Wasomi wanavyokosoa mahesabu ya Serikali tatu

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Rasimu ya pili ya Katiba imetoka hivi karibuni ikipendekeza Muungano wa Serikali tatu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Tanganyika.

Mjadala wake umeanza, ambapo wasomi wameanza kwa kukosoa takwimu za Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu idadi ya waliotoa maoni, kuwa zimetumika kuupotosha umma, kama wanavyosema wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sabato Nyamsenda na Bashiru Ally wakati wakizungumza katika kipindi cha Je, Tutafika? kinachorushwa na Channel Ten.

Nyamsenda anasema ukweli wa takwimu hizo uko kwenye ripoti ya Tume hiyo, ambayo haipatikani kwa urahisi huku watu wakiishia tu kusoma tu rasimu ambayo haielezi majukumu waliyopewa, mahali walipopita, idadi ya wananchi na maoni yao.

Takwimu za Tume

Akifafanua zaidi, Nyamsenda anasema takwimu zinazotajwa kwamba asilimia 61 ya Watanzania Bara wanataka Serikali tatu, asilimia 60 ya Wazanzibari wanataka Serikali ya Mkataba si za kweli.

“Tume ya Warioba imetoa takwimu kuwa, watu waliotoa maoni kwa jumla ni 333,537. Kati yao, waliogusia Muungano ni 77,000, kwa hiyo 256,537 hawakugusia Muungano,” anasema na kuongeza:

“Ukiwagawanya katika Bara utakuta ni watu wapatao 36,000 na Visiwani watu 38,000. Kati ya waliozungumzia muungano. Kwa Zanzibar watu 19,000 hawakugusia muundo na watu 10,400 ndiyo waligusia Muungano wa Mkataba.”

Anaendelea kufafanua: “Waliozungumzia Serikali mbili ni 6,460 sawa na asilimia 34. Kwa hiyo ni wachache kuliko waliozungumzia Serikali ya Mkataba ambao nao ni wachache kuliko wale ambao hawakugusia kabisa suala la muungano. Ni sawa na tone la maji katika bahari,” anasema.

Anaendelea kufafanua kuwa waliotoa maoni kuhusu Serikali ya Mkataba na Serikali tatu, ni wachache huku wengi wakiwa Bara.

“Kama jumla ya watu waliotoa maoni ya Katiba ni 333,537, huwezi ukachukua watu 16,000 waliotaka Serikali tatu ukawaziba wengi ambao hawakutaka,” anasema na kuongeza:

“Ukijumlisha watu wanaotaka Serikali moja na mbili ambao ni 16,475, utaona ni wengi kuliko wanaotaka Serikali tatu ambao ni 16,470.”

Anasema watu hao wakiwekwa katika kundi ambalo halikugusia kabisa muundo wa muungano, ni watu 287,537 sawa na asilimia 86.

Wasomi wanavyokosoa mahesabu ya Serikali tatu - Makala - mwananchi.co.tz
 
Je hawa wametoa wapi hizi takwimu, ningeomba kama kuna mjumbe wa tume humu atusaidie kutufafanulia katika hili
 
Hii ilishawahi kutokea miaka ya 90 , CCM wakiwa wameshajiandaa kuanzisha vyama feki kutii shinikizo la wafadhili wakageuza matokeo ya kura za maoni ya uanzishwaji wa vyama vingi.
Hili la sasa sijui lina mkono wa nani, labda zenji?
 
WARIOBA

"Mheshimiwa Rais ; sheria ya madiliko ya katiba ilieleza kwamba tume itaongozwa na misingi mikuu ya taifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha mambo kadhaa
Moja kati ya mambo hayo no uwepo wa jamhuri ya muungano .kwahiyo tume ilianza kazi kwa madhumuni ya kuboresha muungano .

Mheshimiwa Rais wananchi wengi walitia maoni yao lakini wengi wao walijikita kwenye muundo wake .
Kwa Tanzania bara wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni kuhusu muungano kati yao watu 27,000 walizungumzia muundo.
Kwa Zanzibar wananchi karibu wote walizungumzia kuhusu muungano kati ya wananchi karibu 38,000 waliotoa maoni , wananchi 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wa muungano .
Kwa takwimu hizi zinaonesha upande wa Tanzania bara 13% walitaka serikali moja ,24% walipenda serikali mbili , na 61% walilitaka serikali tatu .
Kwa upande was Zanzibar 34% walitaka serikali mbili ,60% walitaka muungano wa mkataba , na 0.1% (watu 25) walitaka serikali moja .
Aidha taasisi nyingi kama vile vyama vya siasa ,asasi za kiraia name jumuiya za kidini zilitaka serikali tatu"

Ni kieneo kidogo turn hiko kupinga twakwimu za huyo msomi

Nauliza huyo nyamaenda yeye ndio amekusanya maoni ama warioba
 
WARIOBA

"Mheshimiwa Rais ; sheria ya madiliko ya katiba ilieleza kwamba time itaongozwa na misingi mikuu ya taifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha mambo kadhaa
Moja kati ya mambo hayo no uwepo wa jamhuri ya muungano .kwahiyo tume ilianza kazi kwa madhumuni ya kuboresha muungano .

Mheshimiwa Rais wananchi wengi walitia maoni yao lakini wengi wao walijikita kwenye muundo wake .
Kwa Tanzania bara wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni kuhusu muungano kati yao watu 27,000 walizungumzia muundo.
Kwa Zanzibar wananchi karibu wote walizungumzia kuhusu muungano kati ya wananchi karibu 38,000 waliotoa maoni , wananchi 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wa muungano .
Kwa takwimu hizi zinaonesha upande wa Tanzania bara 13% walitaka serikali moja ,24% walipenda serikali mbili , na 61% walilitaka serikali tatu .
Kwa upande was Zanzibar 34% walitaka serikali mbili ,60% walitaka muungano wa mkataba , na 0.1% (watu 25) walitaka serikali moja .
Aidha taasisi nyingi kama vile vyama vya siasa ,asasi za kiraia name jumuiya za kidini zilitaka serikali tatu"

Ni kieneo kidogo turn hiko kupinga twakwimu za huyo msomi

Nauliza huyo nyamaenda yeye ndio amekusanya maoni ama warioba

Kile kipindi kimepoteza credibility kwa kualika wazungumzaji wote kutoka uvccm. Hapakuwa na hadidu kwamba kila anayetoa maoni aseme kama anataka muundo gani wa muungano. Ni ujinga kusema kwa kuwa asilimia 80 hawajagusia chochote kuhusu muungano basi wanataka serikali mbili,umejuaje au kwa sababu mwendesha kipindi ni mjumbe wa umoja wa wazazi ccm
. Mimi hapa sikugusia muundo wa muungano lakini nataka serikali moja ambayo si gharama kama 2 za ccm. Wasomi madesa wanapotosha wananchi, warioba yupo sahihi
 
asante sana Baba Ruu
WARIOBA

"Mheshimiwa Rais ; sheria ya madiliko ya katiba ilieleza kwamba tume itaongozwa na misingi mikuu ya taifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha mambo kadhaa
Moja kati ya mambo hayo no uwepo wa jamhuri ya muungano .kwahiyo tume ilianza kazi kwa madhumuni ya kuboresha muungano .

Mheshimiwa Rais wananchi wengi walitia maoni yao lakini wengi wao walijikita kwenye muundo wake .
Kwa Tanzania bara wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni kuhusu muungano kati yao watu 27,000 walizungumzia muundo.
Kwa Zanzibar wananchi karibu wote walizungumzia kuhusu muungano kati ya wananchi karibu 38,000 waliotoa maoni , wananchi 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wa muungano .
Kwa takwimu hizi zinaonesha upande wa Tanzania bara 13% walitaka serikali moja ,24% walipenda serikali mbili , na 61% walilitaka serikali tatu .
Kwa upande was Zanzibar 34% walitaka serikali mbili ,60% walitaka muungano wa mkataba , na 0.1% (watu 25) walitaka serikali moja .
Aidha taasisi nyingi kama vile vyama vya siasa ,asasi za kiraia name jumuiya za kidini zilitaka serikali tatu"

Ni kieneo kidogo turn hiko kupinga twakwimu za huyo msomi

Nauliza huyo nyamaenda yeye ndio amekusanya maoni ama warioba
 
nilushangaa sana na waanidhishi wakakomali pointi ya huyu dogo
Kile kipindi kimepoteza credibility kwa kualika wazungumzaji wote kutoka uvccm. Hapakuwa na hadidu kwamba kila anayetoa maoni aseme kama anataka muundo gani wa muungano. Ni ujinga kusema kwa kuwa asilimia 80 hawajagusia chochote kuhusu muungano basi wanataka serikali mbili,umejuaje au kwa sababu mwendesha kipindi ni mjumbe wa umoja wa wazazi ccm
. Mimi hapa sikugusia muundo wa muungano lakini nataka serikali moja ambayo si gharama kama 2 za ccm. Wasomi madesa wanapotosha wananchi, warioba yupo sahihi
 
Wasomi wa kitanzania are very good at summerizing but not initiating. Kwa hiyo sishangai wasomi kusaisha maoni ya wenzao that critically wakati wao wenyewe hawana kitu cha kukitoa kilicho kipya bali copy and paste kama kawa. Warioba kaandika historia ambayo wasomi madesa hawataki kuona mafanikio hayo.
 
ukiona mtu anapinga Tanganyika kurudi ulingoni ujue huyo ana matatizo ya kifikra, Huyo hata kwao kijiji anakukataa kuwa sio kwao. Mbona Wazenj, wana serikali nasi tunataka serikali ya Tanganyika. Hata kama Muungano za Zenj na Tanganyika utakufa kwa sababu ya hiyo, let it die a natural death. Kwanza hata kama ukifa sisi Watanganyika hatutaathirika na kufa huo Muungano. Wazenj watakuja kwetu kununua mchele, unga wa mahindi, ng'ombe, umeme nk kwa passport na visa juu. But this will happen only if Wazenj wakiamua kuvunja Muungano uliopo

Tanganyika IRUDI ULINGONI MAKELELE YA SISI KUWAONEA WAZENJ YAISHE, TURUDISHE TANGANYIKA ILI TUHESHIMIANE
 
Katika takwimu,jaribio la idadi ya 1024 linatosha kuelezea maoni ya watu. Hivyo si kweli kuwa tume ilikosea kwenye mahesabu. Kwa maneno mengine tume ilifanya kazi ya ziada kuchukua maoni ya watu 77,000 kuhusu serikali. Na vilevile maoni ya watu 333,537 yasingebadilisha maoni ya watu 77,000 au 1024 kama maoni yalichukuliwa kwa njia sahihi. Asilimia ya maoni ingebaki palepale 60.
 
Tatizo la tume ya warioba waliingia tayari na mfumo wao wa muungano kwani kama kweli wangetaka maoni ya wananchi wangepeleka maoni yote kuhusu muundo wa muungano je wananchi wanataka muundo wa namna gani?
1.serikali moja
2.serikali mbili
3.serikali tatu
4.serikali nne
5.muungano wa mkataba
Na sio kutuaminisha kuwa wananchi wengi walitaka serikali tatu hayo ni mawazo yao binafsi ndio maana pamoja na kazi ya tume kuisha amebaki kutetea hoja ya serikali tatu wakati hiyo ni kazi ya bunge la katiba kuamua
Wachambuaji wamechambua kitakwimu nashangaa watu wengine mnapinga bila kutoa takwimu zenu
 
Haya mshaurini jk aitishe kura za maoni tuone kati ya ccm na watanzania nani atashinda...
 
Back
Top Bottom