Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Hawa wasomi njaa hawa kipindi kile cha nyuma walitusababishia ikawa ukienda kula ndizi choma na mishkaki unawekewa kavu na ukitaka chachandu unatakiwa ulipie.
Yaani Ghafla Chachandu ikawa dawa ya Corona. Kwa utafiti gani haijulikani. Yaani sisi watu wa hovyo sana.
Wauzaji chips wakawa sasa wanauza na chachandu kwa kijiko kimoja tsh 300 ukitaka 3 unalipa tsh 1000 wakati chachandu ilikuwa bure.
Wenye mtaji wakaanza tengeneza chachandu wanaweka kwenye chupa wanazipa jina flani zinauzwa tsh 15,000. Tumeona waziri na jopo lake akinywa kwa majidai kabisa. Alichunguza wapi?
Yule waziri mwingine akakumbuka jinsi ambavyo huwa akienda kwa mganga anafanywa, akaanzisha naye mambo yake ukawa wimbo wa Taifa. Yaani Tanzania ikawa ni kichwa cha mwendawazimu. Kila aliye kwenye nafasi alikuja na dhana yake na kuifanya kuwa ya Taifa.
Wasomi walikuwa wakishadadia au kunyamaza tu. Yaani kama mazezeta flani hivi.