Wasiwasi Mwabulambo wa Azam TV atajwa kupokea Rushwa ya Tsh. 800,000 ili aidhinishe kipindi cha TV

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Your browser is not able to display this video.

=====
UPDATES: 01 DEC 2023
=====
Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigizaji na mtengeneza filamu, Deogratius Shija, akiwatuhunu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yetu kwa vitendo vya rushwa.

Kampuni yetu inamuarifu Shija na umma kwa ujumla kuwa, haivumilii vitendo vya rushwa, udanganyifu na mbinu zozote chafu katika kusaili maudhui kwa ajili ya kuonyeshwa katika chaneli zetu, kadhalika hatupendezwi na tabia ya watengeneza maudhui kutunga shutuma dhidi ya watendaji wetu kwa sababu tu kazi zao hazikupitia kwenye chujio la kupima ubora.

Kwasababu hizo, tunatoa muda wa wiki mbili kwa Deogratias Shija, kuwasilisha ushahidi au vielelezo kuhusu tuhuma alizozitoa kwa Mkurugenzi Mtendaji au kwenye mamlaka za kisheria, TAKUKURU, Film Board, au Jeshi la Polisi, ili kuwezesha hatua stahiki zichukuliwe kwa watuhumiwa wote wanaodaiwa kuihujumu kampuni kwa vitendo vyote kinyume na taratibu za kazi.

 
Akhu mi nafatilia ubuyu wa wambea wa JF
Sijui na mimi nije na story zenu wazee wa usajili mpya?! 🀣🀣🀣🀣
Usajili mpya unamwambia kakusanye hela kwingine kwanza utamalizia hapa,ukute anakaaa mbagala πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ usafir mpaka saa tano au sita ww tu ni mwendo wa 'fwingaz'

Fwingaz
 
swahiba wangu mwabulambo ameyatimba safari hii.

naona 2023 inaisha vibaya kwa baadhi ya wadau wa sector ya media

leo nikiwa viunga vya azamtv tabata nilipishana na bibie sophia mgaza, uso wake ulikuwa umejaa unyonge sana mpaka nikamuonea huruma.

ifahamike tu kwa sasa azam media ipo chini ya uongozi wa kijana machachari patrick kahemele baada ya mzee tido mhando kujiandaa kustaafu mwishoni mwa mwaka huu.

kwa maana hiyo sidhani kama patrick ataacha hili lipite hivihivi bila kuwawajibisha wanaotuhumiwa. mda ni rafiki mzuri, tusubiri kuona kile kitakachojiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…