ASCUDA T
Senior Member
- Sep 10, 2013
- 120
- 33
Ndugu wasomi wa nchi hii embu tutafakari leo na kushirikishana kuhusu suala la nchi yetu kujiingiza katika vita mbalimbali. Je bajeti ya nchi yetu inatosha mpaka kupeleka majeshi katka kila nchi amani inapotoweka? Tazama uchumi wetu unasuasua sasa je tunafanya haya kwa faida? Ushauri kwa taifa langu vita ianpotoke kwa wenzetu iwe fursa kwa kuuza chakula na kujifunza mapungufu ya wenzetu. Kwani wakati mwingine tunaweza kuona tunatenda wema bali tunaongeza maadui. Navyoelewa ukiitaka kuishi kwa amani duniani inabidi kupunguza mafungamano. Kwa xasa taifa limeshindwa kuwapa fedha wanafunzi kusoma elimu ya juu lakini inapesa za kupeleka wanajeshi kongo poleni wema usizidi uwezo. Nafikiri katiaba mpya iangalie suala la kupunguza mamlaka ya rais maana sidhani kama tunafaidika kwenda kongo. Hosptals hazina dawa, wagonjwa wanalala wawili kitanda kimoja, shule hazina maabara walimu hawatosho,bado watoto wanakalia ndoo za maji darasani, akinamama wanasafiri umbali mrefu kwenda hospita kujifungua wengine hufia njiani.