Frumence M Kyauke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2021
- 630
- 1,262
Tatizo la tozo kuwa nyingi sio makusudi ya raisi wala serikali. Lawama hizi napeleka kwa wasomi wenye taaluma ya uchumi kwasababu wanatakiwa kubuni njia nyingine za mapato na kuwasilisha serikalini.
Mfano rahisi ni kuwa, badala ya Serikali kuongeza tozo katika miamala ya simu na benk ilipaswa wasomi wenye taaluma ya uchumi wakishirikiana na waziri wa viwanda na biashara ikiwemo uwekezaji kushawishi wawekezaji kutoka mataifa makubwa kuja kuwekeza hapa nchini kwa wingi ikwemo kujenga viwanda ili serikali ijipatie mapato mengi nadhani hii itasaidi tozo kupungua ama kuondolewa kabisa katika miamala ili wananchi wapate ahueni.