Wasitutoe kwenye mjadala wa Gesi kwa kuleta mada za Simba na Yanga

Wasitutoe kwenye mjadala wa Gesi kwa kuleta mada za Simba na Yanga

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2019
Posts
1,521
Reaction score
4,381
Mjadala wa Simba na Yanga umehamisha mjadala mkali uliokuwa ukiendelea juu ya uhalali wa Rais ambaye siye waziri wa Nishati na wala si mwanasheria mkuu wa serikali wala hatujaona anawashirikisha popote ghafla anaanguka sahihi hapana tunataka ulinzi wa rasilimali zetu tena kwa wivu mkubwa sana na wenye mamlaka huu urithi ungechezewa na akina Nyerere leo tusingekuwa na chochote.

Sisi Magufulists tunahoji uhalali wa kufanya usiri kwenye mikataba hii na tunahoji kauli za kuhalalisha uchimbaji wa madini kwenye hifadhi za Taifa.

Ikumbukwe kuwa uchimbaji wa madini huambatana na uharibifu wa mazingira kwa sababu ya chemicals zinazotumika kama Mercury ambazo ni heavy metals ambazo zinaitwa mutagenic agents hizi chemicals zikisambaa kwenye vyanzo vya maji ni hatari kwa wanyama wetu hasa endangered species.

Limetokea suala la kukamatwa tani moja ya Heroine nalo tunaliona la kawaida tu na tunaliacha lipite bila kufafanuliwa kuwa ule mzigo uloikuwa wa nani, wahusika wamechukuliwa hatua gani na umetektezwa wapi.
 
Kwanza kitendo cha kukamatwa tu hayo madawa tayari serikali imehusika kwenye ukamataji huo, wewe unataka mpaka ujue mzigo ni wa nani? ili iweje?

Wewe unaesema hutaki mikataba ya siri tueleze JPM ni lini aliweka wazi mikataba yake, au ile hela ya yale makinikia ililipwa lini tuanzie hapo kwanza

Tutegemee Mama atakuwa na mapungufu yake maana nae ni binadamu sio malaika, ila nakuahidi mazuri yatakuwepo pia tena mengi
 
Uzi wa kipuzz unaleta hebu nenda kajitafutie riziki huko Acha kulialia

Ova
 
Kabla ya hapo anza na kutuwekea wazi mikataba ya ununuzi wa ndege please,ukimaliza weka na wa makinikia sawa, halafu pindua na wa bwawa la mwalimu Nyerere si na lenyewe linajengwa kwenye hifadhi? Halafu wakati mwenda zake akisaini hiyo mikataba yote alikuwa waziri eti? hata hivyo bomba la gesi mzee ni kwa ajili ya kusafirisha gesi watakayonunua toka kwetu ubaya wake nini sasa? Kwa hiyo hata hiyo laini ya msongo mkubwa wa umeme kwenda Kenya nayo isijengwe kwa kuwa tutaibiwa umeme, hivi leo umevuta bangi za wapi!
 
Mimi ni mpenda maendeleo ya kweli, kwahiyo huwa sina upande( sio Magufulists wala Samiasts) Ki kubwa ninachohitaji au ninachopenda kukiona Tz ni maendeleo ya vitu na watu. Yan mimi kwa upande wng najifananisha na abiria ambae anaenda safari ya mbali huku akihitaji kufika salama na kwa wakati. Ikitokea dereva wa kwanza (ambae ni hodari) amefika njiani akapata matatizo ya kiafya na Mungu akamchukua kabla ya kufika tunapokwenda, basi hata akichukua msaidizi wake (ambae yeye mwenyew marehem alikuwa anamuamini kwa uendeshaji wake) siwezi kuwa na hofu wala wasi wasi kwan wote lengo lao ni moja tu, kutufikisha abiria wao salama na kwa muda muafaka.
 
Back
Top Bottom