Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Stephen Wasria, amesema kufanya maandamano kama njia ya kutatua changamoto, kumepitwa na wakati. Wasira aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM alipokuwa mkoani Kilimanjaro katika moja ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
Wito huu unatolewa huku kukiwa na vuguvugu inayoendelea mitandaoni ya kutaka watu wajitokeze siku hiyo ya kupiga kura kwa ajili ya kufanya maandamano yatakayodai mabadiliko ya katiba. Hata hivyo, Rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan ambae pia ni mgombea urais wa CCM amewatahadharisha wananchi dhidi ya maandamano hayo na kusema vyombo vya dola viko macho.