Kumbe kuna watu wanataka wafe?
==========
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Steven Wasira, ameshangazwa na baadhi ya watu wanaohoji kwa kejeli “mbona hamfi”.
Wasira amesema ni jambo la kushangaza mtu kuuliza swali hilo kuhusu binadamu au taasisi, akisisitiza kuwa uhai wa CCM hauwezi kutiliwa shaka kwa maneno ya aina hiyo
Mtu anaweza kuuliza nyinyi mna siri gani mbona nyinyi hamufi? Kwanza ni jambo la ajabu mtu kukuuliza mbona hufi... na sisi tunaambia hatufi ng'o. Kwa hiyo nataka niwaambie sisi Chama Cha Mapinduzi kilichozaliwa na Afro-Shirazi na TANU tuliachiwa kazi... Kazi ya kwanza ni kuendeleza uhuru maana tulidai uhuru na hatukutaka kuwa huru kwa muda. Tulitaka kuwa huru na uhuru uwe wa kudumu