Wasomi hawa tulio nao vyuo vikuu, ni sawa?

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Inashangaza kuona wasomi wengi wa vyuo vikuu wanaadhimisha kifo cha Kanumba kwa ushawishi kutoka redio ya watu, lakini sijawaona miongoni mwao wakiadhimisha kifo cha Profesa Haroub Othman, au haya marehemu Chacha Wangwe.

Anyways, kama msomi huna tofauti na mcheza kiduku katika kufikiri na vipaumbele vyako, lazima tuisikitikie kodi ya mwananchi unayosomeshwa nayo, unayolewea, kuvaa vizuri kama msanii na kufanyia starehe munazoita 'bata'.

Nataraji siku moja serikali itaona umuhimu wa kupeleka hili fungu kusomesha wataalamu wa ukweli huko VETA na vyou vinginevyo vya ufundi vinavyozalisha wafanyakazi kuliko hivi vinavyotoa matozi na masista duu.
 
Usiwe biased! Kanumba anamchango mkubwa japo kama si mfuatiliaji ni ngumu kuuona. Kwa kazi zake wengi wameajirika, wametoka, wamejulikana kimataifa na kuifanya ardhi yetu ikajulikana. Anamengi ya kusifiwa. Ni mfano wa kuigwa kwa kujiajiri.
 
..Prof. Haroub ni nan!? Ni yule mzenj aliyekuwa 'obsessed' na Palestine-Israel-US na Mwl. Nyerere? I would rather cherish and celebrate Shivji than him. Anyways, may his soul rest in peace!
 
Hapo ndo mtu unaweza kupima uelewa wa watanzania. Nakumbuka siku Kanumba alipofariki ni siku hiyo hiyo Profesa Mutta wa pale Geology UDSM alipofariki. Ila cha ajabu hata Mlimani TV inayomilikiwa na UDSMwalitumia muda wao mwingi kwenye taarifa ya habari kuongelea kifo cha Kanumba badala ya Prof ambaye ni part and parcel ya UDSM.Sasa hao ndo Watanzania wanaodhani kua tutapiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwa kuweka msukumo mkubwa kwenye sanaa bila elimu ambayo kisingi hatuwezi fika popote
 
Je ni wanachuo wa chuo kipi? Hebu malizia habari. Au wamenunuliwa????
Naamini, hao ni wale wanaopenda mambo laini zaidi, ukiwaambia habari za Prof. Wanakumbuka mihadhara na mitihani kisha kuishiwa nguvu. Ila wakimskia Kanumba wanaona kama ahueni kwao kwa kuwa wapo tayari kuangalia maigizo na kuwapigia zogo asubuhi hata jioni.
 
Nasikitika kusema kuwa mleta mada siyo mwana historia au siyo mfuatiliaji wa mambo au ni mshabiki wa hisia na siasa. Kila mwaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam huadhimisha siku ya Prof. Haroub Othman na mara nyingi huandaliwa na UDASA, Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha umajumui wa Afrika na Taasisi ya Taaluma za Maendeleo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia hao hao huandaaa maadhimisho ya Prof. Chachage S. Chachage na kuna mfuko maalumu ambao mpaka mwaka jana nilipohudhuria maadhimisho yake pale ukumbi wa ATB ulikua na takribani milioni 35. Sasa badala ya kusema Chachage unasema Chacha wangwe anaingiaje kwenye usomi?


Sijajua mtoa mada na wanaomshabikia wanakusudio gani dhidi ya usomi wanaoujua wao maana hata aliyeuliza ni wasomi wa chuo kipi hakupewa jibu. Jamani tujitafakari kabla ya kuzungumzia maswala ya elimu. Mh. Mbatia alishasema unapogusa swala la elimu au usomi lazima utambue unagusa jambo nyeti sana si kukurupuka mradi uonekane upo na unaijua elimu au we ndiyo msomi. Kimsingi wasomi wapo na walikuwapo na watendelea kuwapo. unaweza kumaliza madgree yote unayoyajua alau ukawa msomi ila hujaelemika. tafakari chukua hatua....
 
shikamoo..naomba shilingi mia...
 

Matukio yote hayo huwa yanaandaliwa na jopo la wanazuoni, mimi nazungumzia msukumo binafsi walionao wasomi.

Ukiona wanafunzi wengi wanahudhuria kigoda cha Nyerere ujue wanafata kifungua kinywa cha bure kama kipindi kile cha mwaka juzi.
 
Vijana hawawezi kuwakumbuka maprofessor wanabifu nao kwa kuwa maprof hawatoi maksi za bure, umesahau yule aliyepost juzi akishangilia UDSM kugoma kuongeza mikataba ya maprofessor.
 
 
Usiwe biased! Kanumba anamchango mkubwa japo kama si mfuatiliaji ni ngumu kuuona. Kwa kazi zake wengi wameajirika, wametoka, wamejulikana kimataifa na kuifanya ardhi yetu ikajulikana. Anamengi ya kusifiwa. Ni mfano wa kuigwa kwa kujiajiri.
Okey, sawa kabisa. Haya, na Prof. Haroub Othman nae? Maana mleta uzi ameshabihisha.
 
ntamkumbuka sana huyu mzee,kwa bahat nzuri alinifundisha,ila kabla hatujamaliza semester ALLAH akamchukua ikabid TUTORIAL ASSISTANT WAKE AJE KUIMALIZIA ILE KOZ,MSIMAMO WAKE ULIKUA NI MMOJA TU HAKIKISHA UNASIMAMIA UKWELI KWA JAMBO UNALOLIONA,UNAFKI HAKUPENDASasa hawa wanaomshabikia kanumba kwa ujue kuwa hawamjui Profesa Haroub wala Wangwe na wala michango yao,na hata hiyo redio inayomuenzi kanumba ndio hao hao waliohusishwa na wizi wa fedha za michango ya HARUSI,NI NADRA SANA KWAO KUZUNGUMZIA MAMBO SENSITIVE,,,,ILA WASOMI WETU WANAPASWA KUKUMBUKWA SANA,R.I.PCHACHAGE NA HAROUB WA IDS
 
bahat mbaya hata mawaziri wa hiyo wizara hawajui kua elim ni suala nyeti
 
Vijana hawawezi kuwakumbuka maprofessor wanabifu nao kwa kuwa maprof hawatoi maksi za bure, umesahau yule aliyepost juzi akishangilia UDSM kugoma kuongeza mikataba ya maprofessor.

Inaonekana akitokea mdau awaambie waache shule awalipe milioni kila mwezi wataacha hawa,kwa kuwa wana ndoto za kupata maisha bora kwa shotkat... Kuna usomi tena hapo?
 
Inaonekana akitokea mdau awaambie waache shule awalipe milioni kila mwezi wataacha hawa,kwa kuwa wana ndoto za kupata maisha bora kwa shotkat... Kuna usomi tena hapo?

Tunatakiwa kuanzisha utaratibu wa matokeo ya vyuo vikuu kuwekwa kwenye magazeti kama ya sekondari ili tujue japo viwango vyao vya ufauru.
 
Tunatakiwa kuanzisha utaratibu wa matokeo ya vyuo vikuu kuwekwa kwenye magazeti kama ya sekondari ili tujue japo viwango vyao vya ufauru.

Matokeo wakati mwingine sio ishu sana wala nini, maana huku wanafaulu tu. Mimi nataka wasomi wawe na uwezo wa kufikiria kwa niaba ya jamii yao...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…