Mosses Mashili
Member
- Jun 21, 2013
- 47
- 29
Amani iwe kwenu,
Wana jf leo nikiwa kanisa katoliki lilipo huku njiro katika misa ya kwanza tumetangaziwa kwamba wasomi wa kanisa katoliki wameipitia na kuichambua kwa umakini rasimu ya kwanza ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kutoa mapendekezo kadhaa. Tangazo hilo lilo elezewa kwa ufasaha na padri aliyeongoza misa hiyo lina wataka waumini wa parokia hii kushiriki kikamilifu katika maoni ya kuwasilishwa kwa tume ya mzee Warioba.
Katika utaratibu ambao kanisa limejipangia ni kwamba viongozi wa jumuiya tofauti watachukua maoni hayo ya wasomi wa kanisa katoliki na kuwapelekea waumini katika jumuiya zao, katika jumuiya hizo waumini watatakiwa kuyasoma na kutoa maoni yao mengine kisha yatakusanywa na kurudishwa parokiani, mwisho wa kuwasilishwa kwa maoni hayo ya jumuiya yatakua ni tarehe 10/7/2013.
Kila parokia itayachambua maoni hayo na kuyawasilisha jimboni, jimboni nako wataalamu watakaa na kuyachambua kisha kuyawasilisha taifani mwisho wa kuwasilisha maoni hayo taifani itakuwa tarehe 10/8/2013. Kwa sababu na mie na mwanajumuiya nitajitahidi kuwapa yale yaliyopo katika maoni hayo ya wasomi hawa wa kanisa katoliki, lakini kwa wana jf naomba tutembelee website ya TEC ili kuipata ishu hii kwa uzuri zaidi.
Kanisa katoliki limefikia hatua hii wakati chama kikuu cha upinzani CHADEMA kikiwa bado hakija onyesha msimamo wao kama chama kuhusu rasimu hiyo ya katiba licha ya kwamba viongozi wake wakuu kadhaa kwa nyakati tofauti wakionyeshwa kuridhishwa na baadhi ya mambo mfano uwepo wa serikali tatu huku mh. Mbowe akisema hawajakubaliana na baadhi mambo kabisa na watayapinga kwa nguvu zote, ccm wenyewe bado wanakusanya maoni ya wanachama wao kupitia mabaraza yatakayo undwa na chama chao na bado hatujajua nini msimamo wa cuf na vyama vingine vya siasa mfu ukiondoa nccr- mageuzi yenye uhai wa kiasi. Natoa wito kwa wakatoliki wote kushiriki katika mchakato huu ambao unatengeneza mustakabali wa nchi yetu.
My take;
Kesi wanazo bambikiziwa Chadema na serikali zinalenga kutuondolea utulivu chadema katika ushiriki wao katika mchakato huu muhimu kwa nchi yetu hasa ikizingatiwa kwamba wanasheria wa chadema wako bize kushugurikia kesi za makamanda wetu. MUNGU IBARiKI TANZANIA na kutuondolea hili jinamizi liitwalo ccm na viongoze wake.