Katika mambo machache ambayo naweza kumuunga mkono Magufuli, hili ni moja.
Ila lisifanywe kisiasa tu.
Sijui details za kesi ya Wassira, lakini najua wazee wengi wa CCM wame abuse sana power.
Kuna jamaa mmoja alikuwa mhasibu mkubwa sana NIC (Bima).
Nilikuwa naongea naye siku moja kwenye msiba, story zikaenda, zikafika kwenye abuse of power (sijui zilifikaje, lakini marehemu Mzee Bob Makani alikuwepo karibu hapo, so no wonder).
Basi, yule mzee wa Bima akasema, kipindi cha "chama kushika hatamu", alifuatwa na Kawawa, akaombwa mkopo na Kawawa, Katibu Mkuu wa CCM, kwa niaba ya chama.
Akasema, sawa, leteni collateral, leteni documents, tutaziangalia. Kawawa akamjia juu kiaina, akamwambia, chama ndicho kilichowezesha hii kampuni ya Bima kuwa ya wazalendo, the integrity of the party is more than enough collateral kijana.
Jamaa akaona kama Kawawa anamtisha, akasema isiwe tabu, kubishana na wazee si kitu kizuri.
Akasaini mihela itolewe, Kawawa apewe.
Bada ya muda, huyu mhasibu akafuatilia lile deni kuona kama chama kinalipa, akaona chama hakilipi.
Akamtafuta sana Kawawa, akawa hampati. Siku moja baada ya kuzungushwa sana akampata.
Akamwambia, Mzee, naulizia lile deni, naona halilipwi.
Kawawa akamjibu, akamwambia "Kijana, kwani hapo kwenye shirika lenu hamna bad loans ledger ? (kitabu cha kuandika madeni ambayo hayalipiki katika mchakato wa kuyasamehe). Akajibiwa tunayo hiyo ledger. Akaambiwa tuweke humo.Hatutaki mjadala zaidi.
Jamaa akajiona bonge la bwege. Na hapo ndipo habari za lile deni zilipoishia.
Wazee wa CCM wamekula sana hela za umma katika mtindo huu, hususan nyakati za uchaguzi.
So, as much as I dislike Magufuli's style of leadership, kwenye hili, kama anafanya kwa njia iliyo fair bila visasi vya kisiasa, namuunga mkono kabisa.
Wassira atoe ushahidi kwamba alilipa deni.