Wasomi tunaomba ufafanuzi kwenye hili

Wasomi tunaomba ufafanuzi kwenye hili

Kwanza kabisa nakushukuru kwa kuleta hoja hii ya tofauti ya wasomi wa nchi zilizoendelea na wasomi wa nchi ulizoziita ZISIZOENDELEA.. mwingine angesema nchi ZINAZOENDELEA.

Pili, siyo kweli kwamba tofauti ya wasomi nchi zilizoendelea na wale wa nchi ZISIZONDELEA ni moja. tofauti ziko nyingi sana. Na pia hiyo uliyosema SIYO KWELI, UKWELI NI KWAMBA WASOMI WA NCHI ZILIZOENDELEA WANA MASWALI MENGI SANA. WASOMI WA NCHI ZISIZOENDELEA HAWARUHUSIWI KUULIZA MASWALI BALI WANATAKIWA KUTOA UFUMBUZI TU BILA KUULIZA MASWALI, BILA KUFANYA UTAFITI. KWA KIFUPI WANATUMIA USHIRIKINA BADALA YA USOMI WAO.

Hebu tuangalie tofauti chache:
Tofauti ya kwanza ni katika umahiri wao. Ni wazi wasomi wa nchi zilizoendelea wanapita kwenye mifumo ya elimu ambayo uwekezaji wake ni mkubwa zaidi. NA NDIO MAANA WAMEENDELEA ATI. Siri ya maendeleo ya kwanza kabisa ni ELIMU BORA. Hapa Tanzania hatuna ELIMU BORA, na wala serikali ya CCM haitaki kabisa hicho kitu. kwa aina ya utawala wa serikali ya CCM, inahitaji watu wawe mbumbumbu. kwa hiyo tunacho kitu kinaitwa ELIMU BURE, ambayo kwa kweli ni kufundisha vijana wetu USHIRIKINA. USHIRIKINA ni pamoja na kununua ndege ili kuwezesha shirika la Ndege, bila kwanza kufanya utafiti, BILA KUULIZA MASWALI huko nyuma ilikuwaje, tuko wapi, tunataka kwenda wapi. USHIRIKINA pia ni kustaafisha wasomi wetu mapema ili hela zinazopatikana zikajenge barabara, badala ya kuwatumia KUULIZA MASWALI na kufanya TAFITI na kubainisha vipaumbele vya taifa letu, kujua tuanze na kipi na tuanze na mambo mangapi.

Tofauti ya pili ni kwamba wenzetu mtu ana SPECIALISE katika eneo fulani mapema. sisi tunabebesha watoto wetu mabegi makubwa na kuwashindilia masomo mengi sana ili KUWACONFUSE waone kwamba ELIMU BORA HAIWEZEKANI ili wawe WASHIRIKINA NA WACHAWI kwa urahisi. Matokeo yake wahitimu wetu hawana UBOBEZI wa kutosha. Mwalimu wa sayansi badala ya kujikita katika somo moja tu unakuta analazimishwa mawili, nk.

Nadhani hizo mbili zinatosha kwa sasa. karibu tujadili
Duh! Aiseeee !!
 
Mkuu hizo histogram zinakuwa kwa kwenda chini. Hawa BOT na TRA ni wasaliti. Hizo histogram zao kwanza hazijathibitishwa na NBS. Washtakiwe kwa uhujumu uchumi na kukosa uzalendo kwa Jamhuri yetu
Naunga mkono hoja
 
Unaanzaje na solution bila maswali? Hata research procedure lazima ianze na research questions halafu research hypothesis mwishoni huko kwenye conclusion ndio unapata solutions sasa hao wasomi wako wanafanyaje?

utapataje solution bila maswali.kwanza kunakuwa na tatizo na tatizo linazaa swali au maswali na hayo maswali yanatafutiwa majibu na majibu ndo solution/s
 
Hahaha Alphayo Kidata yuko wapi?! Kama ni fisadi mbona hashitakiwi?! Toka TRA mpaka Ikulu mpaka ubalozi Canada, na alivyo toka Canada sijui meli aliyopanda ilipitea au ndege aliyopanda haijafika?!
Mkulu aligundua walimpikia data, alizitafuta pesa hakuziona, akamuita aliyepika naye hazioni, msala ukaanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Embu elezea vizuri hapa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofauti ya wasomi wa nchi zilizoendelea na zisizoendelea ni moja wasomi wa nchi zilizoendelea na tajiri hujikita kwenye solution wakati wasomi wa nchi zisizoendelea hujikita kwenye maswali.
Kwa hiyo? Wewe ni msomi au mjinga?
 
Unaanzaje na solution bila maswali? Hata research procedure lazima ianze na research questions halafu research hypothesis mwishoni huko kwenye conclusion ndio unapata solutions sasa hao wasomi wako wanafanyaje?
umemjibu kisomi
 
Back
Top Bottom