Wasomi tunaomba ufafanuzi kwenye hili

Unaanzaje na solution bila maswali? Hata research procedure lazima ianze na research questions halafu research hypothesis mwishoni huko kwenye conclusion ndio unapata solutions sasa hao wasomi wako wanafanyaje?
Umemjibu vizuri sana, na ndiyo nilicho mjibu, sasa yeye ni msomi kundi lipi

Super hero daddy
 
Kwan usomi wako ulisoma ili ufanye nini?
Lakini kaka wasomi walishausoma mchezo na kushauri kuliacha soko huria lifanye kazi yake..akiwemo huyu tusiye mpenda CCM Mh. Zitto Kabwe. Lakini Msomi mkuu alisisitiza bei ni ndogo Serikali itazinunua. Akatokea Msomi wa Physical Education Mh. PM Majaliwa akatangaza kabla ya masaa yaliyotolewa na Rais kuwa amejitokeza mnunuzi kutoka China annunua..akajibiwa Mh. Rais Msomi Mkuu kuwa wamechelewa na tutanunua wenyewe.. Nadhani wasomi walijitahidi sana tumefikia hapa. Labda ushauri kama wosomi wasiosoma kama sisi tusubirie mwakani msimu mpya tutumie soko huria kuipatia fedha za kigeni nchi yetu. Kwa sasa tuzigawe kwa wabanguaji wadogo wabangue na kutuuzia mtaani baada ya kupata kile kitambulisho cha machinga. Asante sanaYehodaya.
 
Tofauti ya wasomi wa nchi zilizoendelea na zisizoendelea ni moja wasomi wa nchi zilizoendelea na tajiri hujikita kwenye solution wakati wasomi wa nchi zisizoendelea hujikita kwenye maswali.
Kwa sababu solution watoazo zinafanyiwa na hapa zinabezwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We si ndiyo umesema wasiulize maswali watoe solution...mbona unajichanganya mwenyewe?
Nimekulia Denmark ambako nilizoea kuona wasomi wanatoa solution sio kuuliza maswali.
 
Naona chat inaonyesha comparisons ya commodities kwa miaka miwili yofauti.. Hapo nadhan downfall of korosho revenue imebe influenced by only factor korosho bado ipo gharani(Good on Transit). Na report imecgukua only sales recorded on cash book.(korosho iliyouzwa tayari)
Haziwezi fanana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basically it is ridiculous tunasoma mambo ya INTERNATIONAL BUSINESS, INTERNATIONAL MARKETING in our DEGREE COURSE lakini hatuvitumi, serikali ndiyo wameweka ugumu sana to exercise this system, sasa tunasoma ili kusaidia taifa letu na serikali yetu ama tunasoma ili kutoa ujinga kichwani

Super hero daddy
 
tumeona juzi hapa korosho ilivyokuwa inakusanywa na kurudishwa kwa wakulima kwamba eti imekosa ubora, haya ndiyo matokea yake

Super hero daddy
 
Good on transit ama wakulima walirudishiwa kwa kigezo hazina ubora?

Super hero daddy
 
Fafanua Chart hii. Sio kila swali lazima liwe na Question Mark! Wasomi wakweli wanajua kufafanua na kutoa maelezo ambayo 'a lay person' anaweza kupata kuelewa chart ina maana gani katika maisha yake. Hata kwenye mtihani wa darasa la nne kuna maswali kama: "fafanua msemo huu."
Unaanzaje na solution bila maswali? Hata research procedure lazima ianze na research questions halafu research hypothesis mwishoni huko kwenye conclusion ndio unapata solutions sasa hao wasomi wako wanafanyaje?
 
Mfano hesabu Kama hiI 3+X=5 tafuta X ukimuuliza msomi Kwa nini umeweka hiyo X namba isiyojulikana niitafute? Atakujibu kisomi kuwa maisha yako yote una Kazi ya kutafuta X ni nini ili ufanikiwe. Ukiwa maskini unakuwa bado hujajua X ni nini ili uwe tajiri
 
Tofauti ya wasomi wa nchi zilizoendelea na zisizoendelea ni moja wasomi wa nchi zilizoendelea na tajiri hujikita kwenye solution wakati wasomi wa nchi zisizoendelea hujikita kwenye maswali.
Kwanza kabisa nakushukuru kwa kuleta hoja hii ya tofauti ya wasomi wa nchi zilizoendelea na wasomi wa nchi ulizoziita ZISIZOENDELEA.. mwingine angesema nchi ZINAZOENDELEA.

Pili, siyo kweli kwamba tofauti ya wasomi nchi zilizoendelea na wale wa nchi ZISIZONDELEA ni moja. tofauti ziko nyingi sana. Na pia hiyo uliyosema SIYO KWELI, UKWELI NI KWAMBA WASOMI WA NCHI ZILIZOENDELEA WANA MASWALI MENGI SANA. WASOMI WA NCHI ZISIZOENDELEA HAWARUHUSIWI KUULIZA MASWALI BALI WANATAKIWA KUTOA UFUMBUZI TU BILA KUULIZA MASWALI, BILA KUFANYA UTAFITI. KWA KIFUPI WANATUMIA USHIRIKINA BADALA YA USOMI WAO.

Hebu tuangalie tofauti chache:
Tofauti ya kwanza ni katika umahiri wao. Ni wazi wasomi wa nchi zilizoendelea wanapita kwenye mifumo ya elimu ambayo uwekezaji wake ni mkubwa zaidi. NA NDIO MAANA WAMEENDELEA ATI. Siri ya maendeleo ya kwanza kabisa ni ELIMU BORA. Hapa Tanzania hatuna ELIMU BORA, na wala serikali ya CCM haitaki kabisa hicho kitu. kwa aina ya utawala wa serikali ya CCM, inahitaji watu wawe mbumbumbu. kwa hiyo tunacho kitu kinaitwa ELIMU BURE, ambayo kwa kweli ni kufundisha vijana wetu USHIRIKINA. USHIRIKINA ni pamoja na kununua ndege ili kuwezesha shirika la Ndege, bila kwanza kufanya utafiti, BILA KUULIZA MASWALI huko nyuma ilikuwaje, tuko wapi, tunataka kwenda wapi. USHIRIKINA pia ni kustaafisha wasomi wetu mapema ili hela zinazopatikana zikajenge barabara, badala ya kuwatumia KUULIZA MASWALI na kufanya TAFITI na kubainisha vipaumbele vya taifa letu, kujua tuanze na kipi na tuanze na mambo mangapi.

Tofauti ya pili ni kwamba wenzetu mtu ana SPECIALISE katika eneo fulani mapema. sisi tunabebesha watoto wetu mabegi makubwa na kuwashindilia masomo mengi sana ili KUWACONFUSE waone kwamba ELIMU BORA HAIWEZEKANI ili wawe WASHIRIKINA NA WACHAWI kwa urahisi. Matokeo yake wahitimu wetu hawana UBOBEZI wa kutosha. Mwalimu wa sayansi badala ya kujikita katika somo moja tu unakuta analazimishwa mawili, nk.

Nadhani hizo mbili zinatosha kwa sasa. karibu tujadili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…