Samiaagain2025
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 4,834
- 5,310
- Thread starter
- #21
Huwezi kuelewa,maana hujayajua maisha halisi ya watanzania wengi.Mkuu ina maana wote waliojiajiri hawakusoma kwa kutumia hiyo mitaala, mitaala ni kama nyenzo tu kujiajiri ni uthubutu wa mtu, duniani kote hakuna nchi ambayo haina tatizo la ajira hata hao wenye mitaala unayofikiria wewe, kujiajiri siolazima ufuate kozi uliyosomea, huyo atakuwa sio msomi,msomi yeyote lazima atumia akili na maarifa yake kufikiria nje ya box, sababu naamini msomi ni msomi tu hata kama anashinda akivuta bangi , tatizo la wasomi wa Tanzania wanatakiwa waletewe kila kwetu kwenye hotpot mezani wao wapakue tu. Tanzania pana fursa nyingi sana sio lazima mtu akuajiri, kama wasomi mnaweza kuunda vikundi, mkaandika mpango biashara/kazi na mkapata mikopo au mkajichangisha vijisenti kidogo mkaanza kufanya shughuli zenu,tumeona baadhi ya vijana waliosomea kwa mfano uhasibu wakianzisha kampuni za uhasibu na ukaguzi na wanaendelea vizuri ,wao wameona kuna pengo kati ya wafanyabiashara na mambo ya kodi au ukaguzi wa vitabu kutokana na sheria kwamba kwa biashara yoyote lazima uwe na vitabu vya mahesabu ndio ukadiriwe TRA au upate tenda kwenye mashirika, waliosomea uganga au maabara wanaweza kuanzisha maabara zao za uchunguzi wa magonjwa na kutokona na hali ya aisha siku hizi watu wa maabara wanapiga pesa ndefukutokana na kazi zao. Tatizo tunataka serikali iwe mwaajiri wakati ni jambo lisilowezekana na kujiajiri serikali imeweka mazingira bora ya kila mtu afanye kazi,imetengeza miundo mbinu, imerahisisha usajiri wa kampuni na hata sasa inafanya maboresho kwenye mambo ya ukusanyaji mapato hivyo ndio serikali inasaidia.Fanyeni kazi ,ajira zisizo rasmi zipo nyingi ,lima hata bustani utapata pesa, nendeni nje mkabebe box sio mnakaa tu ,wenzetu Wakenya wana uthubutu wa kutoka nje na kujiamini kwenda kutafuta au kufanya kazi, hiyo ni njia nyingine ya ajira.
Mfano,mtaji wa kujiajiri unapatikana wapi?
Hata hao serikali wenyewe huwa hawasemi mtaji unapopatikana.