuwa huru na uhuru uwe wa kudumu

 
Back
Top Bottom