Wasomi shikilieni ndoto zenu...

Wasomi shikilieni ndoto zenu...

Alola

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
476
Reaction score
299
Tanzania ina vijana wengi ambao mpaka wanamaliza kidato cha 4/6 hawajui watakuja/wanapenda kuwa wataalam wa fani gani. Hii ni changamoto kubwa sana katika nchi yetu. Moja ya sababu ni kuhofia kiwango cha ufaulu kama kitatosha kusomea taaluma fulani. Na pia hutokea mtu anapenda taaluma fulani, na anapata daraja la kwanza katika mtihani wa NECTA, n.k ila hapo hapo pointi alizonazo zaweza kumnyima nafasi ya kusomea ule utaalam ulio katika ndoto zake(mwaka 2005 UDSM ilichukua divisheni 1.3 mpaka 1.4 kusomea Telecom Engineering, vijana wengi waliopata 1.5 waliitwa mwaka ujao yaani 2006). Kwahiyo vijana wengi huenda kusoma taaluma fulani sababu ndio wastani/pointi alizopata zinakubalika. Ushauri wangu ni kwamba hata ukienda kusomea taaluma nyingine, usisahau kurejea malengo ya kutafuta namna za kujiendeleza katika kile ulichokipenda mahali popote pale. Mtihani wa NECTA au NACTE usiwe ndio mhimili wa malengo yako. Wengi wetu hatuwezi kuhairisha masomo kama walivyo fanya baadhi ya wataalam kama(Steve Jobs, Mark Zuckeberg, etc) sababu ya umasikini na kutegemewa,n.k lakini kusoma taaluma nyingine haizuii wewe kuja kuwa mtaalam wa jambo fulani ambako ndio ndoto zako zimeegemea.
 
Back
Top Bottom