Wasomi wafanye utafiti wa madhara ya kutopandishwa mishahara kwa wafanyakazi, lobbyist wanaweza kutusaidia

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ili mfanya kazi afanye kazi inayoleta matunda anahitaji kula vizuri, kuwa na afya njema, alale vizuri na pia afya yake ya akili iwe njema. Kwa wengi laki tatu mshahara wa kima echo chini tunafahamu una changamoto hasa kuishi mijini ambako unalipia kodi ya nyumba, unahitaji usafiri wa kukufikisha kazini na unahitaji kununua maji kila siku ndoo 200.

Watafuti wanaweza kufanya utafiti wa mortality rates, age groups na magonjwa makuu yanasobabisha vifo. Tafiti zifanyiwe ulinganisho na nchi ambazo walikua na matatizo hayo na jinsi wakivyopambana kuya ondoa.

Inawezekana ufahamu wa kupoteza nguvu kazi kwa matatizo yanayoweza kuzuilika unaweza kuwashtua watawala wetu. Tatizo kubwa tulilo nalo pia ni kuwa wasomi wengi ni wanasiasa kwanza kabla ya kuwa wana taaluma.
 
Wasomi ndio wadudu gani?
Sidhani hata kama kuna taasisi zinazofanya hiyo shughuli unayotaka ifanyike
 
Kitengo cha Uchumi katika Vyuo Vikuu vinaweza kulifanya hili.
 
Usiwe na wasiwasi kuna wataalamu lukuki, watafanya upembuzi yakinifu.

Usikute hata hao watumishi hawataki nyongeza ya mshahara, wao wanataka tuendelee na kasi ya kuutangaza utalii🐒

20220502_071339.jpg
 
Madhara yapo mengi.ikiwemo na go slow strikes.productivity inapungua na malengo kutofikiwa
 
Wakati mwingine unajiuliza hizi njoo kesho zisizoisha ofisi za serikali zinasababishwa na nini, na zitaisha lini,? Kamwe hazitaisha, rushwa na wizi ndio vitashamiri, CAG na ripoti zake ni burudani kwa rais na wanasiasa wenzie.
 
Ili mfanya kazi afanye kazi inayoleta matunda anahitaji kula vizuri, kuwa na afya njema, alale vizuri na pia afya yake ya akili iwe njema. Kwa wengi laki tatu mshahara wa kima echo chini tunafahamu una changamoto hasa kuishi mijini ambako unalipia kodi ya nyumba, unahitaji usafiri wa kukufikisha kazini na unahitaji kununua maji kila siku ndoo 200.

Watafuti wanaweza kufanya utafiti wa mortality rates, age groups na magonjwa makuu yanasobabisha vifo. Tafiti zifanyiwe ulinganisho na nchi ambazo walikua na matatizo hayo na jinsi wakivyopambana kuya ondoa.

Inawezekana ufahamu wa kupoteza nguvu kazi kwa matatizo yanayoweza kuzuilika unaweza kuwashtua watawala wetu. Tatizo kubwa tulilo nalo pia ni kuwa wasomi wengi ni wanasiasa kwanza kabla ya kuwa wana taaluma.
Matokeo ya tafiti hizo yaainishe kwa kina athari hasi zitokanazo na vipato vidogo vya mishahara. Mbali ya athari za kiuchumi na kijamii kwa wafanyakazi, lipo tatizo lingine kubwa la kisaikolijia.
 
Mshahara usipolingana na kupanda kwa gharama za maisha maana yake unakula unachomudu kukipata. Watoto watapata utapia mlo na madhara yake makubwa ni kwa kizazi kijacho.
 
Kitengo cha Uchumi katika Vyuo Vikuu vinaweza kulifanya hili.
Fedha za kufanya huo utafiti watazitoa wapi?
Serikali haiwezi kuwa na mambo yakibabaishaji namna hii inaelewa kila kitu ina data zoteee.

Maisha yamekuwa juu na hakuna mfanyakazi aliyeongezwa mshahara je ikiongezwa si tutakimbiana wabaki wafanya biashara tu wakoi-survive
 
Kitengo cha Uchumi katika Vyuo Vikuu vinaweza kulifanya hili.
Tatizo kubwa la wasomi wetu hawapo kwa ajili ya kutetea Taifa na watu wake

msomi wa kitanzania anawaza asome , apate kazi nzuri ili alipwe mshahara mkubwa + ale kwa urefu wa kamba yake

atembelee gari nzuri , nyumba nzuri na asomeshe watoto zake bas

ila ule uzalendo hawana

hoja yako ni nzuri sana dada sky eclat sema tatizo ndio hilo tanzania hatuna raslimali wasomi
 
Kutoongezewa mishahara watumishi anaeumia ni mwananchi na mtumishi ni bilabila
 
Back
Top Bottom