Wasiwasi watanda, Tume ya Jaji Chande ikikamilisha ripoti yake

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Tume.jpeg

Wakati muda wa Tume ya Kuchunguza Uvunjifu wa Amani kabla na baada ya Oktoba 29, 2025 ikikaribia mwishoni katika uchunguzi na kutoa ripoti yake, Watanzania wana kiu ya kuona ripiti hiyo itakuja na majibu gani.

Tume hiyo iliundwa Novemba 20, 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kuwepo kwa shinikizo la kufanyika kwa uchunguzi huru kuhusu matukio ya vurugu zilizosababishwa na maandamano na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Maandamano hayo yalizuka kuanzia majira ya saa 5 asubuhi katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro na baadaye kuambukiza mikoa ya Dodoma, Iringa, Njombe, Rukwa na Ruvuma, ambapo waandamanaji walipinga uchaguzi huo wakisema haukuwa huru wala wa haki.

Ndipo vyombo vya Dola vilipowakabili waandamanaji na kusababisha vifo na majeruhi kwa waliokuwa wakiandamana na wengine waliokuwa wamejificha majumbani.

Tume hiyo inaongozwa na Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Othman Chande, akiwa na Jaji Mkuu mstaafu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Stergomena Tax, Waziri wa Ulinzi mstaafu Ombeni Sefue, IGP mstaafu Said Mwema, Balozi paul Meela, Balozi David Kapya, Balozi Radhia Msuya na Balozi Joseph Madafa.

Hadidu za rejea

Akizundua tume hiyo jijini Dodoma, Rais Samia alitaja mambo saba yanayotakiwa kuchunguzwa ndani ya miezi mitatu kuwa pamoja na kuchunguza chanzo cha kadhia na sababu halisi zilizoibua vurugu, kutathmini madai ya vijana walioingia barabarani na kubaini walikuwa wanadai haki gani, kuchambua matamshi ya vyama vya upinzani, ikiwemo kauli za uchochezi zinazodaiwa kutolewa kabla ya uchaguzi.

Pia aliwataka kuangalia uhusiano kati ya vyama vya siasa na Tume ya Uchaguzi, kuchunguza mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ya ndani na nje katika matukio ya Oktoba 29, 2025, kutathmini kama kulikuwa na njia mbadala zaidi ya maandamano, uvunjifu wa amani, na vitendo vya uchomaji, ili kushughulikia changamoto kati ya tume, vyama vya siasa, na serikali.

Rais Samia aliiambia pia Tume hiyo kuangalia hatua zilizochukuliwa na vyombo vya dola kukabiliana na vurugu, na kama zilikuwa sahihi au zilikithiri.

Awali tume hiyo ilipewa miezi mitatu hadi Februari 20, 2026, lakini ilipofika tarehe hiyo ilitangaza kuongeza muda wa siku 42 ili kuipa muda kukamilisha uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Kwa nyongeza hiyo ya muda, tume sasa inapaswa kukamilisha kazi na kuwasilisha taarifa yake kabla au ifikapo Aprili 3, 2026.

Tume yapingwa

Suala la uhuru wa tume hiyo limekuwa likihojiwa mara kwa mara, ambapo tangu awali

vyama vya CHADEMA na ACT-Wazalendo vikisema haitakuwa huru, kwa kuwa Serikali ndiyo inatakiwa kuchunguzwa, hivyo aikupaswa kujichunguza.

Akizindua tume hiyo Novemba 20, 2025 Ikulu, Chamwino Dodoma, Rais Samia alisema amefanya hivyo kwa kuzingatia Sheria ya Tume za Uchunguzi ya mwaka 2023, Sura ya 32 ambayo inampa mamlaka Rais kuunda Tume za kuchunguza masuala mbalimbali ya kitaifa.

Kama hiyo haitoshi, baadhi ya wanaharakati akiwamo Rosemary Mwakitwange, Deogratius Mahinyila na Edward heche walifungua kesi kuipinga tume hiyo. Lakini Machi 13, Mahakama kUuu ilitoa hukumu ya kesi hiyo na kuyatupilia mbali madai yao.

Upinzani dhidi ya tume hiyo uliendelea hata kwenye anga za kimataifa, ambapo mapema Machi 2026), Serikali ya Uingereza ilieleza wasiwasi wake kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Tanzania, hasa kuhusiana na vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi.

Katika kikao cha Baraza la Haki za Binadamu (UNHRC) kilicgofanyika Geneva Uswisi, Balozi wa Haki za Binadamu wa Uingereza, Eleanor Sanders, liitaka Tanzania kufanya uchunguzi huru na wazi kuhusu vurugu hizo, ili kuhakikisha haki inatendeka na wahusika wa vurugu hizo wanawajibishwa.

Lakini akizungumza katika Kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Machi 2, 2026, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Abdallah Possi, alikosoa kauli zilizotolewa na Jumuiya ya Ulaya, pamoja na nchi za Uingereza, Uswisi, Sweden, Ireland, Ubelgiji na Norway, pamoja na asasi za kimataifa za Human Rights Watch na Amnesty International kuhusu matukio yaliyohusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

Dkt. Possi alisema Serikali imesikitishwa na kile ilichokiita kauli zenye kuchagua matukio bila kuzingatia muktadha na chanzo chake, hususan madai yanayohusu vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Waandishi wa habari wazuiwa kuripoti mikutano ya tume

Wakati tume hiyo ikiendelea na vikao vyake vya kuwahoji mashahidi mbalimbali, Januari 24, 2026 ilitangaza kuwazuia waandishi wa habari kuripoti mwenendo wa vikao vyake, kwa madai kuwa baadhi ya mashahidi wanataka maelezo yao yawe ya faragha.

Tangazo la kuwazuia waandishi wa habari lilitangaza na Jaji Ibrahim Hamisi Jumla wakati tume hiyo ipo wilayani Ubungo iikizungumza na mashahidi walioathiriwa na vurugu hizo.

Hatua hiyo ilifuatia taarifa mbalimbali zilizoonyesha mashahidi wakieleza matukio ya mauaji kwa hisia kali katika vikao mbalimbali mikoani. Hatua hiyo inadaiwa kufaywa ili kuficha ukweli wa atukio hayo na kupunguza hisia kali miongoni mwa wananchi.

Wasiwasi kuhusu matokeo

Wakati ikiwa imebakiza wiki moja kukamilisha muda wake wa uchunguzi na kuja na ripoti yake, kumekuwa na wasiwasi kuhusu ripoti hiyo kama itagusia muhimu, huku tayari ikidaiwa imeshatoa ripoti yake ya awali.

Mambo yanayotiliwa shaka ni pamoja na tume hiyo kumgusa Rais Samia aliyeituma kutokana na kauli zake na maamuzi yake hadi kufikia watu kuandamana? Nani aliyeagiza vyombo vya Dola kuua na kujeruhi watu hata kama hatua hiyo ililenga kulinda amani na Serikali isipinduliwe?

Je, tume hiyo itakuja na ripoti itakayoibebesha lawama Serikali na kutaja vyombo vya Dola vilivyohusika na mauaji ya wananchi wasio na hatia?

Katika maelezo ya mashahidi wengi walidai kuwa wapendwa wao waliuawa wakiwa majumbani, Je, tume itakuwa tayari kueleza jinsi vyombo vya Dola vilivyohusika na mauaji ya wananchi ambao hata hawakuhusika na maandamano hayo?

Je, tume itakuwa tayari kutaja idadi kamili ya watu waliouawa na kujeruhiwa? Waliohusika na mauaji ni kina nani na watachukuliwa hatua gani?

Kama Tume itaangusha lawama kwa CHADEMA kama chanzo cha vurugu hizo, vipi kuhusu kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu ambayo bado inaendelea mahakamani? Je, akishinda kesi itakuwaje?

Uchunguzi wa Jumuiya ya Madola umeishia wapi?

Awali kabla ya kuundwa kwa Tume ya Jaji Chande, Jumuiya ya Madola ilimtuma Rais mstaafu wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera kuja Tanzania kuchunguza yaliyotokea Oktoba 29.

Lakini baadaye ziara yake iliyeyuka bila Serikali na jumuiya hiyo kutoa taarifa yoyote.

Kufuatia hatua hiyo, Desemba 2025 kupitia mkutano wake wa 71 wa CMAG ulioongozwa na Dkt. Ian Borg Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Utalii wa Malta, uliiweka Tanzania katika ajenda maalum ya kikao cha Machi yakizingatiwa masharti manne yaliyotolewa katika kikao kilichoijadili Tanzania Disemba 2025.

Tanzania ilitakiwa kutoa nafasi iliyokamilika bila kikwazo kwa Msafara Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kuweza kukutana na wadau wote katika nafasi za mwanzo.

Pia kuondolewa kwa vikwazo kwenye uhuru wa kukusanyika na kujieleza, makundi maalum na vyombo vya habari.

Pamoja na hayo masharti mengine ni kufanyika kwa jukwaa la mashauriano kati ya vyama vya siasa ili kukubaliana mfumo wa pamoja wa hatua za kuendelea mbele kuelekea uchaguzi ujao.

Uchukuaji wa hatua za kisheria na kiutawala zilizo wazi ili kuwawajibisha wahusika wa vitendo vya vurugu na athari zake, pamoja na kutoa fidia kwa waathirika pale inapofaa.

Taarifa ya Jumuiya ya Madola iliyotolewa Machi 7, 2026 baada ya kikao cha 72 cha Kamati Maalum ya Jumuiya ya Madola (CMAG) kilichoketi jijini London Uingereza, ilieleza kuwa Dk Chakwera atatumwa tena Tanzania Machi 2026, kuchunguza matukio ya Oktoba 29.

Hayo yalielezwa baada kamati hiyo inayoshughulikia masuala ya demokrasia, utawala bora, na haki za binadamu kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum Prof. Palamagamba Kabudi.

Licha ya taarifa hiyo, hadi sasa hakuna taarifa yoyote kuhusu ujio wa Dk Chakwera nchini Tanzania.

Ujio wa mwakilishi wa UN

Mapema Machi 2026 alikuja Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika, Balozi Parfait Onanga-Anyanga kwa lengo la kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025.

Balozi Onanga-Anyanga alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Rais Samia Suluhu Hassan, wawakilishi wa vyama vya CCM, CHADEMA, ACT Wazalendo na CHAUMMA.

Hata hivyo, CHADEMA waliingiwa na wasiwasi wa balozi huyo na kumwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres, wakieleza wasiwasi wao, iwapo mwakilishi waliyekutana naye, alitumwa rasmi na ofisi yake au la.
 
Sio tume, ICC, EU Wala Washington itakayowapa watz wengi wanachomani kuhusiana na mauaji ya 29 okt. Mungu anaweza lakini huwa anachelewa sana wakati mungine. Hapa dawa ni kuishawishi Iran walau itufikirie kwa target tatu kwenye majumba ya blue. Kombora moja lije dar, lingine Dom la mwisho kidhi.
 
C
View attachment 3562124

C & P

Kutoka hapa EMILIO MZENA Kuna hekaheka kwa ajili ya Public Figure fulani
Msechu Yuko Studio kufyatua Wimbo Mpya.
 
Hapo hawatasema wametumia mabilioni kibao kufanya tume njaa. Millions of dollars have been spent, under the taxpayers' burden. 😁

Hapo bado huyo mama atawapa shukrani kwa kumsafisha. Nchi ya kufala hii. 😁
 
Back
Top Bottom