Wazo la kabwela
JF-Expert Member
- Feb 13, 2013
- 1,812
- 1,373
Maisha yalibadilika, wasomi (wetu) wakaanza kuziona thamani zao katika ombwe la utupu. Walishindwa kuthamini hata vyungu vilivyowapika wakajiona wameiva. Wengine waliamua kujiita wamepikwa matopeni. Lakini kubwa ni kwamba tuna falsafa. Itikadi ambazo zinafumbatwa katika lugha zetu. Pengine matopeni tutokako ni falsafa inayofumbatwa katika lugha.
Usomi ulituburuza na kutuingiza katika usasa. Tukaona kila kitu ni kipya. Tukafurahia uvumbuzi wao wa neno uhalisiajabu ( magic realism) na kuona tumeletewa dhana na mtindo mpya. Wengine waligundua hila za kujitukuza kwao lakini wenye akili zao wakasema: tuliwawahi kitambo katika fasihi nenwa yetu. Huo ni urejelezi tu.
Wakaendelea kutufanya tuone upya katika tathmini ya uzuri na ubaya wa falsafa yetu. Wakaleta ujumi mweusi. Eti wakadhani wanatuengua na miktadha ya uzuri na ubaya was falsafa yetu tuliyoifumbata toka nyakati zileeeeeee za mila desturi na tamaduni zetu. Hivi hawajui katika fumbato la istilahi hizo tunaweza rejelea falsafa zetu kwa jina la omorembe? Wamefanikiwa kucheza na akili zetu za kutofautisha vitu visivyotofautika Pengine ni uenguaji wa majambo kitaaluma) au ubinafsi wa kukumbatia maarifa?
Nimebaki naduwaa. Naendelea kuwaza ufutuhi, uramsa, utanzia nao umeleta upya? Pengine upya nikatika uga wa kitaaluma.
Lakini bado nasafiri. Natafuta majibu. Natamani mdahalo wa kifalsafa. Inshalaah! Wapo wanafalsafa wachanga watayavumbua haya.
Wataleta upya uliofumbatwa katika urazini wenye asili yetu na sio wa mwigo!