Wassira amgomea JPM, asema halipi deni la Commodity Import Support. Akataa wito, Task Force kutuma Polisi. Yeye adai yuko tayari kupigwa pingu!

Wassira amgomea JPM, asema halipi deni la Commodity Import Support. Akataa wito, Task Force kutuma Polisi. Yeye adai yuko tayari kupigwa pingu!

Wewe ni zero Brain kupindukia, tangu lini Rais akahusika na mikopo ya watu Benk?
Yeye ni Meneja wa Benk? Mikopo ina masharti yake, hakuna mkopo bila dhamana, hiyo ni kazi ya Bank na Mahakama, Rais anakujaje? Kuishi kote huko ulaya, kichwani uko mweupe hivyo
Tatizo lako unaparamiaga mambo bila kuelewa mantiki yake, naishia hapa
 
Unoko wa watu ya kanda ya ziwa, wana mahasira, uchoyo, Ubinafsi, visasi na kila kitu walicho kiona kuwa na manufaa, kama viranja wa namala, Nyakato sec. school, ile ya Bukoba vijijini.

Wasira usikubali wanakuonea gele kwa sababu ya upekee wa sura yako. njia nyeupe kugombea Urais utapamba bara la Africa kwa uzuri wa sura tofauti na hawa warembo wa sasa.

Warembo siku zote wana wivu sana.
 
Hao ndio wana siasa wa Tanzania. Wengi ni wezi kweli kweli wa mali ya umma. Ndio maana majungu na fitna yamekuwa msingi wao imara wa kuendelea kushiriki siasa. Hawana kipya cha kuongeza.
Wewe siyo mwizi? yaani hata kuibia tu drsn, upate marks za juu. unanyoosha vidole tu kwa wengine.

na kama hujawahi kuiba una majungu na mpaka sasa utakuwa maskini sana.
 
Huo wizi ni wizi wa mbolea kupeleka shambani ili uvune mazao mengi na wengi wale.

Sawa yeye kaiba hela kijanja sababu ya kuto lipa deni,but ametumia hapa nyumbani, mfano amejenga Maghorofa , amefungua mashamba, mahotel,anaishi vizuri na famila yake, watu wanapata ajira. tatizo liko wapi.Pembejeo, na Building materials amenunua kwa wabongo.
Familia yake ambayo ni sehemu ya watanzania iko salama tena na furaha na amani, wengine mtapata wachumba na kuoana hapo, hamja faidi? hata akifa leo atayaacha hapa nyumbani.

Laiti Wasira angekamatwa afungwe pale tu angemiss use that fund, au angetelekeza familia, angelewa both chini na juu, au tuseme akafungua Account Ulaya. kuwafadisha wazungu.
But mwafrica kma mwafrica yeye hapendi mazuri, yamfikie japo anayatamani, mazuri ya mwenzako ni mazuri yako pia,M azuri yote yanaanzia kwa kuwaza na kufikiri, mawazo ni maombi kwa Mungu baba, bu black people wote wengi wenu mnawaza the same evils, act the sameevils. mimi tu ndo nimewaza tofauti na nyie wote.

Wahindi na Weupe wote wanaiba vitu kama makanikia, Dhahabu, Almas tena wanaviwanja vya ndege huko huko migodini wanapelaka Canada, India, Uk. mmenyamaza kimyaaaa! wakifa mali zinabaki Ulaya.

Mnashangilia, na kujisikia burudaniii kabisa, mweusi tena mhesimiwa mtanzania aliye watumikia, mwenzenu, kuitwa majina mabaya kama ya mwizi, jizi, muhujumu uchumi,.mkwepa kodi, afungwe Segerea, yaani mnafurahia ubaya ubaya tu.

Ndiyoo maana mnabaguliwa Duniani kote hampendwi na wenye akili zao. na mtakuwa hivyo ndvyo mlivyo,
msiwalaumu weupe kabisa kuwafanya mambulula.

Eti kabisaa mtu mzima ana simama na JPM kumkandamiza mheshimiwa aliyekutumikia aende kusota Segerea. ndiyo umaskini wako utakwisha au?

Hakuna hata mmoja humu ndani anaye advocate postive standing points upon this man's deed, Mi-Africa ndo mlivyo, hata kushauri njia nzurii tu ya kumsadia alipe hilo deni, ufurahie amani yake km mtu aliye kosea. kwa mfano tukimchangia Tsh. 1000/= kwa kila mwana JF, si atakuwa amelipa deni?
unafurahia Familia ya mwenzako inapo dhalilika kwa kukosa Shelter kwa sababu tu amefilisiwa, au kupelekwa Segerea. eti ili wewe upate kuwa na akili nzuri?

Hapo ujue babu zetu waliuzwa hivyohivyo utumwani, baadhi ya ndugu zao ambao walibaki Africa walicheka sana na kushangilia, walivolia moyoni, na kuswagwa kimbuzimbuzi, na muarabu tena mmoja tu, kwenda utumwani, hawakuwasaidia, wala kuwakomboa, ambao yamkini mazalia haya korofi, leo hii yako humu JF. tuanaishi nayo.

Lazima hapo mhesimiwa Wasira, na familia yake pendwa wanalia kimoyomoyo, wanaomboleza, wanaomba labda wapate huruma ya Rais ipitepite hivi.
Na kuna mweusi mwenzake, anasimama na JPM kumkandamiza wasira, tena kwa kutamka mchana kweupee, na huyu eti amesoma UDSM, chuo chetu..

Angalia sasa maajabu ya Musa Weupe wote,wanaoishi Mara na kwingineko, yaani Wazungu, Waarabu, Wahindi, hawashadadii, kumkandamiza mwafrica km Wasira.

Kwanza huyo jiwe wenu, siyo kuwa anawapenda sana ila anachukulia udhaifu wenu kupata political credit, nisifunguke sana nisije pigwa ban bure
 
Unakopa pesa bank...na sio BOT ila serikal ndyo inakuja kukudai, tena Rais ndye anakudai! Huki ni kizungumkuti...lumumba achen propaganda za kumpaisha JPM.
 
Tatizo lako unaparamiaga mambo bila kuelewa mantiki yake, naishia hapa
Sema tu umechemka sana mkuu, mantiki ipo wazi, ni Wasira alikopa mil 100 Benk na amegoma kurejesha.
Mikopo yote ipo kisheria, sasa Rais anatoaje amri kumshurutisha Wasira alipe?
Kweli Tundu Lissu alisema tuna Rais wa ajabu haijawahi kutokea halafu nimeona humu vichwa panzi wanasifia Sana uamuzi wa Rais.
Sasa tangu lini Rais akahusika na mikopo ya watu Benk? Huoni kuwa hicho ni kioja cha karne?
Au kukopa pesa Benk ni ufisadi pia?
Kubali tu kwamba umechemka kweli kweli.
 
Kumekucha!

Steven Wasira,mmoja wa wadaiwa sugu wa mfuko wa Commodity Import Support amesema hatalipa deni hilo kamwe na kwamba yeye si mmoja wa wadaiwa wa mabilioni hayo.

Wasira ambaye anakiri kukopa milioni mia moja miaka ya tisini,anasema alikuwa na makubaliano ya kulipa benki ya T.I.B, na kwamba makubaliano hayo yalifanywa wakati Mkurugenzi wa Benki hiyo,na mtuhumiwa wa ufisadi,bwana Peter Noni akiwa mamlakani.

Cha ajabu,Benki hakuna kumbukumbu za kulipa deni kama Wasira anavyosema alilipa, na hana hata barua ya Benki kuonyesha kwamba imethibitisha kwamba kalipa na hadaiwi, wasira ana maneno tu hana documents za benki kuonyesha uthibitisho kwamba hadaiwi,je mchezo ulichezwa hela ikarudi kwa wasira,hivyo Wasira anaweza kuwa ametakatisha pesa?

Muda wote anaimba "noni,noni,noni"

Je Wasira na kundi lake la awamu ya tano walikuwa wanashinikiza na kuwatisha watendaji wawafutie madeni yao kiaina? Anasema aliachana na kampuni iliyokopa akaenda kufanya siasa,sasa kwa nini Benki au yeye aambiwe na Benki aiandikie ili ifute deni wakati yeye si mtumishi wa kampuni ya SIZYA COLD STORAGE?

Wasira alikopa milioni 100 miaka ya tisini,anataka alipe hizo pesa hivyo hivyo bila riba! Amekopa miaka 30 iliyopita?!

Haiwezekani, akamatwe na apewe kesi ya uhujumu uchumi,tena anamgomea Rais wa Jamhuri ya Muungano ! Anajiamini nini huyu mtu?hajui hii ni awamu ya tano!

Asomeshwe namba,
Wewe ni mpumbavu hasa, Rais ni nani ktk Huo mkopo wa Wasira? Ndo alisaini ili Wasira apewe mkopo? Hujui kuwa Urais ni taasisi Binafsi inayojitegemea?
 
Wakubwa hawana madeni .... Sawa sawa Mr
. Wasira.
 
Linapokuja suala la kubana wabadhilifu na washenzi nakuwa na JPM upande mmoja
Katika mambo machache ambayo naweza kumuunga mkono Magufuli, hili ni moja.

Ila lisifanywe kisiasa tu.

Sijui details za kesi ya Wassira, lakini najua wazee wengi wa CCM wame abuse sana power.

Kuna jamaa mmoja alikuwa mhasibu mkubwa sana NIC (Bima).

Nilikuwa naongea naye siku moja kwenye msiba, story zikaenda, zikafika kwenye abuse of power (sijui zilifikaje, lakini marehemu Mzee Bob Makani alikuwepo karibu hapo, so no wonder).

Basi, yule mzee wa Bima akasema, kipindi cha "chama kushika hatamu", alifuatwa na Kawawa, akaombwa mkopo na Kawawa, Katibu Mkuu wa CCM, kwa niaba ya chama.

Akasema, sawa, leteni collateral, leteni documents, tutaziangalia. Kawawa akamjia juu kiaina, akamwambia, chama ndicho kilichowezesha hii kampuni ya Bima kuwa ya wazalendo, the integrity of the party is more than enough collateral kijana.

Jamaa akaona kama Kawawa anamtisha, akasema isiwe tabu, kubishana na wazee si kitu kizuri.

Akasaini mihela itolewe, Kawawa apewe.

Bada ya muda, huyu mhasibu akafuatilia lile deni kuona kama chama kinalipa, akaona chama hakilipi.

Akamtafuta sana Kawawa, akawa hampati. Siku moja baada ya kuzungushwa sana akampata.

Akamwambia, Mzee, naulizia lile deni, naona halilipwi.

Kawawa akamjibu, akamwambia "Kijana, kwani hapo kwenye shirika lenu hamna bad loans ledger ? (kitabu cha kuandika madeni ambayo hayalipiki katika mchakato wa kuyasamehe). Akajibiwa tunayo hiyo ledger. Akaambiwa tuweke humo.Hatutaki mjadala zaidi.

Jamaa akajiona bonge la bwege. Na hapo ndipo habari za lile deni zilipoishia.

Wazee wa CCM wamekula sana hela za umma katika mtindo huu, hususan nyakati za uchaguzi.

So, as much as I dislike Magufuli's style of leadership, kwenye hili, kama anafanya kwa njia iliyo fair bila visasi vya kisiasa, namuunga mkono kabisa.

Wassira atoe ushahidi kwamba alilipa deni.
 
Wewe ni mpumbavu hasa, Rais ni nani ktk Huo mkopo wa Wasira? Ndo alisaini ili Wasira apewe mkopo? Hujui kuwa Urais ni taasisi Binafsi inayojitegemea?
Povu,hiyo benki ni Mali ya Serikali,na Rais ndio Kiongozi Mkuu wa Serikali,na hizo pesa ambazo wasira kagoma kulipa ni Mali ya serikali
 
Katika mambo machache ambayo naweza kumuunga mkono Magufuli, hili ni moja.

Ila lisifanywe kisiasa tu.

Sijui details za kesi ya Wasira, lakini najua wazee wengi wa CCM wame abuse sana power.

Kuna jamaa mmoja alikuwa mhasibu mkubwa sana NIC (Bima).

Nilikuwa naongea naye siku moja kwenye msiba, story zikaenda, zikafika kwenye abuse of power (sijui zilifikaje, lakini marehemu Mzee Bob Makani alikuwepo karibu hapo, so no wonder).

Basi, yule mzee wa Bima akasema, kipindi cha "chama kushika hatamu", alifuatwa na Kawawa, akaombwa mkopo na Kawawa, Katibu Mkuu wa CCM, kwa niaba ya chama.

Akasema, sawa, leteni collateral, leteni documents, tutaziangalia. Kawawa akamjia juu kiaina, akamwambia, chama ndicho kilichowezesha hii kampuni ya Bima kuwa ya wazalendo, the integrity of the party is more than enough collateral kijana.

Jamaa akaona kama Kawawa anamtisha, akasema isiwe tabu, kubishana na wazee si kitu kizuri.

Akasaini mihela itolewe, Kawawa apewe.

Bada ya muda, huyu mhasibu akafuatilia lile deni kuona kama chama kinalipa, akaona chama hakilipi.

Akamtafuta sana Kawawa, akawa hampati. Siku moja baada ya kuzungushwa sana akampata.

Akamwambia, Mzee, naulizia lile deni, naona halilipwi.

Kawawa akamjibu, akamwambia "Kijana, kwani hapo kwenye shirika lenu hamna bad loans ledger ? (kitabu cha kuandika madeni ambayo hayalipiki katika mchakato wa kuyasamehe). Akajibiwa tunayo hiyo ledger. Akaambiwa tuweke humo.Hatutaki mjadala zaidi.

Jamaa akajiona bonge la bwege. Na hapo ndipo habari za lile deni zilipoishia.

Wazee wa CCM wamekula sana hela za umma katika mtindo huu, hususan nyakati za uchaguzi.

So, as much as I dislike Magufuli's style of leadership, kwenye hili, kama anafanya kwa njia iliyo fair bila visasi vya kisiasa, namuunga mkono kabisa.

Wassira atoe ushahidi kwamba alilipa deni.
Mwanasheria mmoja wa Taasisi ya Bima(sisemi Bima ya Afya au NIC) miaka ya karibu na chaguzi za juzi aliambiwa jambo hilo, akakataa,akapigwa zengwe,ka-resign miaka hiyo ya juzi
 
Mwanasheria mmoja wa Taasisi ya Bima(sisemi Bima ya Afya au NIC) miaka ya karibu na chaguzi za juzi aliambiwa jambo hilo, akakataa,akapigwa zengwe,ka-resign miaka hiyo ya juzi
Najua mkuu, najua haya yapo mpaka leo. Kwa sababu hawa wakuu ni ndugu zetu na tunaongea nao masahibu wanayokutana nayo makazini huko.

Wengine ndiyo maana tuliamua kusepa mapema sana kabla hatujakutana na majaribu haya ya kimfumo huko nyumbani.
 
Povu,hiyo benki ni Mali ya Serikali,na Rais ndio Kiongozi Mkuu wa Serikali,na hizo pesa ambazo wasira kagoma kulipa ni Mali ya serikali
Hata kama ni ya serikali lakini Rais hahusiki, zipo sehemu za Rais kuhusika siyo mikopo ,kwani alipewa bila utaratibu wa kisheria?
Kinachohusika kumdai Wasira ni sheria husika siyo Rais kuingilia, zipo Mahakama.
Nyie watu ni wajinga hasa.
 
Alipe deni Magufuli haangalii sura wala kujuana ,lipa deni Rais apate pesa ya kufanya miradi ya maendeleo
 
Hata kama ni ya serikali lakini Rais hahusiki, zipo sehemu za Rais kuhusika siyo mikopo ,kwani alipewa bila utaratibu wa kisheria?
Kinachohusika kumdai Wasira ni sheria husika siyo Rais kuingilia, zipo Mahakama.
Nyie watu ni wajinga hasa.
Mahakama CCM wanasema zinachukua muda mrefu, ifanyike kama ya Lissu,atajitetea akiwa gerezani
 
Wewe siyo mwizi? yaani hata kuibia tu drsn, upate marks za juu. unanyoosha vidole tu kwa wengine.

na kama hujawahi kuiba una majungu na mpaka sasa utakuwa maskini sana.
Jamii yetu ina kasoro. Imejaa wezi wanaojiita wazalendo. Mimi sio mmoja wao. Akalipe tu hela za umma. Hakuna namna.
 
Back
Top Bottom