LICHADI
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 4,491
- 12,560
Ni muda muafaka sasa tujadili hizi taasisi zinatusaidia nini kama Taifa maana kila kukicha bei za vyakula ni juu hasa mafuta ya kupikia na Ngano, serikali inaingia garama kubwa kuwalipa mishahara minono waprofesa na wataalam wengine wa kilimo katika hizi taasisi lakini sijui wanamchango gani kwa Taifa hawa.
Mpaka sasa Mafuta ya kula tunaagiza Nnje ya nchi kitu ambacho kimefanya matuta yamepanda sio mchezo kile kipimo kidogo cha sh 200 kwa sasa ni 700 hadi 800, ndoo ya lita 20 kwa sasa ni 110,000 hadi 120,000
Na bado tunajivunia tuna Chuo cha wataalam kilimo na tuna wasomi wa kilimo sasa hawa watu wanalisaidiaje Taifa wakati vitu muhim kama mafuta ya kula tunaagiza nnje wakati tuna Ardhi ya kutosha kulima mawese na na mimea mingine ambayo itatuletea mafuta ya kututosheleza bila kuagiza nnje
Ngano imetoka 1200 kwa sasa ni 2000, sababu tunaagiza nnje na huko nnje vita ya urusi na Ukraine ni sababu moja wapo maana inasemekana wanazalisha ngano kwa kiasi kikubwa kwa sasa hawauzi popote kwasababu ya vita na vikwazo alivyowekewa Urusi
Ukiingia mtaani chapati na vitu vingine bie ni juu sababu mafuta na ngano vimepanda kwa kasi ya ajabu,yote hayo ni kwa sababu vitu vya muhim kama hivi tunaagiza nnje hatuzalishi sisi wenyewe kwa kiwango kikubwa na kututosheleza wakati uwezo tunao
Hivi wasomi wetu wa sua kwa Ardhi tuliyonayo hatuwezi kulima ngano ikatutosha bila kuagiza nnje? Tatizo ni nyie au ni Serikali haitoi bajeti kubwa kwenu
Sua mnalisaidia nini Taifa kama bado tunaagiza vitu muhim nnje na nyie wataalam wa kilimo mpo?