Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,258
Rasimu ya pili ya Katiba imetoka hivi karibuni ikipendekeza Muungano wa Serikali tatu Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Tanganyika.
Mjadala wake umeanza, ambapo wasomi wameanza kwa kukosoa takwimu za Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu idadi ya waliotoa maoni, kuwa zimetumika kuupotosha umma, kama wanavyosema wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sabato Nyamsenda na Bashiru Ally wakati wakizungumza katika kipindi cha Je, Tutafika? kinachorushwa na Channel Ten.
Nyamsenda anasema ukweli wa takwimu hizo uko kwenye ripoti ya Tume hiyo, ambayo haipatikani kwa urahisi huku watu wakiishia tu kusoma tu rasimu ambayo haielezi majukumu waliyopewa, mahali walipopita, idadi ya wananchi na maoni yao.
Takwimu za Tume
Akifafanua zaidi, Nyamsenda anasema takwimu zinazotajwa kwamba asilimia 61 ya Watanzania Bara wanataka Serikali tatu, asilimia 60 ya Wazanzibari wanataka Serikali ya Mkataba si za kweli.
Tume ya Warioba imetoa takwimu kuwa, watu waliotoa maoni kwa jumla ni 333,537. Kati yao, waliogusia Muungano ni 77,000, kwa hiyo 256,537 hawakugusia Muungano, anasema na kuongeza:
Ukiwagawanya katika Bara utakuta ni watu wapatao 36,000 na Visiwani watu 38,000. Kati ya waliozungumzia muungano. Kwa Zanzibar watu 19,000 hawakugusia muundo na watu 10,400 ndiyo waligusia Muungano wa Mkataba.
Anaendelea kufafanua: Waliozungumzia Serikali mbili ni 6,460 sawa na asilimia 34. Kwa hiyo ni wachache kuliko waliozungumzia Serikali ya Mkataba ambao nao ni wachache kuliko wale ambao hawakugusia kabisa suala la muungano. Ni sawa na tone la maji katika bahari, anasema.
Anaendelea kufafanua kuwa waliotoa maoni kuhusu Serikali ya Mkataba na Serikali tatu, ni wachache huku wengi wakiwa Bara.
Kama jumla ya watu waliotoa maoni ya Katiba ni 333,537, huwezi ukachukua watu 16,000 waliotaka Serikali tatu ukawaziba wengi ambao hawakutaka, anasema na kuongeza:
Ukijumlisha watu wanaotaka Serikali moja na mbili ambao ni 16,475, utaona ni wengi kuliko wanaotaka Serikali tatu ambao ni 16,470.
Anasema watu hao wakiwekwa katika kundi ambalo halikugusia kabisa muundo wa muungano, ni watu 287,537 sawa na asilimia 86.
Wasomi wanavyokosoa mahesabu ya Serikali tatu - Makala - mwananchi.co.tzMjadala wake umeanza, ambapo wasomi wameanza kwa kukosoa takwimu za Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu idadi ya waliotoa maoni, kuwa zimetumika kuupotosha umma, kama wanavyosema wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sabato Nyamsenda na Bashiru Ally wakati wakizungumza katika kipindi cha Je, Tutafika? kinachorushwa na Channel Ten.